Nukta muhimu.
Katika pita pita zangu sehemu mbalimbali na kukutana na watu wa aina tofauti nimegundua bado swala la
Nia limekuwa likieleweka vibaya miongoni mwetu.
Ni kweli hakuna ibada inayokubaliwa pasipo kuangalia nia ya mfanyaji .Moja kati ya malengo ya nia ni kutofautisha Kati ya kufanya ibada kwa ajili ya mazoea ,watu na malengo ya kidunia
na mtu kufanya kwa ajili ya kupata malipo na radhi za Allah tabaraka wataala. Vilevile kutofautisha baina ya ibada mfano funga ya Suna na faradhi ,Swala nk.
Dhana potofu kuhusu nia.
Kuna dhana imejengeka mtu kuwa na nia ya jambo fulani(la kiibada ) mfano swala ,funga nk lazima unuwie
kwa sauti tena kiarabu. Hili halipo sawa na uchunguzi wangu umebaini sababu hii imepekea wengi kuacha kuanza ibada na uvivu katika ibada na kuacha baadhi ya ibada Ktk dini.Mfano
1.Kuna ndugu yangu alikua na safari fupi akachelewa kuswali swala tatu akaswali Insha tu nikamuuliza vipi nyingine umeswali akasema sijui kunuwia swala za kulipia ikiwa umepata dharura .
2.Mwingine hata kufunga nk analeta kisingizio kua hajui kunuia.
Usahihi wake upo vipi jambo hili?
Kunuia jambo ni hali ya mtu kujua anafanya kitendo gani mfano na kwa ajili ya nani au maslahi yapi na hivi vyote haziitajii au kulazimia utamke kwa sauti na iwe kiarabu.
Na imenukiliwa "Dini ya Uislamu ni nyepesi na yeyote atakayeweka ugumu kwenye dini itamshinda"
Mfano mfupi
Nb:Sijawahi kuona hadithi sehemu imeandikwa Mtume Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) alinuia hivi wakati akifanya ibada fulani.