Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Uzi wa sehemu za gharama nafuu kulala kwa wanaokwenda kwenye saili Dodoma

Gari za Dodoma to Dar zipo mpaka saa ngapi?
Unaweza maliza usaili saa 10 jioni na ukapata gari ya kurudi Dar muda huo?
Ndio, zipo gari zinaondoka saa 11 jioni, pia zipo gari za mikoani zinazoenda Dar zinafika Dom mida hiyo
 
Hii self ya price hiyo sijui itakuwaje! Naona bei ni ndogo sana, sio zile ambazo chumba kizima kinatoa harufu kama chooni?
Iko vizuri hamna harufu.

Hiyo Guest niliwahi kukaa kwa wiki nzima wakati nafanya Induction, maana tulikuwa hatujui vituo vitakuwa wapi na hatukuweza kutafuta nyumba za kupanga.

Pia kipindi cha sahili nilikuwa nafikia pale.

Kuna room za 10k kwenye hiyo Guest ambazo sio self
 
Kama huna pesa lala kituo cha mabasi tu
Nakumbuka nilienda dom kipindi cha bunge, siku ya kwanza nikapata lodge makulu,, kesho yake nikachelewa kuchukua chumba vikajaa, nilihaha na pikipiki kusaka gesti hadi nikataka kwenda stand kuu kulala, kuja kubahatisha gesti four way,, gesti ya hovyo, vyoo vinanuka,,,
😁
 
Iko vizuri hamna harufu.

Hiyo Guest niliwahi kukaa kwa wiki nzima wakati nafanya Induction, maana tulikuwa hatujui vituo vitakuwa wapi na hatukuweza kutafuta nyumba za kupanga.

Pia kipindi cha sahili nilikuwa nafikia pale.

Kuna room za 10k kwenye hiyo Guest ambazo sio self
Gest ya kawaida dodoma, usichukue self,, vyoo vinanuka, sijui shida nini
 
Hapo kupata ni ngumu maana vyumba vingi huchukuliwa na malaya wa pale chako
Kwa uzoefu wangu, ile Guest haitumiwi sana(kwa kiasi kikubwa na wateja wa Chako ni Chako).

Nimeishi pale kwa wiki nzima, sijaona mipishano yenye kuashiria huduma ya namna hiyo.

Wateja wa pale wengi ni Madereva na tunajisajili wakati wa kuingia.

Wateja wa Chako ni Chako sijui wanatumiaga zipi, kila mara nilipokuwa natoka mapema kuelekea kwenye usahili/sehemu ya Induction nilikuwa napita pale naona wengi wao wanatoka mitaa hiyo ya chako ni chako na kubebwa na bajaj/boda kupelekwa makwao.
 
Gest ya kawaida dodoma, usichukue self,, vyoo vinanuka, sijui shida nini
Nilipokuwa nakaa mimi kipindi hicho, ni pazuri hamna harufu.

Kwingine huko ambapo sijawahi kwenda huenda ndio hali iko hivyo kama unavyosema.
 
Habari mkuu, mimi nimeitwa usaili Dodoma. Ni mgeni kabisa Dodoma.

Usaili unafanyikia Royal Village Hotel.

Naomba nisaidie guest ya bei chee ya kufikia.

Na pia kufahamu Royal Village Hotel ipo mtaa gani?
Gesti za bei ndogo zipo nyingi.Nipigie kwa 0765920855 ili nijue siku unayokuja na ikiwezekezekana ntakutumia na picha za vyumba husika,maana kesho nitakua maofisini huko kushughulikia baadhi ya watu walionipa kazi mbalimbali,hivyo ntapita na gesti za jirani na Royal,nikuchukulie hata contacts.
 
Back
Top Bottom