cocastic
JF-Expert Member
- Nov 30, 2019
- 96,456
- 156,324
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawajawah kukutongoza bibie ?Mimi sijuwi Nina bahati gan maana nashemej zangu wote wanataka nikakae kwao, Ila me ndo siwez kuish nje ya nyumban mda mrefu, labda shule tyuuiih.
Sent using Jamii Forums mobile app
Personally nakusupport na nakupongeza kwa kujitambua. Kujitambua ni mwanzo wa mafanikio yako.
Ila kama huwa unashinda nyumbani wewe ni mzigo kwasababu naamini mtembea bure si sawa na mkaa bure.
Amka fanya kazi za nyumbani ukishamaliza jichanganye town hukohuko utapata mishe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini ateseke, ashasema chakula ni kingi na shemeji yake hana noma.... pili wanapendana na mkewe hivyo hana hofu ya kufukuzwa.
Mwaka wa tatu anasubiri kupigiwa simu za intavyuu, akiulizwa huwa anasema kuna mishe anaisikilizia.... binafsi nampa kongole.
Ndugu wa mke mara nyingi wanapata mteremko... Angekuwa ndugu wa mume hapo atii pua... Kila kukicha kesi... Ajibu hapa kama hiyo nyumba ina ndugu wa shemeji yakeAmesema kwa shemeji ana amani na kila kitu anapata, ni ngumu sana kwa mtu wa hv kuwaza inje ya box maana hata kazi atakuwa anachagua na vibarua ataona sio hadhi yake. Lkn angekuwa anaishi kwa kudaiwa kodi, umeme, maji, na huku huna uhakika wa mkono kwenda kinywani, angepata shughuli ya kufanya.
Nilichojifunza katika maisha kwa miaka yangu yote 35 hapa duniani ni kwamba, anayekufanyia roho mbaya, anayekunyanyasa ndio anakufundisha maisha, ndie anakupa akili ya kutafuta any means uweze kusimama na ndie anayekupa ujasiri wa kupambana na lolote linalokuja mbele yako hata liwe gunu kiasi gani.
Hao wanaotulea na kutuonea huruma mara nyingi ndio wanatudumaza na kutufanya tushindwe kujitegemea.
Kama dada yako anauchungu na maisha yako anapenda ufanikiwe angekupa hata mtaji kidogo ukajishughulishe si wana uwezo? Lkn amekuacha mwaka wa tatu huu unamtegemea yeye na umri huo 28 kweli? Au ndio ukitaka kwenda kujitegemea anakwambia kwani hapa unakosa nini?
Maisha ni zaidi ya kula na kulala na usiogope kutoka eti utakwama, mikwamo ndio maisha yenyewe, unakwama ili akili ifanye kazi..
Jiongeze bwashee, shemeji hatongozwi... wanamgombea ili wakamle kimasihara.
Kuna vitu vingi sana vya kufanya na kujitia moyo heti umerudisha mpira kwa kipa siku utatoka kimaisha ni uboya. Tafuta shughuli yoyote ufanye hata kuuza matunda.Kutokana na hali Ngumu ya maisha na tatizo la ajira vijana wengi tumeamua kurudisha mpira kwa kipa huku tukisubilia mambo yakae sawa tujipange upya na sis tufanye maisha yetu kama awali.. Wengine wamerudisha mpira kwa wazazi wao, wengine wamerudisha mpira kwa Ndugu, ila sisi Ma Pro na Ma Legendary tumerudisha mpira kwa mashemeji zetu walipo olewa dada zetu na hatujali..
Kama ilivyo kawaida kila kitu kina kanuni, sheria na taratibu zake endapo ukizifata zitakusaidia sana jins ya ku survive kipindi hichi kigumu cha mpito. Haya ni mambo muhimu sana ya kuzingatia pindi unapo rudisha mpira kwa shemeji yako.
1. Usipige Gym. Gym inamfanya mtu awe na confidence sana hivyo kupelekea kuingilia ugomvi pindi Shem wako anapo mkata dada yako makofi.. Pia Gym hufanya kiwango cha kula kuongezeka ivyo unapo kaa kwa mtu jitahidi sana uwe una kula kiasi kama wenyeji ulio wakuta..
2. Kamwe usije ingilia Ugomvi wa dada yako na shemeji yako pindi wakikusana/ kuzozana au hata kurushiana makofi.. Jitahidi sana kubaki chumbani kwako jifanye kama hujasikia kitu.. Ugomvi wa mke na mume always unakuwa ni wa muda tu lazima watapatana.. Vip kama uliingilia? Itakuwa ndio mwisho wako kukaa kwa shemeji..
3. Kin'gamuzi kikiisha either Dstv or Azam mwambie dada yako amwambie Shemeji yako / mme wake.. Hili litafanyika kwa haraka zaidi sababu Shemeji yako atajua ni kwa ajiri ya mke wake.. Wew shughulika na mambo kama Luku zikibakia unit chache mjuze shemeji yako hii itasaidia akuone active sana mfatiliaji..
4. Siku za weekend shemeji yako akiwepo jitahidi sana usishinde sebleni kwenye Tv. Hata ukiwa seblen basi jitahidi kukaa mbali na remote.. Sababu wengi huwa wanapenda weekend kuinjoi na familia zao wew pale unahesabika kama mzigo na sio part ya familia only dada yako anakuona memba wa familia..
5. Kamwe usije kuwa shabiki wa Team tofauti na anayo shabikia Shemeji yako. Hii huwa inajenga sana chuki hivyo ili uishi kwa aman kuwa team moja na shemeji yako .. Pia jitahidi sana kumsifia sifia.. Kama ana gari pia jitahidi sana kusifia gari yake ajue ndio dream car yako hata kama ni starlet or Vitz.
6. Usiwe unaleta marafiki zako nyumbani kwa shemeji yako.. Jitahidi sana wanao wote muwe mnakutana nje uko.. Sababu shemeji yako. Mashemeji zetu huwa wanaona sisi tunao kaa kwao kama tumesha feli maisha.. Ivyo huwa wana hisi hata marafiki zetu ni wale walio feli maisha wanawaona ni wezi tu.. Hivyo jitahidi sana kutopeleka marafiki kwa nyumbani kwa shemeji yako.
7. Jitahidi kila ukikaa kimaongezi na shemeji yako mwambie kuna Interview fulani nilipiga wamesema watanipigia simu ivyo nasubilia waniite.. Hii itampa moyo sana shemeji yako atajua soon ukipata kazi utaondoka kwake na ukakae kwako..
NB: Kama kijana usione aibu kurudisha mpira kwa kipa mambo yanapo kuwa magumu sababu kila mtu na maisha yake. Maneno yapo tu binadamu huwa hakosi cha kusema.. Na always mambo huwa yanabadilika hivyi ishi maisha yako.
Hii dhana ya kutuona watu tunao kaa kwa mashemeji zetu ni watu wadhaifu ife leo, Sababu baadhi yetu tumesha pitia mambo magumu na struggle za kila aina na tumesha wai shika hela ambazo wengine mbaka mnakuja kufa haiji tokea ukazishika kwa mkupuo.
Kweli tupu aiseeNdugu wa mke mara nyingi wanapata mteremko... Angekuwa ndugu wa mume hapo atii pua... Kila kukicha kesi... Ajibu hapa kama hiyo nyumba ina ndugu wa shemeji yake
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu umenichekeshq sanaUmetisha sana aisee.. Hizi huwa nafanya pia ndio maana nimedumu sana hapa.. Huwa naamka mapema sana kabla ya mtu yeyote, napukuta gari yake , naandaa madogo wenyewe akiamka wanakuta mambo mengi yasha kamilika..
Pia ukienda matembezi usipende kurudi usiku sana mpaka wanakufungulia getiUmetisha sana aisee.. Hizi huwa nafanya pia ndio maana nimedumu sana hapa.. Huwa naamka mapema sana kabla ya mtu yeyote, napukuta gari yake , naandaa madogo wenyewe akiamka wanakuta mambo mengi yasha kamilika..
Umesahau jambo hili. Usimchunguze sana shemeji ako, anaweza kuwa anatumia hii kitu kila jioniView attachment 1374465
Sent using Jamii Forums mobile app