Washauri Wa mh. Rais hawajarudi kutoka likizo ya pasaka? Kama bado, vipi ile kamati ya maadili ya viongozi wa umma nao wapo likizo? Kama wote wapo likizoni, mkulu mwenyewe haangalii luninga akaona jinsi huyu mpendwa wake anavyomvunjia heshima na adabu?
Najua mkulu hushauriki na Tabia za MTU siyo kigezo cha uteuzi Bali uchapakazi wake ndio anaouhitaji kitu ambacho hakina uhalisia kwani unadhifu Wa MTU humtambulisha alivyo smart ubongoni! Najua ukiuapply ualimu wako kuna kitu tunaita personality au haiba ya mwalimu ambayo huanzia mavazi! Basi itumie hiyo haiba ya mwanao kumrejesha kwenye kumbi za disco akawe baunsa angalau na kuyavaa mavazi hayo aliyoyavaa Leo msibani!
Hebu hekima, busara na adabu iwe nuru na taa kwa aina hii ya viongozi kabla ya kutumia mabavu yao! Mvue hayo mavazi na madaraka yake ili angalau uitunze heshima ya uongozi wako na kuziondoa hizi sintofahamu kwa wananchi! Ana nini cha mno katika uongozi hadi umng'ang'anie hivyo?