Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Viatu na Kivuli cha Magufuli kwa Tanzania ya Samia - Kuna cha Kuhofia?

Tumekuwa sasa na matumaini ya kuwa watu-huru, matamanio ya waTanzania wengi yalikuwa hivyo bila kujali walikuwa viongozi au tuliopachikwa jina 'wananchi walio wanyonge'.

Sasa hali imebadilika kuna mwangaza unaonekana katika safari yetu ndefu iliyokuwa kizani ndani ya handaki refu kupindukia la miaka mitano iliyopita na mitano-tena tuliyokuwa tumeingizwa kupitia mchakato wa uchaguzi 2020 uliogubikwa na utata mwingi .
Mzee Mwanakijiji said: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ana kibarua kigumu. Anakabiliwa na kuridhisha pande nyingi kiasi kwamba upande wowote ambao hatouridhisha au hatoonekana kuuridhisha hautachelewa kumpinga na upande ambao utaonekana unapendelewa utachukiwa na ule upande mwingine.


Toka Maktaba sauti nyingi zilitaka kuwa watu-huru :

Mwaka 2018 mwezi Machi tarehe 3
Dr. LWAITAMA, AMVAA MAGUFULI ATAKA ADHIBITIWE
Wananchi wanataka Maendeleo ndani ya uhuru, hawataki kupokonywa uhuru wao kwa kisingizio cha Maendeleo ya Vitu

Watu hawataki kuwa mateka wa kikundi cha watu kwa kuwatisha kupitia chama dola. Chama dola siyo chama cha kweli cha kisiasa maana hakina ushawishi bali kinatumia dola kutisha
 
Tutaijua dira yake baada ya siku 100....
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Tatizo la ninyi "Watumishi wa Serikali" msiojitambua mnahisi na kufikiri kuwa Rais mzuri ni yule anayewalipa ninyi vizuri. Mnasahau ya kwamba nchi hii sio ya kwenu peke yenu. Kama mko "objective", piganieni maslahi yaliyo sawa kwa makundi yote.
Mbona hueleweki? Makundi yote yapi? Kila kundi lina watu wake, na lina wawakilishi wake. Sheria za Utumishi wa Umma ziko wazi na SIYO HISANI!
 
Hapapaswi kuwa na tofauti katika mwelekeo kati ya mama na Magufuli. Hii ni kwa sababu ataongozwa na ilani ya uchaguzi ile ile aliyoinadi pamoja na Magufuli!! Mbinu na kasi zinaweza kutofautiana lakini si majengo!
 
Watumishi wa umma tunamuangalia tu kama ataendeleza dhuluma ya mtangulizi wake, au atatenda haki! Mwaka wa sita huu! Hakuna madaraja, hakuna annual incriment, hakuna nyongeza ya mishahara.

Zaidi tu tumeongezewa makato ya Bodi ya Mikopo na rentation fees. [emoji56]

Tatizo watumishi wa umma hapa Tanzania mnajiona nyie ndiyo mnastahili kupewa nyongeza za mishahara kila siku, mnajiona nyie ndio taifa hili leni peke yenu, kila Mtanzania ana haki ktk nchi hii, acheni uninafsi wenu.Kwanza nyie ndiyo wala rushwa namba moja na wavivu mliopitiliza , hata mkiongezewa mishahara bado siyo watu wa kujituma. Mjirekebishe tabia zenu.
 
Mambo ya makundi yafutwe. Hii nchi ilishavurugwa na mambo ya makundi ya chama tawala. TUACHE!

Raisi hana wakati mgumu.
Kaanza vizuri na mengineyo. Na hahitaji kumfuata yoyote zaidi ya uzoefu, busara, hekima na weledi wake.
Hahitaji kuridhisha makundi zaidi ya kuridhisha watanzania, walio wengi, hao wachache na makundi yao potelea pote wakafie mbali.
Hajawekwa pale na mtu au kundi la watu, kawekwa na katiba.

She doesn't owe anybody! Hana deni!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Na. M. M. Mwanakijiji
(Makala hii imetoka kwenye gazeti la Raia Mwema, Jumatano Machi 31, 2021. Picha juu kutoka kwa Michuzi Blog).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan ana kibarua kigumu. Anakabiliwa na kuridhisha pande nyingi kiasi kwamba upande wowote ambao hatouridhisha au hatoonekana kuuridhisha hautachelewa kumpinga na upande ambao utaonekana unapendelewa utachukiwa na ule upande mwingine. Kama kuna mtu anadhania kuwa Rais Samia atafanya Watanzania wote tushikane mikono na kuanza kuimba kwa pamoja “Ukuti Ukuti” kana kwamba hatuna tofauti za msingi mtu huyo anajidanganya. Tofauti na mtangulizi wake Rais Samia anaingia akiwa anakabiliwa na changamoto ambazo hakuna Rais mwingine yeyote wa Tanzania amewahi kuzipata. Ni katika hili hekima, ujasiri, ubunifu, na uthubutu wake utaenda kupimwa na labda ataangaliwa kwa macho makali zaidi kuliko Rais mwingine yeyote.

Viatu vya Magufuli

Upande wa kwanza anakabiliwa kujaribu kuvivaa viatu vya kiungozi vya Magufuli. Mtu anapojaribu kuvaa viatu vya mtu mwingine anakabiliwa na changamoto; ama vitamtosha, vitambana, au vitampwaya. Kama vitamtosha bado ataangaliwa kama vimemkaa; vinaendana naye au la; kama vitambana swali ni kwa kiasi gani au vipanue au atafute vingine; na kama vitampwaya ni je anahitaji kuongeza nini ili vimtoshe au bado atahitaji kutafuta vile vinavyomtosha tu hadi atakapokuja mwingine ambaye viatu hivyo vitamtosha.

Rais Samia atahukumiwa kwanza kwa kabisa ni kwa kiasi gani ataenda kusimamia miradi mikubwa “ya kimkakati” iliyoanzishwa chini ya Rais Magufuli. Ni kwa kiasi gani mradi wa SGR (treni ya umeme) utaenda kukamilika na kusimamiwa; mradi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere, na kuhamia Dodoma. Hii ni baadhi tu ya miradi hiyo. Uzuri ni kuwa kwa vile alikuwa ndani ya serikali hii toka mwanzo mama Samia inawezekana ni mtu pekee anayeilewa na kujua ni kwa kiasi gani inahitajika na hivyo kwake inaweza isiwe ngumu kabisa kufuatilia miradi hii mikubwa, ile ya kati na midogo.

Kama tulivyoshuhudia suala la ubadhirifu, ufisadi na kutokuridhika na utendaji kazi aliouonesha siku ya Jumapili akipokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali; Rais Samia atahukumiwa pia ni kwa jinsi gani hatoacha uzembe, kubebana na kupeana “second chances” kutaendelea. Hii ina maana hatoacha wateuliwa wa Rais Magufuli ambao wanapwaya sasa hivi na labda walishaonekana wanapwaya. Je, atatakiwa asubiri hadi arudi ofisini kabla ya kuchukua hatua au atachukua hatua pale pale kwa staili ya Magufuli ya “kutumbua”. Je, tumbua yake itakuwa ni ile ya kupisha uchunguzi ili mtu achunguzwe kabla ya kumfuta mtu kazi papo kwa papo kama alivyokuwa akifanya Magufuli?

Ataangaliwa kwa jinsi gani analiongoza taifa kuelekea kujitegemea kuliko kurudi kwenye kutegemea. Je, katika hili atatumia lugha tofauti kuliko ile ya Magufuli? Je, katika kujitegemea atajaribu kulitenga taifa na dunia au atajaribu kuliweka taifa katika nafasi yake sahihi ya kushirikiana na dunia. Kwamba, kama Magufuli hatolirudisha taifa katika aibu ya kuombaomba hata kwa vitu visivyoombeka? Je, ataanza safari za kwenda duniani kujitambulisha na kuomba misaada tena? Au ataangalia kimkakati ni wapi Watanzania bado tunaweza? Na katika hili tena alikuwa chini ya mwalimu mzuri. Rais Samia aliona na kuielewa kiu ya Rais Magufuli ya kuona Watanzania wanajiamini na kuwa hawajioni wanyonge; na jinsi gani aliwahusisha Watanzania katika kutekeleza mambo mbalimbali bila kusubiri vibali vya wakubwa wa dunia.

Ni kwa sababu hiyo wapo watakaoangalia na kuona kama amevivaa viatu vya Magufuli au vimemvaa yeye; ama ameingia na viatu vyake na vikapendeza zaidi kuliko vile vya Magufuli. Akaamua kupita alikopita Magufuli lakini kwa hatua zake na kwa mwendo wake. Inawezekana akawa ametengenezewa njia nzuri zaidi ya kupita na Magufuli na yeye akaipita kwa urahisi zaidi kuliko kama mtangulizi wake asingekuwa Magufuli.

Kivuli cha Magufuli

Lakini Rais Samia pia anauamuzi wa kwake mwenyewe. Japo ameingia kuziba pengo la Magufuli na chini ya mwaka mmoja tu wa ngwe yao ya pili kwa kweli si lazima afuate kila alichofanya Magufuli. Si lazima azungumze alivyozungumza Magufuli, si lazima aoneshe ukali kama Magufuli au afanye maamuzi kama alivyofanya Magufuli. Kwa hakika kabisa japo kinadharia hapaswi kwenda nje ya Ilani na ajenda yao na Magufuli lakini pia hafungwi kuanzisha ya kwake na hata kufutilia mbali ajenda ya Magufuli. Lakini vyovyote atakavyoamua kufanya kivuli cha Magufuli kitaendelea kumfunika.

Kundoka kwa Magufuli na kumwachia Samia kunamfanya Samia aingie akiwa na jukumu kubwa la kuonesha siyo tu alikuwa Makamu lakini alikuwa Makamu aliyeweza kuwa Rais kama historia inaita hivyo. Kumuondoa Ronaldo uwanjani kunatoa nafasi kwa mchezaji wa akiba kuonesha kama anastahili kuchukua nafasi ya mchezaji huo nyota. Lakini uchezaji wote utapimwa na kuona kama anaweza kutoa mchango wa kuisaidia timu kushinda. Mama Samia anaingia kuchukua nafasi ya mchezaji nyota; ni jinsi gani ataifungia magoli timu yake na kuisadia kushinda na hivyo kujihakikishia namba ni suala la muda.

Lakini la muhimu ni kuwa si lazima afanye kazi akiwa na kivuli cha Magufuli mgongoni. Japo, anaenda kuibeba ajenda ya Magufuli si lazima aibebe mabegani kama Magu kama ana uwezo wa kuibeba kichwani. Kivuli cha Magufuli kisiwe kizuizi bali kiwe ni daraja la kuvukia kwenda anakotaka kuipeleka Tanzania. NI kwa sababu hiyo asiogope, asifikirie mara mbilimbili, au hata kujishuku endapo ataamua kufanya mabadiliko ya lazima ambayo labda Magufuli asingeyafanya. Kipimo chake sasa siyo Magufuli tena bali ni yeye mwenyewe kama Rais. Kauli yake msibani kuwa aliyesimama pale ni “Rais” itume ujumbe kwa yeyote mwenye shaka na shuku; kwamba siyo tu yeye ni Rais bali pia madaraka aliyokuwa nayo Magufuli ndiyo aliyonayo yeye leo; uwezo aliokuwa nao Magufuli aliopewa na Katiba ndio uwezo ule ule aliopewa yeye. Yeye sasa anatakiwa kutengeneza kivuli chake mwenyewe na akifanya vizuri basi atajitengenezea haki na nafasi ya kutengeneza ajenda yake ya 2025 akitaka kugombea tena.

Tanzania ya Samia

Ni wazi basi kuwa Watanzania wanapompokea Rais wao mpya wapo wenye matarajio mengi na yenye kutofautiana. Wapo ambao wanatarajia kuwa anaingia na kuwa kama Rais kutoka upinzani ambaye atafutilia mbali jina, historia, mafanikio, na maamuzi yote ya Magufuli na hivyo kutengeneza historia (legacy) yake mwenyewe nje ya Magufuli. Kwamba, akijiweka mbali na Magufuli na ajenda yao basi atakubalika zaidi na wapinzani na wakosoaji wa Magufuli. Kwamba, atake kupendwa na wale waliomchukia Magufuli.

Lakini pia anaweza akajikuta anajitahidi sana kuwa kama Magufuli na kujikuta anatengeneza maadui na wakosoaji wengi zaidi kuliko aliokuwa nao Magufuli na hivyo kuoneakana ni Magufuli 2.0. Changamoto kubwa ya Tanzania hii ya Samia ni kutafuta mizania kati ya alikotoka na Magufuli na anakotaka kwenda bila Magufuli. Je, itakuwa ni Tanzania ya namna gani? Je, watu wake watasimama vipi? Je, atatengeneza taasisi na kuinua watu kwa namna gani? Je, anatamani iwe Tanzania ya namna gani. Swali hili naamini litajibiwa siku si nyingi pale atakaposimama kulihutubia taifa na kutoa mwelekeo wa maono yake kwa taifa na tutaona atakavyoanza kuipanga serikali yake ili kutimiza maono hayo.

Kwa sasa ni wazi kuwa Watanzania bado wamegawanyika na wanasubiria kuona kama mgawanyiko wao utaendelea kuwa ni wa kudumu au utawasogeza karibu karibu au utapanua zaidi mgawanyiko huo. Kwa kweli, siwezi kumuonea wivu katika kibarua hiki. Ninachomtakia ni kila la kheri katika kuliongoza taifa letu na kuwa vyovyote atakavyokuwa historia itaweza kumhukumu si kwa jinsi gani alivyokuwa kama Magufuli au kwa jinsi gani alivyokuwa tofauti na Magufuli; atahukumiwa kwa jinsi gani aliliongoza taifa letu kuelekea mafanikio ya kweli, ubora wa maisha, kuinuliwa kwa tunu zetu mbalimbali za kitaifa kiasi kwamba ije kusemwa Tanzania ya Samia ilikuwa ni Tanzania tuliyoitarajia.

Na ili kuifikia Tanzania hiyo ni lazima tukatae mbinu, majaribio au hata jitihada zozote za kumshusha Rais Samia, kumdhoofisha au kumtendea kana kwamba si Rais “kamili” kwa sababu tu ni mwanamke. Tukatae tena kwa ukali wote unaostahili lugha zote za kinyanyasaji kijinsia ambazo nyingine zimeenea mitandaoni. Tuwakatae wale wote wanaozungumza kana kwamba wanamuunga mkono lakini wanafanya hivyo ati kwa sababu “ni mama” kana kwamba umama wake ni kitu cha kumdhoofisha. Tujue kuwa anaingia madarakani akiwa na nguvu zote kama Rais wa Tanzania bila kujali jinsia yake. Lakini pia inatupa nafasi ya kuwa na kiongozi ambaye ana mtazamo tofauti kuliko wengine na hivyo labda ataweza kuwainua pia wanawake wengi wenye uwezo ambao labda hawakupata nafasi zozote za juu za uongozi kwa sababu ya mitazamo mibaya ya kijinsia (gender biases). Lakini pia naamini atawapa nuru mabinti zetu kutamani kufikia nafasi yoyote ya uongozi wa nchi yetu na kuwa wale wote wenye nafasi za uongozi wafanye hivyo kwa weledi mkubwa zaidi bila kuonekana wanajikomba kwa mwanamme yeyote. Na kama nitakavyoonesha wiki ijayo kuna mambo ambayo naamini Rais Samia ni LAZIMA ayafanye tofauti na Magufuli.

Katika Tanzania ya Samia hakuna cha kuhofia.

Niandikie: klhnews@gmail.com
Samia anatosha kupita maelezo aisee;
Kwanza Yuko composed and relaxed....na kwa kuwa team inayomzunguka iko bomba (mpango,majaliwa na katanga)watapata wasaa wa kukunjua uwezo wao na kumsaidia kazi huku yeye akiendelea kuharmonise Mambo...utawala wake utakuwa moja ya tawala Bora kuwahi kutokea Tz.
 
...vipi kuhusu waliohujumiwa na hao jamaa, wao watapataje haki yao?.

..inahitaji mabadiliko makubwa sana ya kiuongozi, na kiutawala, ili kuweza ku-prosecute maovu yaliyofanywa na kundi la WASIOJULIKANA.

..i am trying to be realistic au kuangalia hali halisi ya mazingira yetu ni nini kinawezekana kututoa hapa tulipo.

..Trust me, wasiojulikana, na waliokuwa wakiwatuma wasiojulikana, ni watu wabaya, washenzi, na wasaliti nambari moja ktk nchi yetu.

..Mimi kwa maoni yangu sidhani kama CCM na watawala wetu wanaweza kuwashtaki wahusika wa kundi hilo. Lakini nadhani wanaweza kuacha kulitumia kundi hilo, na likaishia kimyakimya.

..Mtizamo huo ndio ulionifanya nipendekeze wahusika wa genge la WASIOJULIKANA wapangiwe majukumu mengine.
 
Mwacheni Rais Samia aongoze kwa maono yake na si vivuli au viatu vya wengine
Kumtaka afuate nyayo ni kumkwaza. Samia ana personality yake tofauti na ya mwendazake

Hawezi kutumia personality yake kufanya ya Marehemu, JK, Hayati Mkapa, Mwinyi au Hayati Nyerere!
kila zama na kitabu chake , ni wakati wake kuandika zama hizi kwa kitabu chake

Katika mambo aliyoandika Mzee Mwanakijiji moja ni sisi kuwa Taifa lililogawanyika.
Kazi ngumu mbele ya mama Samia ni kuliunganisha Taifa lilivyovurugwa na Marehemu

Marehemu aliligawa Taifa kwa namna zozote unazofikiri, iwe jinsia, ukabila, udini , hata rangi

Marehemu hakujali Utu alijali Vitu, Mama Samia arudishe hadhi , heshima na utu wa mwananchi
Kiongozi anaongoza watu si madaraja au miti, hivyo kutojali uhai na maisha ya watu si kiatu cha kuvaa

Hivi mnataka Rais Samia avae viatu vya kukataa sayansi na kuhubiri madogori na mapambio kwa gharama kubwa sana za maelefu ya maisha ya wananchi! kiatu hicho mama asikijaribu wala kukifikiri!

Rais Samia halazimiki kufuta kila kilichoachwa na Marehemu lakini analazimika kufuta mabaya aliyoacha na yaliyoliacha Taifa hili na makovu makubwa sana.

Kiongozi hapimwi kwa Vitu bali Utu. Mwendazake anapimwa kwayo ndiyo maana kipimo cha utu wake kipo mgongoni kama si kushoto. Hukumu yake imesimama katika utu licha ya vitu alivyotengeneza

Mwacheni Rais Samia aongoze kwa zama zake na aandike legacy yake kwa maono yake
 
Tatizo watumishi wa umma hapa Tanzania mnajiona nyie ndiyo mnastahili kupewa nyongeza za mishahara kila siku, mnajiona nyie ndio taifa hili leni peke yenu, kila Mtanzania ana haki ktk nchi hii, acheni uninafsi wenu.Kwanza nyie ndiyo wala rushwa namba moja na wavivu mliopitiliza , hata mkiongezewa mishahara bado siyo watu wa kujituma. Mjirekebishe tabia zenu.
Usiwe na hasira na watumishi wa umma! Unachotakiwa kufanya na wewe ni kupigania haki zako pale ulipo! Sasa kama hutaki mtumishi wa umma aongezewe mshahara au kupandishwa cheo, hizo huduma bora unazotaka kupata utapewa na nani?

Na tukiacha kazi mtahudumiwa na nani nyinyi ndugu zetu wanyonge? Tuishi kwa kupendana basi! Ila haya mambo ya kuoneana wivu na kuombeana mabaya, hayatatufikisha kokote kama Taifa.
 
Siku nyingi Sana sijasoma makala ambayo mleta mada ameandika kwa kutumia akili yake niliyoifahamu miaka mingi.Tangu Rais Magufuli (R.I.P) aingie madarakani(au labda niseme tangu Dr W Slaa alipojiengua chadema),mzee amekuwa anaandika kwa hisia zaidi kuliko hii akili ambayo inaonekana ameitumia kwenye hii makala.

Napongeza marejeo haya ya matumizi ya akili.Japo bado ninahofu kwamba,pengine tunapopata Rais asiye mkatoliki huyu mleta mada huwa ni mtumiaji mzuri wa akili yake.Anapokalia kiti mkatoliki,huyu mleta mada huwa anatumia Sana hisia kuliko akili.Natumai awamu hii atakuwa tena popular humu na atabeba tena wafuasi wake wa JF ambao walikuwa wamemtupa kwa kumuona sio 'mwenzao'!

Nimeisoma hii makala katikati ya mistari.....
 
Siku nyingi Sana sijasoma makala ambayo mleta mada ameandika kwa kutumia akili yake niliyoifahamu miaka mingi.Tangu Rais Magufuli (R.I.P) aingie madarakani(au labda niseme tangu Dr W Slaa alipojiengua chadema),mzee amekuwa anaandika kwa hisia zaidi kuliko hii akili ambayo inaonekana ameitumia kwenye hii makala.

Napongeza marejeo haya ya matumizi ya akili.Japo bado ninahofu kwamba,pengine tunapopata Rais asiye mkatoliki huyu mleta mada huwa ni mtumiaji mzuri wa akili yake.Anapokalia kiti mkatoliki,huyu mleta mada huwa anatumia Sana hisia kuliko akili.Natumai awamu hii atakuwa tena popular humu na atabeba tena wafuasi wake wa JF ambao walikuwa wamemtupa kwa kumuona sio 'mwenzao'!

Nimeisoma hii makala katikati ya mistari.....
Hapana ndio amekuwa na maandiko bora kabisa. Mimi naheshimu sana wetu kama MM Mwanakijiji wanaoweza kusimama na wanachoamini bila kujali msimamo wa wengi! Binafsi heshima yangu kwake ilifikia kiwango cha juu nyakati hizo.

Sisi wengine hatupelekwi na upepo, tunaacha akili zitupe majibu sahihi na si matumbo yetu.
 
Tatizo la ninyi "Watumishi wa Serikali" msiojitambua mnahisi na kufikiri kuwa Rais mzuri ni yule anayewalipa ninyi vizuri. Mnasahau ya kwamba nchi hii sio ya kwenu peke yenu. Kama mko "objective", piganieni maslahi yaliyo sawa kwa makundi yote.

Sure wana ubinafsi sana. Everyone deserve same and equal opportunities
 
Back
Top Bottom