Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Wazo zuri Jiji lazima lipangike liwe safi Biashara zitengewe maeneo Maalumu sio kila sehemu ni vibanda Angalia Posta Mpaka wachina Mahindi na viazi utadhani Mbagala Ofisi za Serikali Wamejaa Mama lishe shoe shines uchafu mtu
Mkuu wewe unaona uchafu, wenzako ndio mahali wanapotafuta riziki zao kwa ajili ya familia zao
 
Haaaaa Haaaaa 😂 jamani na walivo wengi. Yan walijiona wao ni jeshi
 
... safi sana! Mitaa ilichafuka mno! Wananchi watafutiwe maeneo bora na salama ya kufanyia shughuli zao badala ya hizi hadaa za kisiasa - WANYONGE!
Tayari wameshatafutiwa au watoke kwanza,
MAANA kilio chao toka zamani ni kuwa maranyinhi huwa wanapelekwa au kutengewa maeneo yasiyo na tija kwa biashara zao
Duh sijui itakuwaje
 
Kuna kijiwe fulani hivi cha kahawa huwa naendaga kunywa. Bwana hicho kijiwe kinachekesha jamani, kuna Mama ntilie kama watano hivi wamekuja kupika pika hapo, amekuja na shoe shine, wauza dawa za kiume., wachoma mishkaki hapo hapo wote hao wapo chini ya mti huo huo mmoja sema huo mti ni mkubwa
 
wanaingiza kipato cha kula na familia zao na kusogeza siku, Maisha magumu sana ila itabidi wkubaliane na hali halisi
 
Wewe ulilipokea kama dongo, badala yakulipokea in positive way,
Utafakari ni namna gani utaongeza kipato chako na kujiinua zaidi ya hapo!

Tujitahidi kuwa na mawazo chanya kadri tuwezavyo..jamani (hata mimi na jifunza)

"Sasa ndio atajua hajui"- hii sasa ni chuki

"Hawa wenye vibanda barabarani walidharau wafanyakazi wa serikalini" - hapana sio wote, dharau hailetwi na kumiliki kibanda barabarani ni tabia tu ya mtu!
 
Kariakoo njia ya mwendo kasi hakuna pakupita, ni kubanana hatari wamejaza vibanda tunapita yanapopita magari
 
Sawa mkuu
 
Wanyonge tukale wapi?.
Mtapata laana ya marehemu
Kwani mmeambiwa msiuze? Fanyeni biashara halali mahali panapofaa wateja watawafuata. Kwanza walio wengi biashara si zao wamewekwa na wakwepa kodi kwa ujira kiduchu. Acheni kudeka!
?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…