Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Washauri wengi waliomo mtandaoni ni sehemu ndogo sana ya wapiga kura,hawa ndo TL alipokuwa akisoma comment akajua atashinda asubuhi,kumbe wapiga kura wengi zaidi hawamo JF.
wengi wao ni upinzani wanatoa Ushauri ili mama akikosea wapate ajenda baadaye.
maana tangu mwendazake aende wamekosa ajenda.
wamachinga ni watz kama wengine lishughulikiwe kwa busara jambo hili.
 
Hao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
Kwani hapo waliletwa na nani si walivamia tu?? Warudi tu Machinga Complex hamna namna!
 
Endelea kujidanganya tu.

Acha vibidhaa vyako kwenye hayo mabanda uone Kama asubuhi hutakuta uchafu.

Si mrudi vijijin kwenu mkalime.
 
We inaonekana una uchungu wa kuvunjiwa nyumba mzee [emoji23][emoji23][emoji23] pole sana ila sikuingine usinunue kiwanja barabarani mkuu
Milestone ya kuvunja sheria huwa fupi sana.

Hata Kama wasipotolewa Leo siku yao yaja. Kama una kakibanda kako nakushauri ondoa maana utaratibu wa kuvunja siku hizi ni usiku kwa usiku.


Sasa endelea kukenua tu hapa na kujaza wenzio ujinga.
 
Ili machinga complex iweze kuvutia wangeweka lift za ngazi zile watu wangevutiwa kwenda sababu ya kupanda ngazi zile lakini at the same time wangeweza kununua kitu chochote.

Pia sehemu kama zile wangeweka hata vivutio kama michezo ya watoto ili kupata watu wa aina mbalimbali.
 
Hizi akili za kibavicha hatari, sasa hujui ukimbimolea kesho atakuvamie akuibie hata kandambili nyumbani kwako
Kumbe waliotoa hiyo amri ni bavicua!
 
Wameponzwa na kutandika kanga barabarani ....
 
Yaani siku zote kutatua tatizo lazima ujue mzizi wake ulipoanzia na umelielezea vizuri kabisa hili sula la Wamachinga (marching guy) na jinsi walivyo evolve mpaka leo hii tunawaona ni kero

Watu wa Dar es Salaam tunakumbuka lile jaribio la kuwaweka pale KIGOGO SAMBUSA lilivyoshindikana tena nadhani hapo hata machinga Complex bado haikuwa imekamilika..

Wamachinga hawana shida ya kutengewa maeneo.. Inahitajika ubunifu tu wa kuwaweka karibu na movements..
 
Huyo mkurugenzi anayetaka kuwatimua machinga na mama ntilie anaijua ilani ya uchaguzi ya ccm kweli? Ilani hiyo ya chama tawala imetamka wazi kuwa machinga, bodaboda na mamantilie watafanya kazi zao kando kando ya barabara yo yote mijini. Kwamba mjini tutabanana wote: matajiri na wanyonge hawa.

Huyu mkurugenzi anayekiuka ilani ya chama tawala ajiandae kutimuliwa. Kuondoka kwa JPM, Bashiru na Polepole haina maana ilani hiyo imeondoka. Asilimia 60 ya wapiga kura ni machinga, bodaboda na mama ntilie. Hawa ndiyo walichagua ilani hiyo nzuri ya ccm itakayodumu hadi 2025.
 
Wafanye hivyo kila majiji maana imekuwa uchafu na kupunguza barabara na kuleta msongamano
 
Bodaboda na machinga walilelewa vibaya,watoto vitinda mimba wa mwendazake
Mkuu Mkombengwa kwani bodaboda wanavibanda ama unajumlishia humohumo kwa sababu boda zao? Hawa machinga wapo na bado wanaendelea na biashara zao za kutembeza kwenye mabaa, stand za mabasi n.k. hawa ndio wenye jina la MACHINGA. Leo jina hili limevamiwa na mama Lishe, baa bubu (glossary), magenge ya mbogamboga na matunda. Kundi lingine linauza bidhaa za maduka badala ya kutembeza kama wamachinga wenyewe, hili ndilo lenye vibanda, na kupanga bidhaa ovyoo barabarani. Kwa sasa Jiji la Dar limejengwa vizuri sana hivyo ni lazima LISAFISHWE. Kila bidhaa iuzwe kwa mujibu wa sheria.
 
Mkuu Kerubi naungana nawe kwa hoja zako, ila tambua kuwa humu Jf wengi ni athirika wa hawa wamachinga huko barabarani, mbele ya maduka yao n.k, hivyo ni vyema proposal zako ukazipeleka kwenye ofisi inayohusika kwa hatua zaidi. Hakuna mtanzania anayependa mtanzania mwezake anyanyasike ama anyanyaswe lakini kwenye mambo yenye mashaka mashaka lazima sheria zifutwe.
 
YAANI MJI UMECHAFUKA SANA AFADHALI, SISI WAENDA KWA MIGUU TULIKUA TUNAPATA SHIDA SANA KUTEMBEA, HAKUNA NJIA YAANI.

TENA KAMA WANACHELEWA, HAWA WATU WAENDE MACHINGA COMPLEX PALE. SISI TUTAWAFUATA HUKO.
Kuna watoto ada zao zinatoka hapo, furaha Yao inatoka hapo.

Kuweni na huruma kwa watu.
 
Kwa tamaduni zetu sisi waafrika sioni haja ya kuiga miji yetu iwe kama ulaya, tunaweza kuwaiga ustarabu mwingine, ila huu wa kuwaondoa raia waliojiajiri kujitafutia mikate yao mahala ambopo wao wanahisi ni mazingita rafiki ya biaashara hili ni tatizo. Huku kwetu kuna uhaba mkubwa wa ajira hawa watu wanaweza buni kaxi zingine za kufanya kutokana na kubugudhiwa halafu mtaani kukawa kugumu.
 
Wazo zuri Jiji lazima lipangike liwe safi Biashara zitengewe maeneo Maalumu sio kila sehemu ni vibanda Angalia Posta Mpaka wachina Mahindi na viazi utadhani Mbagala Ofisi za Serikali Wamejaa Mama lishe shoe shines uchafu mtu
Hata wanao ziba biashara za watu wengine, kwa panga vitu toka dukani hadi barabarani na kuzuia biashara za wengine wapigwe marufuku
 
Yaani wametubanaaje!!! Tunakoswa koswa na magari utadhani hatuna haki kutembea pembeni maana wamejaa wao. Halafu ole wako ukanyage kitu cha mtu!!!!
Umenikumbusha kijana aliyeuawa na wamachinga kkoo baada ya gari lake kukanyaga fungu la nyanya barabarani, Iliniuma sana walivyochangia kumpiga. Sad.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…