Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Vibanda vilivyowekwa kando ya barabara Jijini Dar es Salaam kuondolewa

Hao wanaotolewa maeneo hayo wanatarajiwa kuhamishiwa wapi?. Mtihani mpya kwa wale waliochukua mikopo haswa kina mama wanaotegemea vikoba na pesa za aina hiyo.
umeelewa lakini?!? Hawajazuiwa kuendelea na shughuli zao lakini sio kujenga kibanda, akiwa na meza ambayo inahamishika no problem. lakini kusimika kibanda no.
 
Wenye nguvu ya fedha washafanya Yao tena,

Ndiyo tunajua, kila kitu lazima kiende Kwa utaratibu, Labda niulize Kwa Mleta uzi, Je Hilo gari linalotangaza halisemi mbadala wa hao wenye vibanda wanapaswa wapelekwe wapi?..
someni muelewe, hawajazuiwa kuendelea na shughuli zao walichozuiwa ni kujenga vibanda ambavyo sasa vimejengwa hata kwenye njia zza waenda kwa miguu! wawe na meaza zinazohamishika akiwa hayupo kazini pawe wazi!!!.

Unajua bwashee sheria inazuia hilo na sisi kawaida yetu tukizoea kitu tunaona kama ni haki yetu mwiso wa siku utakuta kakibanda hako kanawekewa zege mwishowe mall!

Halafu badae inakuwa nipo hapa tangu enzi zileeee! tufuate sheria tuache kwenda hovyohovyo!! Bwana mkubwa aliruhusu hilo lakini hakuigusa sheria alijua iko siku atawaondoa
 
hawa ndio walio piga kura zaidi ya milion 4 sasa acha kazi iendeleeee.
 
--- UPDATE MAY 11, 2021--

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amewataka wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuviondoa kabla ya Mei 18, 2021.

Wakati Shauri akieleza hayo, gari lenye spika za matangazo linapita katikati la mitaa ya Jiji hilo likitangaza kuhusu mchakato huo kwamba vibanda havitakiwi kuonekana kando ya barabara.

Akizungumza na Mwananchi Digitial leo Jumanne Mei 11, 2021 Shauri amesema hawajazuia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao, wanachotakiwa kufanya ni kutojenga vibanda na kuwataka wauze bidhaa zao kwenye meza ili wakimaliza iwe rahisi kuziondoa na kuacha maeneo wazi.

Amebainisha kuwa sheria ya mipango miji hairuhusu kujenga vibanda, kuwataka wafanyabiashara hao kutii agizo hilo.

“Mwisho Mei 18 kama ambavyo gari la matangazo linavyotangaza waviondoe vibanda vyao kwa sababu vingine vinajengwa hadi kwenye njia za watembea kwa miguu na barabarani na kuleta adha kwa watumiaji. Wanatakiwa watii sheria bila shuruti waviondoe wenyewe,” amesema Shauri.

MWANANCHI
Mwanjelwa1.jpg
HAMISHWA.jpg
 
Hata hizo meza hazitakiwi sehemu isiyo rasimi tena barabarani hakuna vyoo wala mabafu alafu wanauza wengine chakula, hizo meza waweke nje ya nyumba zao Kama zamani wauze huku wanapata huduma zao za choo na bafu.

Watu wa mazingira sijui wanafanya nini ofisini bila kuwachukulia hatua wachafuzi wa mazingira Kama hao wanaojirundika pembezoni mwa barabara bila huduma muhimu hivyo kugeuza barabara choo.
 
Sina la kusema yangu yenyewe yananishinda inshort kila mtu ajitetee kwa upande wake
 
Mji ukikua unachafuka kwa ujinga na ushamba...wamachinga wafanye kazi zao ila ustaarabu wa mjini nao uwepo
 
Waviondoe jamani kabla ya IDD,haiwezekani waifanye Tanzania kama Kibera
 
Hata hizo meza hazitakiwi sehemu isiyo rasimi tena barabarani hakuna vyoo wala mabafu alafu wanauza wengine chakula, hizo meza waweke nje ya nyumba zao Kama zamani wauze huku wanapata huduma zao za choo na bafu.

Watu wa mazingira sijui wanafanya nini ofisini bila kuwachukulia hatua wachafuzi wa mazingira Kama hao wanaojirundika pembezoni mwa barabara bila huduma muhimu hivyo kugeuza barabara choo.
Mkuu ni kweili kabisa inatakiwa iwe kama zamani, weka biashara yako nyumbani ambapo huduma za ufasi zipo kama choo, sehemu ya kutupia takataka n.k. Kule Mbezi Luis kingo za barabara ya Morogoro kumepandwa nyasi, nyasi hizo sasa zimekuwa ni malisho ya mbuzi, sehemu ya haja ndogo na maficho ya vibaka.
 
--- UPDATE MAY 11, 2021--

Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Jumanne Shauri amewataka wafanyabiashara waliojenga vibanda katikati ya Jiji la Dar es Salaam kuviondoa kabla ya Mei 18, 2021.

Wakati Shauri akieleza hayo, gari lenye spika za matangazo linapita katikati la mitaa ya Jiji hilo likitangaza kuhusu mchakato huo kwamba vibanda havitakiwi kuonekana kando ya barabara.

Akizungumza na Mwananchi Digitial leo Jumanne Mei 11, 2021 Shauri amesema hawajazuia wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao, wanachotakiwa kufanya ni kutojenga vibanda na kuwataka wauze bidhaa zao kwenye meza ili wakimaliza iwe rahisi kuziondoa na kuacha maeneo wazi.

Amebainisha kuwa sheria ya mipango miji hairuhusu kujenga vibanda, kuwataka wafanyabiashara hao kutii agizo hilo.

“Mwisho Mei 18 kama ambavyo gari la matangazo linavyotangaza waviondoe vibanda vyao kwa sababu vingine vinajengwa hadi kwenye njia za watembea kwa miguu na barabarani na kuleta adha kwa watumiaji. Wanatakiwa watii sheria bila shuruti waviondoe wenyewe,” amesema Shauri.

MWANANCHIView attachment 1781714View attachment 1781715
Update hiyo mzee ondoa kibanda chako
Kabisa,usije ukasema hatujakuambia
Elitwege

Ova
 
Huwa tunaacha jambo lisilo sahihi lifanyike kwa miaka mingi kisha ghafla tunakuja kulifanyia kazi.
Hivi huwa tunakuwa wapi?

Unaondoa vibanda ila unaacha meza?!
 
Back
Top Bottom