Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Vibarua kiwanda cha Bakhresa Buguruni

Itoshe kusema tu kwamba kupitia huu uzi nimejifunza kwamba nisiidharau kazi yangu ya Bodaboda maana nina degree yangu hapa inanifanya niidharau hii kazi ya Boda naona kama sistahili kuifanya kumbe kuna watu wanapigika kinoma tena kwa malipo madogo sana kwa siku nzima wakati mie kwenye boda naweza pata mara Tano ya wao [emoji119]

Maisha yamenifundisha kuwa ukitaka kuijua thamani ya neema yoyote uliyojaaliwa na M/Mungu basi jilinganishe na walio chini yako usijilinganishe na walio juu yako.
 
Hiyo 10k ipo ila sio kwa kazi kama hizo

Nadhani ukienda kwenye viwanda vya steel unaweza ukapata hadi 15k

Ila changamoto yake ni kwamba unaambiwa kila mfanyakazi unayemkuta pale ujue hiyo ni siku yake ya kwanza hapo kiwandani.

Ukishachukua malipo ya 15k ukitoka hapo utachagua mwenyewe ukapatiwe huduma kati ya Amana au Muhimbili

Au usizi home ujiuguze mwenyewe
Ni hatari mimi nilipitia hiyo changamoto nikiwa mwanza,jamaa yangu akanambia pale nyakato still kazi nje nje akaniuliza utaweza?,nikaona kanidharau nikamwambia we nipeleke,nikashangaa jamaa alivyonifikisha pale akaniachia na nauli ya kurudia[emoji1787],
Wazee nilianza vikazi vidogo dogo,kifupi zilianza kupakuliwa nondo zilizoiva sasa kazi kuzibeba uku zinatoa mvuke,weeee,nilivua gloves na nilikaa masaa matatu,wiki nzima nilikuwa sina hali[emoji706]
 
Kabisa mkuu
 
🤣 duh sio poa
 
Hizi ni kazi ambazo zinatakiwa zifanywe na marobot lakini eti wanafanya binadamu ambao home kaiacha familia inayomsubiria awaletee mkate

Inatia huzuni sana kuona vijana wapo tayari kufanya kazi yeyote ku risk hadi maisha yao ili wamudu mahitaji matatu

Miezi minne iliyopita kuna mwanangu alikatika mkono wa kulia huko viwandani

Ule mkono haukukatika into two pieces ila ulisagika kwa kiwango ambacho hata mifupa haikuweza ku survive

Saizi namuona anahangaika na wanasheria kufatilia kuhusu kulipwa fidia
 
[emoji1787] duh sio poa
Mzee ni balaa tupu[emoji1787][emoji1787].
Kwanza wale wanaozifanya zile kazi wanajuana na wamesha fanana nazo,,
Niliisi kufa kabisaa nikawa naona nyota nyota machoni umo ndani joto lake kama jehanamu alafu nondo inatoka kwenye kinu ya moto inapita tu pale kwenye maji shwaaaa[emoji1787][emoji1787] inakuja na mvuke unashika tatu tatu unazikunja,weee kidogo niwe kama wale wacheza salakasi nilivyoziinamisha tu kurudi kidogo zinipeleke angani[emoji119][emoji119]
 
Hizi ni kazi ambazo zinatakiwa zifanywe na marobot lakini eti wanafanya binadamu ambao home kaiacha familia inayomsubiria awaletee mkate

Inatia huzuni sana kuona vijana wapo tayari kufanya kazi yeyote ku risk hafi maisha yao ili wamudu mahitaji matatu

Miezi minne iliyopita kuna mwanangu alikatika mkono wa kulia huko viwandani

Ule mkono haukukatika into two pieces ila ulisagika kwa kiwango ambacho hata mifupa haikuweza ku survive

Saizi namuona anahangaika na wanasheria kufatilia kuhusu kulipwa fidia
[emoji26][emoji17]ni uzuni sana zile kazi ni ngumu sana mimi nilikaa masaa matatu tu wala sikuomba ata mia mzee.
 
Elfu 4 kiwandani!
Kwa hiyo mama ntilie wanawalipa vizuri wafanyakazi wao kuliko hao matajiri [emoji15]
Sio efu 4 tu, sometimes hiyo hiyo unayoiona ndogo unaweza ukadhulumiwa usiipate hata kuipata

Hiyo 4k watu wanaikeshea usiku kucha tena kwa sheria ngumu na bado watu wanazisaka hizo ajira na bado wanakosa

Na kuna muda wanawake wanatoa hadi rushwa ya ngono ili waipate.

Njoo kwa Mo pale vingunguti mida ya asubuhi angalia getini namna watu wanavyo jishusha kuomba kibarua
 
Hizi ni kazi ambazo zinatakiwa zifanywe na marobot lakini eti wanafanya binadamu ambao home kaiacha familia inayomsubiria awaletee mkate

Inatia huzuni sana kuona vijana wapo tayari kufanya kazi yeyote ku risk hafi maisha yao ili wamudu mahitaji matatu

Miezi minne iliyopita kuna mwanangu alikatika mkono wa kulia huko viwandani

Ule mkono haukukatika into two pieces ila ulisagika kwa kiwango ambacho hata mifupa haikuweza ku survive

Saizi namuona anahangaika na wanasheria kufatilia kuhusu kulipwa fidia
dah inasikitisha
 
Habarini ndugu wana JamiiForums,

Hivi kiwanda cha Bakharesa pale Buguruni ni uhakika kupata kazi ya kibarua ukiwa na barua ya utambulisho wa makazi?

Na hivi wanalipa kwa siku au wiki?
Achana na kazi za viwandani hazina maslahi,chukua elfu 20 au 30 yako nenda kariakoo kanunue dawa za mbu,au pipi , au vidawa vya fungus au kujichua uza mtaani utakuja nishukuru achana na hizi kazi za utumwa
 
Hiyo 10k ipo ila sio kwa kazi kama hizo

Nadhani ukienda kwenye viwanda vya steel unaweza ukapata hadi 15k

Ila changamoto yake ni kwamba unaambiwa kila mfanyakazi unayemkuta pale ujue hiyo ni siku yake ya kwanza hapo kiwandani.

Ukishachukua malipo ya 15k ukitoka hapo utachagua mwenyewe ukapatiwe huduma kati ya Amana au Muhimbili

Au usizi home ujiuguze mwenyewe
Umenichekesha sana km mazuri vile
 
SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo[emoji28].Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012
Watu mna nn lkn mnachekesha sana dah ,eti sitosahau siku nilipotaka kufa pale kiwandan
 
Wanalipa elfu nne hadi tatu then Kazi ni kubeba viroba vya ngano kilo 50 na 25 Kuanzia asubuhi Hadi jioni na pia night shift hipo it about fucking job huyo Bakhressa Ni mpuuzi mmoja. Including Mo dewij and so called matajiri uchwara
Mtu yeyote bila kujali elimu , umri, na hali yake ya maisha anayekubali kutumikishwa hivyo kwa ujira wa elfu 4 basi hana akili kabisa.
 
SITOSAHAU SIKU NILIPOTAKA KUFA PALE KIWANDANI

Ilikua mapema mwaka jana nilipitia kipindi kigumu sana baada ya kuyumba kiuchumi na degree yangu mkononi ikanilazimu kujizima data na kutafuta kazi yoyote iwe rasmi au isiwe rasmi.Nikazama zangu jf ndipo nikapata muongozo wa kwenda kiwanda cha unga kwa kurubuniwa kwamba kwa siku malipo inafika hadi buku 8 nikajipa. moyo..

Basi nikafata tafatibu zote siku ya pili nikaenda na barua ya mtendaji then nikaambiwa siku ya pili usiku nikaanze kazi.Basi bwana nikazama zangu pale mida ya saa 1 jioni nikawakuta wenzangu wapo tayari wanasubiri kuanza kazi.Wakagawa msosi pale ndani kila mtu sahani ya wali(upo kama makande) na maharage na ndizi mbivu.Kwa kua ni siku ya kwanza nikawa na uoga uoga wa kula ule msosi na niliogopa kuja kukatwa kwenye malipo[emoji28].Jamaa wakawa wananishangaa huyu msela vipi huu msosi ni lazima kuchukua haijalishi unataka au hutaki.Basi kuna jamaa akasema chukua nipe mm nitakula,wakawa wanagombania nipe mim nipe mimi.Basi nikachukua ule msosi nikampa jamaa mmoja akala na wa kwake.

Kimbembe kilianza baada ya masaa mawili viroba vilipoanza kushika toka kwenye vinu vinashuka kama mvua na vinu vipo vya kutosha mule ndani.Ili kusubiria viwe vingi ndio kazi ianze wale jamaa wakasema tuchezeni boli humu ndani(mpira wa makaratasi).Basi tukagawana huku na huku tukaanza kucheza mpira.Katika harakati za kuucheza ule mpira nikajibamiza vibaya sana kwenye kinu kipo kama upinde afu kule mbele kama wembe kwa makali yake.Ghafla bin vuu nikajikuta nipo chini nimezungukwa na watu kibao damu zinavuja kama kuku katoka kuchinjwa..Aisee nilijua leo ndio siku yangu siwezi kutoboa maana nilipasuka katikati ya kichwa.Wakaniinua pale sina hata nguvu wakasema nikapumzike pale kazi inataka kuanza.Nilishindwa coz damu zilikua zinavuja sana kuna jamaa akanielekezaa bafu akasema nikaoge ili niwe sawa.

Nilijivuta nikaenda kuoga kule bafuni maji yote yalijaa damu tu yani ili siku ilikua ndio bye bye sema Mungu hakupanga tu.Nikarudi kule ndani jamaa ndio wanagawana watu kwa makundi waanze kazi.Cha ajabu na mimi nikaitwa nikapangiwa kundi nibebe viroba.Nikawaeleza siko sawa damu zinavuja sana lakini hakuna aliyeelewa.Wakasema humu ndani ni lazima kila mtu afanye kazi.Kazi ikaanza nikaambiwa na mm nibebe kichwani zile kilo 25 kwa 50 yena viwili trip moja.Ilikua ngumu sana kubeba lakini sikua na jinsi nikajaribu tripu moja nakashindwa kichwa kilikua kinauma sana.Wakanibadilisha section wakasema niwe nawapakia watu kichwani wenyewe wanaita kijiko,yani unabeba viroba viwili pale chini na kumpa mtu kichwani.Nimefanya mara moja tu kuna jamaa akanigusa pale kichwani na kiroba basi damu zikaanza upya kutoka nikaamua kuacha nikasema liwalo na liwe cha kufia nini.

Basi nikatoka pale nikaenda nje kukaa toka ile saa 4 mpaka saa 12 asubuhi jamaa wanabeba tu vile viroba.Walikua kama 30 hivi lakini viroba walivyobeba ni zaidi ya 6,000 yani kila mmoja kama mia 2 hivi.Asubuhi ya saa 1 tukaitwa wote kwenye mgao wa pesa.Kaja kiongozi wao akasema leo kazi hamna hivyo kila mtu atapata elfu 2,aisee nilichoka mwili na akili yani kazi yote ile mtu alipwe elfu 2.Kuna watu walikua wanapinga mm kupewa ile elfu 2 kisa sijafanya kazi.Sema jamaa akanipa ile buku 2 akasema ukatibiwe.Nimetoka pale naona kama ndoto nikarudi zangu geto ile pesa nikafanya nauli sikubakiwa hata na senti..

Nimefika home kichwa chote kimeloa damu na nimepasuka vibaya sana.Sikua na pesa hivyo nikachukua chumvi na beseni nikaanza kujisafisha huku nikipata maumivu makali sana.Sikwenda kabisa hospitali hadi leo hii na nilipona kwa uwezo wa Mungu baada ya mwezi kupita.Nashukuru hivi sasa nipo sehemu nzuri japo sio sana ila sio kama mwanzo.Leo nilipita ile njia ya kiwandani nikakumbuka kuleta kisa hiki.
View attachment 2484012
Pole sana kiongozi
 
Hiyo 10k ipo ila sio kwa kazi kama hizo

Nadhani ukienda kwenye viwanda vya steel unaweza ukapata hadi 15k

Ila changamoto yake ni kwamba unaambiwa kila mfanyakazi unayemkuta pale ujue hiyo ni siku yake ya kwanza hapo kiwandani.

Ukishachukua malipo ya 15k ukitoka hapo utachagua mwenyewe ukapatiwe huduma kati ya Amana au Muhimbili

Au usizi home ujiuguze mwenyewe
Vipi huko chuma kinaua?
 
Shukran sista
Hii kazi nilishaifanya ilinifaa sana kuingiza elfu 15 ni rahisi sana na hamna sheria za kukubana sijui ingia kazini saa ngapi no ,hakuna raha duniani km kujiajiri ila hii biashara ya kununua vitu vidogo kariakoo na kuvizungusha kwenye maduka ya mangi kwa bei ya jumla inalipa unachukua vitu km dawa ya mbu pipi, biscuit superglue nk ukienda siku ya kwanza ya pili utapata idea mpya uongeze nn all the best
 
Back
Top Bottom