Vibarua viwandani au part time job kwa hapa Dar es Salaam zinapatikana wapi?

Vibarua viwandani au part time job kwa hapa Dar es Salaam zinapatikana wapi?

Duuuh Jah asaidie kwa kweli, hali n mbaya sana
 
Mungu akupe hitaji la moyo wako...amini nakuambia haupo peke yako...tupo vijana wengi tunaopitia kwenye hali kama yako kikubwa ni kuto kukata tamaa tu.
 
Huo ushirikina kabsa (negative beliefs).....afu anamwambia mwenzake awe positive...

Sio ushirikina hata kidogo.

Hata Kwenye Biblia chumvi imeandikwa.

2 Wafalme 2:21 BHN

Elisha akaenda kwenye chemchemi ya maji, akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa; tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba.”

Neno rahisi ni kuwa Chumvi ilitumika kutakasa yale maji.

And for sure this is not negative beliefs .
 
Kuna graduates walifungua biashara kisha wakafilisika. Hawa nao unawaambiaje?
Ndo maana tunamkumbuka Jk...Kuna graduates fulani hapa SUA walipigwa tafu na jk...Sasa hivi ni mamilionea...!nakumbuka walipewa ardhi ya kutosha na mheshimiwa...! marais Mengine yamebaki kuua kuua raia tu..kufeli kupo mkuu hiyo haikwepeki...ni kusimama na kuanza upya
 
Mku ni wazo zuri sana
 
Ni muda sasa nimekuwa natafuta kazi zilizo za professional yangu na zisizo zangu Ila kikubwa nina uwezo wa kufanya kazi yoyote ile halali na ambayo inahitaji skills za kawaida na hata zile complicated maana naamini hamna kinachoshindikana ukiamua. Sasa tatzo huja hapa.

Nmehudhuria interview 16 mpaka sasa na kufika mpaka 10 Bora lakini mwishoni hii kitu inaitwa connection na kujuana inanifanya naishia kuwa na uzoefu mwingi wa kujibu maswali ya interview bila kuwa na mafanikio ya kazi.

Niseme Jambo moja kama wewe umetoka familia au ukoo ambao wewe ndo inahitaji ufanikiwe ili utengeneze hyo connection kwa wengine, basi kazi unayo maana nchi imegubikwa na rushwa za ngono na kujuana hadi sisi tunaotokea familia za kawaida hatupati haki ya kusikilzwa pamoja na uwezo au vipawa tulivyo navyo.

Kuna muda natamani nifanye biashara lakini nakumbuka lengo la kutafuta ajira pia ni kutaka kupata mtaji utakaoniwezesha kujiajiri ili nije nipambane na hii kitu sabu inauma sema hatuna pakwenda hadi inafika hatua inatubidi tukimbie mazingira tulioishi ili tusiwakatishe tamaa wadogo zetu wanaoaminishwa kupitia Elimu maisha yao yatabadilika, kwahiyo wakiwa wanatuona kaka zao tupo mitaani hatuna tunachofanya na ikiwa miaka kadhaa nyuma waliambiwa tupo vyuoni tunasoma na ikajulikana hivo kuwa sisi ni wasomi na mbaya zaidi wapo walioweka nia ya kutaka kufika hapa nilipo mimi.

Sasa je, wakajua uhalisia wa haya ninayopitia nani atapata moyo wakuendelea na Elimu?

All in all Kuna mafundisho mengi sana napitia japo najua ipo siku ntahitimu lakini nkifikiria pesa iliyowekezwa kwa shida na wazazi wangu ili mimi nisome wakijua ntawasaidia kulea wadogo zangu kumbe nimerud kuwa mzigo tena kwao.

Samahani kwa nitakayemuudhi na kwa aliye na wakati kama wangu ajipe moyo asikate tamaa kwani haya yote yana mwisho.
Mkuu tupo wengi kama wewe huu mwaka wangu wa tatu mtaani. Interview kama zote hamna hata moja nimefanikiwa. Inaumiza sana sana
 
Sio ushirikina hata kidogo.

Hata Kwenye Biblia chumvi imeandikwa.

2 Wafalme 2:21 BHN

Elisha akaenda kwenye chemchemi ya maji, akatupa chumvi hiyo ndani na kusema, “Mwenyezi-Mungu asema hivi: Nimeyafanya maji haya kuwa yenye kufaa; tangu sasa hayatasababisha vifo au kutoa mimba.”

Neno rahisi ni kuwa Chumvi ilitumika kutakasa yale maji.

And for sure this is not negative beliefs .
Soma vzur hilo andko lako...apo ni Mwenyez Mungu ndie aliye yafanya maji kuwa yenye kufaa...

Sasa apo ni nguvu za Mungu na sio chumvi...ni swala la uelewa tuuh

Sasa ukimwambia mtu akaogee chumvi ili atao mikosi huoni unaipa chumvi nguvu badala ya Mungu,na hyo ndo shirki yenyewe.

Ni bora ukaiamini nguvu yako mwenyewe kuliko nguvu ya kitu....

But anyway a man become what he thinks about most of time...
 
Ndo maana tunamkumbuka Jk...Kuna graduates fulani hapa SUA walipigwa tafu na jk...Sasa hivi ni mamilionea...!nakumbuka walipewa ardhi ya kutosha na mheshimiwa...! marais Mengine yamebaki kuua kuua raia tu..kufeli kupo mkuu hiyo haikwepeki...ni kusimama na kuanza upya
Mimi ninaye mjomba wangu ambaye biashara zake kubwa sana ilikufa enzi za JK. Huyu pia unasemaje?
 
Soma vzur hilo andko lako...apo ni Mwenyez Mungu ndie aliye yafanya maji kuwa yenye kufaa...

Sasa apo ni nguvu za Mungu na sio chumvi...ni swala la uelewa tuuh

Sasa ukimwambia mtu akaogee chumvi ili atao mikosi huoni unaipa chumvi nguvu badala ya Mungu,na hyo ndo shirki yenyewe.

Ni bora ukaiamini nguvu yako mwenyewe kuliko nguvu ya kitu....

But anyway a man become what he thinks about most of time...
Wejamaa ulichofanya ni kuzungushazungusha lugha tu hapo kwani chumvi ya bahari kaiweka nani si Mungu...akisema aoge chumvi atoe nuksi hapo kaitakasa chumvi kivipi, sawa na kusema
1)soma uwe na maisha mazuri (je tumeitakasa elimu)
2)kula matunda upate afya (je limetakaswa tunda)

Kilichopo ni Mungu anatenda kupitia kisababishi (chumvi, matunda, elimu nk) sasa unapotamka sentensi humtaji Mungu ila Lawa ya ulimwengu ukitaja chochote basi nyuma yake umemtaja Mungu sasa ukisema umtaje Mungu utahitajika kumtaja kila sentensi.

Ni kwamba umechengesha lugha tu.
 
Back
Top Bottom