Ni muda sasa nimekuwa natafuta kazi zilizo za professional yangu na zisizo zangu Ila kikubwa nina uwezo wa kufanya kazi yoyote ile halali na ambayo inahitaji skills za kawaida na hata zile complicated maana naamini hamna kinachoshindikana ukiamua. Sasa tatzo huja hapa.
Nmehudhuria interview 16 mpaka sasa na kufika mpaka 10 Bora lakini mwishoni hii kitu inaitwa connection na kujuana inanifanya naishia kuwa na uzoefu mwingi wa kujibu maswali ya interview bila kuwa na mafanikio ya kazi.
Niseme Jambo moja kama wewe umetoka familia au ukoo ambao wewe ndo inahitaji ufanikiwe ili utengeneze hyo connection kwa wengine, basi kazi unayo maana nchi imegubikwa na rushwa za ngono na kujuana hadi sisi tunaotokea familia za kawaida hatupati haki ya kusikilzwa pamoja na uwezo au vipawa tulivyo navyo.
Kuna muda natamani nifanye biashara lakini nakumbuka lengo la kutafuta ajira pia ni kutaka kupata mtaji utakaoniwezesha kujiajiri ili nije nipambane na hii kitu sabu inauma sema hatuna pakwenda hadi inafika hatua inatubidi tukimbie mazingira tulioishi ili tusiwakatishe tamaa wadogo zetu wanaoaminishwa kupitia Elimu maisha yao yatabadilika, kwahiyo wakiwa wanatuona kaka zao tupo mitaani hatuna tunachofanya na ikiwa miaka kadhaa nyuma waliambiwa tupo vyuoni tunasoma na ikajulikana hivo kuwa sisi ni wasomi na mbaya zaidi wapo walioweka nia ya kutaka kufika hapa nilipo mimi.
Sasa je, wakajua uhalisia wa haya ninayopitia nani atapata moyo wakuendelea na Elimu?
All in all Kuna mafundisho mengi sana napitia japo najua ipo siku ntahitimu lakini nkifikiria pesa iliyowekezwa kwa shida na wazazi wangu ili mimi nisome wakijua ntawasaidia kulea wadogo zangu kumbe nimerud kuwa mzigo tena kwao.
Samahani kwa nitakayemuudhi na kwa aliye na wakati kama wangu ajipe moyo asikate tamaa kwani haya yote yana mwisho.