Vibarua viwandani au part time job kwa hapa Dar es Salaam zinapatikana wapi?

Vibarua viwandani au part time job kwa hapa Dar es Salaam zinapatikana wapi?

Ni muda sasa nimekuwa natafuta kazi zilizo za professional yangu na zisizo zangu Ila kikubwa nina uwezo wa kufanya kazi yoyote ile halali na ambayo inahitaji skills za kawaida na hata zile complicated maana naamini hamna kinachoshindikana ukiamua. Sasa tatzo huja hapa.

Nmehudhuria interview 16 mpaka sasa na kufika mpaka 10 Bora lakini mwishoni hii kitu inaitwa connection na kujuana inanifanya naishia kuwa na uzoefu mwingi wa kujibu maswali ya interview bila kuwa na mafanikio ya kazi.

Niseme Jambo moja kama wewe umetoka familia au ukoo ambao wewe ndo inahitaji ufanikiwe ili utengeneze hyo connection kwa wengine, basi kazi unayo maana nchi imegubikwa na rushwa za ngono na kujuana hadi sisi tunaotokea familia za kawaida hatupati haki ya kusikilzwa pamoja na uwezo au vipawa tulivyo navyo.

Kuna muda natamani nifanye biashara lakini nakumbuka lengo la kutafuta ajira pia ni kutaka kupata mtaji utakaoniwezesha kujiajiri ili nije nipambane na hii kitu sabu inauma sema hatuna pakwenda hadi inafika hatua inatubidi tukimbie mazingira tulioishi ili tusiwakatishe tamaa wadogo zetu wanaoaminishwa kupitia Elimu maisha yao yatabadilika, kwahiyo wakiwa wanatuona kaka zao tupo mitaani hatuna tunachofanya na ikiwa miaka kadhaa nyuma waliambiwa tupo vyuoni tunasoma na ikajulikana hivo kuwa sisi ni wasomi na mbaya zaidi wapo walioweka nia ya kutaka kufika hapa nilipo mimi.

Sasa je, wakajua uhalisia wa haya ninayopitia nani atapata moyo wakuendelea na Elimu?

All in all Kuna mafundisho mengi sana napitia japo najua ipo siku ntahitimu lakini nkifikiria pesa iliyowekezwa kwa shida na wazazi wangu ili mimi nisome wakijua ntawasaidia kulea wadogo zangu kumbe nimerud kuwa mzigo tena kwao.

Samahani kwa nitakayemuudhi na kwa aliye na wakati kama wangu ajipe moyo asikate tamaa kwani haya yote yana mwisho.
Mkuu pole sana asee, but nikwambie kitu kaa in touch na Mwenyezi Mungu usikate tamaa ukamuacha, pigana vita huku ukimtanguliza yeye mbele, iko siku hitaji lako utafanikiwa
 
Acha Bro. Ni hatari sana! Mpaka tunaiacha hii Adhri tunapitia meng sana binadamu
Wote tuko hivo usifikiri uko peke yako mkuu, huku kwenye ajira nako ni kizungumkuti hela haitoshi kiasi kwamba kama una roho ndogo unakata tamaa

Kikubwa ni tunatafuta mitaji tuu
 
Unakosa confidence kabisa.... kama ni mwanaume ndio hata gf inabidi upotezee kwa maana utapigwa matukio mara mbili... kupasuliwa moyo na kukosa hela
Ni kweli kabisa, kukosa hela ni adhabu balaa
 
Ukiwa huna hata shilingi hata watu unawaogopa kuchangamana nao yaaan[emoji848]
Nalo ni tatizo witness...unaweza dhani ni wewe tu huna hela kumbe mpo wengi kwenye kundi Hilo unalohofu!>ni kutoka tu my dear na kujimix ..yaani hizi connection tunazoziongeleaga ndo ziko huko nje.. ni kutoa hofu..juzi nilikua idle Sana nimekaa tu nikasema nikamchek mshikaji fulani Kuna ishu anisaidie..ile kuzurura naye mjini nikajikuta napata kakoconnection....kukaa ndan na kijifungia ni Kama dhambi !
 
Nalo ni tatizo witness...unaweza dhani ni wewe tu huna hela kumbe mpo wengi kwenye kundi Hilo unalohofu!>ni kutoka tu my dear na kujimix ..yaani hizi connection tunazoziongeleaga ndo ziko huko nje.. ni kutoa hofu..juzi nilikua idle Sana nimekaa tu nikasema nikamchek mshikaji fulani Kuna ishu anisaidie..ile kuzurura naye mjini nikajikuta napata kakoconnection....kukaa ndan na kijifungia ni Kama dhambi !
Ila kweli kukaa ndani nako mizinguo, unawaza kujiua tu, Bora utoke utapata chochote hata idea si lazima hela
 
Usema kweli wadada wengi tuko hivo, mwanaume kama hana hela anakuwa hadamshi asee

Huu ni uhalisia sio kupretend

Mimi Kama men ni fighter na kipindi hicho Hana hela Wala siwazii...Ila huna hela alafu ni mvivu unapenda kitonga....alafu Mimi nahangaika wewe upo tu umekamatia remote mpira na wewe. .ah mapema sana
 
Mimi Kama men ni fighter na kipindi hicho Hana hela Wala siwazii...Ila huna hela alafu ni mvivu unapenda kitonga....alafu Mimi nahangaika wewe upo tu umekamatia remote mpira na wewe. .ah mapema sana
Ha ha ha, mi nimkute nazo asee, mambo sijui anafight nah, apambane apate tukutane mezani[emoji39][emoji39][emoji1787][emoji28]
 
MMhh hapana aisee..ni Bora kugangamala Sana kabla batch nyingine hazijatoka..yaan ule mwaka unaomaliza piga ua galagalza hakikisha umepata pakujishikiza..
Ni kweli Ila dada yngu uku vyuoni wanafunz wengi tunajisahau Sana,tuna kesho usku na mchana kupambana na ma GPA yaani mtu hataki akose ata kipindi class....hataki kuangalia upande wa shilingi.

apo ndo utakuta mtu kamaliza chuo ana GPA ya first class,akikosa ajiri utamuonea huruma hajui wapi pa kuingilia wapi pa kutokea....coz muda mwingi ameupoteza kumtengeneza GPA ya ajira
 
Back
Top Bottom