Kuna kitu kimoja ambacho niligundua kipindi nipo juu ya mawe ni kwamba watanzania wengi ambao wana elimu ya juu hawana ujuzi wa shughuli za kawaida zinazoweza kuongoza kipato. Mtaji ulikua umekata nikapita sehemu wanapika chapati nzuri hatari nilipokula nikapata wazo kwamba ningependa kufanya ile kazi .
Siku iliyofuata nilirudi pale nikamuomba bosi nijifunze Ile kazi kwa kubembeleza sana,aliguswa nikaanza siku hiyo hiyo. Baada ya mwezi mmoja wa free labor kwake nikaondoka na ujuzi wangu nikaenda kufungua kijiwe changu cha jiko la mkaa. Sikuishia hapo nikawa naenda internet cafe maaana sikua na smartphone kucheki videos za kutengeneza sambusa,maandazi,half cakes nk.
Nikaongeza bidhaa kidogo kidogo nikawa napata hela ya kula pamoja na changamoto nyingine. Brother nakuomba give a try kuingia kwenye shughuli za utafutaji kivingine,usione aibu na hiyo degree wakati ukifika itatumika inavyostahili. Kama unamiliki smartphone sidhani kama utashindwa kununua jiko la mkaa,frying pan,meza ,dishi nk.
Kuna wakati mambo yalikua tight ikabidi nimuombe mtu mwenye duka niwe napikia mbele ya ofisi kwa malipo ya chapati 2 kila siku asubuhi,baadae alinielewa akawa ananunua kwa sababu aliguswa na ile spirit yangu ya kutokata tamaa . Zunguka na kutazama wapi unaweza ukaanzia ukipata ujuzi,aibu tupa kule hata mimi ni X- diaspora,X-machinga wa vitafunwa bado naendelea na maisha. Kila la heri