A
Anonymous
Guest
Sisi ni vibarua wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Idara ya Mazingira na Bustani, tunaomba kuwasilisha malalamiko yetu kuhusu kuchelewa kwa malipo ya mishahara.
Kwa muda sasa, vibarua wa jiji tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya mishahara kuchelewa kulipwa. Mshahara wetu ni Shilingi 150,000 kwa mwezi, lakini hadi leo tarehe 16 Julai 2026 bado hatujalipwa mshahara wa mwezi Juni.
Hali hii imekuwa changamoto kubwa kwa vibarua wengi ambao wanategemea kipato hicho kwa ajili ya mahitaji ya msingi ya maisha.
Tunadai kuwa tatizo hili limekuwa likijirudia mara kadhaa ndani ya kipindi cha takribani miaka miwili ya uongozi wa Mkurugenzi wa sasa. Tunapojaribu kufuatilia suala hili kwa viongozi wa idara, hatupati majibu ya kueleweka, na baadhi yetu tunaishi kwa hofu ya kufukuzwa kazi tunapouliza kuhusu stahiki zetu.
Tunaomba uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga na mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha vibarua wanapata mishahara yao kwa wakati pamoja na majibu ya wazi kuhusu changamoto hii.