KERO Vibarua wa Halmashauri ya Jiji la Tanga idara ya mazingira na bustani, walalamikia kuchelewa kwa mishahara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sisi ni vibarua wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Idara ya Mazingira na Bustani, tunaomba kuwasilisha malalamiko yetu kuhusu kuchelewa kwa malipo ya mishahara.

Kwa muda sasa, vibarua wa jiji tumekuwa tukikabiliwa na changamoto ya mishahara kuchelewa kulipwa. Mshahara wetu ni Shilingi 150,000 kwa mwezi, lakini hadi leo tarehe 16 Julai 2026 bado hatujalipwa mshahara wa mwezi Juni.

Hali hii imekuwa changamoto kubwa kwa vibarua wengi ambao wanategemea kipato hicho kwa ajili ya mahitaji ya msingi ya maisha.

Tunadai kuwa tatizo hili limekuwa likijirudia mara kadhaa ndani ya kipindi cha takribani miaka miwili ya uongozi wa Mkurugenzi wa sasa. Tunapojaribu kufuatilia suala hili kwa viongozi wa idara, hatupati majibu ya kueleweka, na baadhi yetu tunaishi kwa hofu ya kufukuzwa kazi tunapouliza kuhusu stahiki zetu.

Tunaomba uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga na mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha vibarua wanapata mishahara yao kwa wakati pamoja na majibu ya wazi kuhusu changamoto hii.
 
Sisi ni vibarua wa Halmashauri ya Jiji la Tanga tunaohusika na usafi wa mazingira. Tunaomba msaada kufikisha malalamiko yetu kuhusu kucheleweshwa kwa malipo yetu.

Tunalipwa shilingi 150,000 kwa mwezi, lakini mara nyingi hatulipwi kwa wakati. Hadi sasa bado hatujapokea malipo ya mwezi wa sita, jambo linalotuweka katika hali ngumu ya maisha.

Tunaomba uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ulifanyie kazi suala hili na kuhakikisha tunalipwa kwa wakati ili tuweze kumudu mahitaji yetu ya kila siku.
 
Pamoja Na Kuripoti Mara Kadhaa Juu Ya Adha Na Changamoto Tunazopitia VIBARUA Wakusanya Ushuru, Wazoa Taka, Watunza Bustani NK Ndani Ya Halmashauli Hii Ila Bado Tumefumbiwa Macho Malipo Ya Mwezi Wa 7 Mpaka Sasa Tarehe 1 Mwezi Wa 9 Hatujalipwa Licha Ya Gharama Za Maisha Kupanda Ila Viongozi Wanatuchukulia Poa Tu, Naishishi Vipi Kwa Malipo Ya 150,000 Na Ikiwa Sina Muda Wala Tarehe Maalum Yakuyapata Hayo Malipo??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…