Vibendera vya Israel kwenye magari ya Wabongo

Vibendera vya Israel kwenye magari ya Wabongo

Wakuu heshima kwenu.

Naomba tu kuuliza japokuwa najua kufuatilia mambo ya watu sio mchongo wala nini.

Huwa naona vibendera vya taifa la Israel kwenye magari ya watu ambao naamini kabisa ni Wabongo wenzetu.

Sasa wakuu naomba tu kuuliza what is the motive behind this? kunakuwa na affiliation gani na hili Taifa la Israel?

Au ni Waisraeli weusi wanaoishi bongo?
Mkuu, Mungu tunayemwabudu sisi ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo (Israel), yaani Mungu wa Israel. hatuabudu alah wala isa bin mariam. tunamtambua Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo kwa njia ya Yesu Kristo (ambaye sio isa bin mariam ambaye wengine humsema). huyu Mungu aliingia agano na Ibrahim, na Mungu akiingia agano huwa hatengui, kipengele mojawapo cha agano ni kwamba watakaombariki yeye na uzao wake, Mungu pia atawabariki, watakaomlaani Mungu pia atawalaani. Uzao unaotambulika na Mungu kuwa ni uzao wa urithi unaokuwa refered hapa ni Uzao wa Isaka baba yake Yakobo (Yakobo alikuja kubadilishwa jina akaitwa Israel). Ishmael sio uzao wa ahadi wala wa urithi na hana baraka yeyote ya kimungu...nje ya ile moja tu aliyobarikiwa na ibrahim kuwa atakuwa na uzao mwingi/atazaa sasa na ndio hao waarabu.

kwahiyo ukiona vibendera hivyo jua kuwa tunausapoti uzao wa urithi ndani ya Ibrahim Isaka na Yakobo. hatuhitaji Israel itutambue kwa hilo, hata wasipotutambua au hata wasipotupenda au hata wasipokubaliana nasi au hata wasipokubaliana na imani yetu hiyo haituhusu, sisi hatuwatii waisrael, tunatii agano la Mungu. upo hapo?
 
Hao wa nabii wapya ndo wana potosha vijana wenye elimu duni na msongo wa mawanzo, eti nchi ya ahadi ni Israel wakati israel hiyo imeundwa 1948.
Huwezi pangia watu waishi unavyotaka na mambo ya Imani huyajui
 
Kwanini usisapoti Simba Sports Club na Bendera Taifa?

Nauliza tu.
simba na taifa hawana ahadi ya Mungu (kwa maana ya covenant). kumheshimu Mungu au kufuata kile unachoamini juu yake ni muhimu kuliko hata taifa lao mzee.
 
Israel Taifa teule...

Pale kwao wapo Milion Nane ila wamezungukwa na Waarabu zaidi ya Million 200 ila hakuna Mwarabu anae wasogelea[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Tuache ujinga wakati mwingine!Israel ni jamii ya watu weusi!hao unao wasema ni damu za waturuki, German, English, russia etc!!jamii ya watu weusi ndio waisrael!!sio hao!!
 
Wakuu heshima kwenu.

Naomba tu kuuliza japokuwa najua kufuatilia mambo ya watu sio mchongo wala nini.

Huwa naona vibendera vya taifa la Israel kwenye magari ya watu ambao naamini kabisa ni Wabongo wenzetu.

Sasa wakuu naomba tu kuuliza what is the motive behind this? kunakuwa na affiliation gani na hili Taifa la Israel?

Au ni Waisraeli weusi wanaoishi bongo?
Judeo Christianity,
Wakristo tunaamini(sio wote)kwamba Israel ni Taifa la Mungu,
Hata kama wanafanya mabaya lakini kwa wakristo,Israel ni Taifa pekee sana,ni Swala la imani,hata tukitaka kuwapa majina watoto tunaangalia majina ya kiyahudi.
Hata kwa waislam Dunia nzima,hujinasibisha na uarabu,Kwa muislam uarab ni superior race,unakuta mtu mweusi kama mie,mmakonde baada ya kuitwa gwakisa,kwa vile tu ni muislama anaona Bora achukue jina lenye Hadhi ya Kiarabu tu,
Ukienda Zenj,vijana wengi weusi hujaribu kujifananisha na waarabu kwa utamaduni,staili za nywele nk.
Ni mitazamo tu.
 
Vile vibendera ni ujinga tu

People mistake ukristu na Israel
Mbona wewe Umeweka Profile Picture yenye Bendera ya Jamaica??..
Alafu unawadharau wanaovaa za Israel

Ama kweli nyani haoni .........
 
Kila Mtu aabudu anachoabudu isiwe Nongwa

Tuwatake radhi Walokole.

Hiyo Bendera ya Israel hata waigeuze shuka na wajifunike ni juu yao.
 
wanaoweka bendera ya israel kwenye pikipiki na magari huwa hawana akili. huwa wanafikiri waisrael ni wakristo nakumbe waisrael wana dini yao watu wanaangamia kwa kukosa mariifa
 
Hadi masheikh wanapeperusha, umebaki wewe
 
Judeo Christianity,
Wakristo tunaamini(sio wote)kwamba Israel ni Taifa la Mungu,
Hata kama wanafanya mabaya lakini kwa wakristo,Israel ni Taifa pekee sana,ni Swala la imani,hata tukitaka kuwapa majina watoto tunaangalia majina ya kiyahudi.
Hata kwa waislam Dunia nzima,hujinasibisha na uarabu,Kwa muislam uarab ni superior race,unakuta mtu mweusi kama mie,mmakonde baada ya kuitwa gwakisa,kwa vile tu ni muislama anaona Bora achukue jina lenye Hadhi ya Kiarabu tu,
Ukienda Zenj,vijana wengi weusi hujaribu kujifananisha na waarabu kwa utamaduni,staili za nywele nk.
Ni mitazamo tu.

mbona sijamuona mtanzania anaitwa natamyahu jina la kisrael au gugrichi
 
Wengi wao ni religious fanatics hususani new born again Christians, wakati wa Israel wana upinga ukuristo.

Africa is a continent of confused fellows
Israel sio wakristo bali ni wa jewish, na wanaukata/ wanapinga ukristo, ni ushamba wa kiimani tu au kutojua ndio maana wanaweka hivyo vibendera.
 
Mbona wewe Umeweka Profile Picture yenye Bendera ya Jamaica??..
Alafu unawadharau wanaovaa za Israel

Ama kweli nyani haoni .........
Utakua either ni blind au ni idiot

Avatar yangu Iko clear…. Niko na garang

Acheni utumwa wa kingese na kujipendekeza kwa wayahudi…. They are the biggest racists
 
Mimi naona ni tabia tu na kuiganaigana, Watanzania wengi huwa hufanya vitu sio kwa maana ya lile jambo ni bendera fuata upepo
 
Back
Top Bottom