Kwa hiyo yuda eskariot atakua ndani ya ufalme wa milele na bwana yesu!?
Hapana,
Ila unapaswa Kujua Kwamba Yesu Alikufa Ili Damu yake Imwagike Kusudi lipatikane Agano Jipya
Kwa Hyo Yesu Asingekufa Basi Isingemwagika Damu na Kama Damu Isingemwagika Kusingekuwa na Ukombozi kwa Waliopotea.....
Kwa Hyo Yesu alijua kabisa Ni lazima Afe..
Ndyo maana Petro alipomshauri Asisulubiwe Yesu Alimkemea
Mathayo 16:21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kupata mateso mengi kwa wazee na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.
22 Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akisema, Hasha, Bwana, hayo hayatakupata.
23 Akageuka, akamwambia Petro, Nenda nyuma yangu, Shetani; u kikwazo kwangu; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu
Kwa hyo Basi ulikuwa Ni mpango wa Mungu Yesu Afe