Maadamu Biblia Haijaandika hizo sababu za Yuda kutokuingia Peponi Basi Na Mimi Sina Cha Kukuambia
Ila Suala la kwamba Kifo Cha Yesu Ni mpango wa Mungu Hilo Nina Uhakika nalo kwa maana limeandikwa.. katika
Marko 8:31 Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupatikana na mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na wakuu wa makuhani, na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.
32 Naye alikuwa akinena neno hilo waziwazi. Petro akamchukua, akaanza kumkemea.
33 Akageuka, akawatazama wanafunzi wake, akamkemea Petro, akasema, Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu