Vibendera vya Israel kwenye magari ya Wabongo

Vibendera vya Israel kwenye magari ya Wabongo

yaani watu baadala ya kuonyesha uzalendo kwa kutumia bendera za nchi zao na asili za mababu zao wako busy kutukuza mataifa mengine, purely brainwashed Africans.

Huu mimi naona ni ushamba, ulimbukeni na ujuha Mtanzania mzaramo/mnyaki /msukuma/ Mchaga eti analitukuza Taifa la Israeli baadala ya kuitukuza na kuipenda nchi yake Tanzania..
Ni kosa kosheria kuva nembo za taifa la tz , iw e culture, zile skafu, au kupeperusha bendera zenye bedera ya tz
 
yaani watu baadala ya kuonyesha uzalendo kwa kutumia bendera za nchi zao na asili za mababu zao wako busy kutukuza mataifa mengine, purely brainwashed Africans.

Huu mimi naona ni ushamba, ulimbukeni na ujuha Mtanzania mzaramo/mnyaki /msukuma/ Mchaga eti analitukuza Taifa la Israeli baadala ya kuitukuza na kuipenda nchi yake Tanzania..
Wewe umejiita samurai hao kina samurai ni babu zako?
 
Darmian nadhani hii ni moja ya sababu;
Kwenye maandiko kuna sehemu baada ya Mfalme Suleiman kumaliza ujenzi wa Hekalu ambalo Baba yake (Daudi) alielekezwa kujenga, kwenye sehemu ya sala yake / hotuba yake alisema hivi;

“Hata na mgeni naye, asiyekuwa mmoja wa watu wako Israeli, atakapokuja kutoka nchi iliyo mbali sana kwa ajili ya jina lako kuu, na mkono wako ulio hodari, na mkono wako ulionyoshwa; hao watakapokuja na kuomba wakiielekea nyumba hii; basi usikie huko mbinguni, toka makaoni mwako, ukatende yote atakayokuomba huyo mgeni; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe, kama watu wako Israeli, tena wajue ya kuwa nyumba hii niliyoijenga imeitwa kwa jina lako.”
‭‭2 Nya‬ ‭6:32-33‬ ‭

Ndio maana wengi wanaenda kuhiji Israel, na pia wengi wanaitambua kama Taifa Teule la Mungu!
 
Na wale jamaa wakisema kesho tu, hii ndio nchi yao ya ahadi walioahidiwa lazima majamaa yawaunge mkono with reference to the bible.. yatakuwa tayari hata kuwaua wamakonde wenzao ili kuwasaidia waisraeli aka Taifa teule ( ukiwabariki nawe umebarikiwa reference ni bible ambayo imeandikwa na wenyewe)....
Too sad.
 
Wakuu heshima kwenu.

Naomba tu kuuliza japokuwa najua kufuatilia mambo ya watu sio mchongo wala nini.

Huwa naona vibendera vya taifa la Israel kwenye magari ya watu ambao naamini kabisa ni Wabongo wenzetu.

Sasa wakuu naomba tu kuuliza what is the motive behind this? kunakuwa na affiliation gani na hili Taifa la Israel?

Au ni Waisraeli weusi wanaoishi bongo?
Na kwenye madhabau ya makanisa ya EAGT
 
Bila picha huu ni uchonganishi wa wazi. Ninavyowajua walokole wa Bongo hawana muda na bendera za Israel.
 
Ni imani na utaratibu ambao baadhi ya watu wamejiwekea, napia uwepo wa vibendera hivyo ni rahisi kuvipata,Kama ilivyo utaratibu au Imani ya makada wa vyama vya siasa either chama A au B , hivyo usishangae Sana mkuu.
 
Wakristo wa Africa hawapo sawa sidhani hilo jambo kama unaweza kulikuta kwa wakristo wazungu iwe ujerumani urusi au nchi yoyote eti aweke bendera ya Israel
Laiti waktriso wangejua kuwa wayahudi hawampendi huyo Yesu na walimsulubisha kwakuwa alikuwa ana laana ya taurati
Asilimia kubwa ya waisrael wanafata dini ya Judaism ambayo mafundisho yake wanafata The Talmud unmasked
Ukisoma vizuri The Talmud unmasked utakuja kuona mariam aliitwa malaya alimzaa mtoto wake na pepo chafu rejea The Talmud unmasked by Rev I.B Pranaitis chap 1 ukurasa wa 30
"Hayo ndio waliyoyatenda kwa mwana wa Stada katika Lud na wakamsulubisha jioni ya Pasaka.Kwani mwana huyo wa Stada alikuwa mwanaye Pandira.Maana Mwalimu Chasda anatuambia ya kuwa Pandira alikuwa mume wa Stada aliyekuwa mamake,na yeye aliishi katika zama za Paphus wa Jehuda"

Mwandishi wa The Talmud unmasked Rev IB Pranaitis akifanunua maneno hayo juu akisema
"Hayo yanamaanisha ya kwamba Mariam ndiye aliyeitwa Stada yaan malaya kwani sawa na ilivyofundishwa hapo Pumbadita yeye alimuacha mumewe na akafanya uzinzi.Hayo pia yameandikwa katika Jerusalem na Maimonides"

Kwa maelezo zaidi kasome mafundisho ya Talmud kwa uraisi tafuta kitabu cha Talmud unmasked by Rev I.B Pranaitis na uone wakristo na Yesu walivyosimangwa na kutukanwa na wayahudi that's why population yao israel ni asilimia 2 tu
 
yaani watu baadala ya kuonyesha uzalendo kwa kutumia bendera za nchi zao na asili za mababu zao wako busy kutukuza mataifa mengine, purely brainwashed Africans.

Huu mimi naona ni ushamba, ulimbukeni na ujuha Mtanzania mzaramo/mnyaki /msukuma/ Mchaga eti analitukuza Taifa la Israeli baadala ya kuitukuza na kuipenda nchi yake Tanzania..
Hayo makabila uliyoyataja hapo nchi yao ni tanganyika sio tanzania.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wengi ni pambo tu kama wanavyovaa kacha za kinaijeria,kenya etc

Hii ya kacha huwa nawashangaa sana wabongo huezi mkuta mkenya akivaa yakibongo Hata akiwa huku ila sisi sasa mara ya kenya,south Africa utakuta mwingine kazipangilia kabisa hahaha
 
Over 90% ya watu duniani ni majuha [mazuzu], niamini mimi tu…. ni rahisi kuangukia kundi hilo.
 
Tofautisha wa israel na Israeli kama nchi nyie mna kalilishwa vibaya kwasbb hamtaki kufanya utafiti kujua Mungu alikua anamaanisha nini katika hilo.....watu wote tuko sawa mbele ya Mungu hamnaga matabaka mbele ya Mungu
Kama watu wote tuko sawa mbona kuna ambao wanawaita wenzao makafiri.hao nao wawaweke kundi gani?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu heshima kwenu.

Naomba tu kuuliza japokuwa najua kufuatilia mambo ya watu sio mchongo wala nini.

Huwa naona vibendera vya taifa la Israel kwenye magari ya watu ambao naamini kabisa ni Wabongo wenzetu.

Sasa wakuu naomba tu kuuliza what is the motive behind this? kunakuwa na affiliation gani na hili Taifa la Israel?

Au ni Waisraeli weusi wanaoishi bongo?
Ni wajinga wakilokole wanaodhani mabeberu wa kizayuni wa leo ndio wale mayahudi kwenye biblia
 
Wakuu heshima kwenu.

Naomba tu kuuliza japokuwa najua kufuatilia mambo ya watu sio mchongo wala nini.

Huwa naona vibendera vya taifa la Israel kwenye magari ya watu ambao naamini kabisa ni Wabongo wenzetu.

Sasa wakuu naomba tu kuuliza what is the motive behind this? kunakuwa na affiliation gani na hili Taifa la Israel?

Au ni Waisraeli weusi wanaoishi bongo?
Unajua Israeli inaongoza kwa Propaganda,. Na imewakamata wengi
 
Hii ya kacha huwa nawashangaa sana wabongo huezi mkuta mkenya akivaa yakibongo Hata akiwa huku ila sisi sasa mara ya kenya,south Africa utakuta mwingine kazipangilia kabisa hahaha
Ujinga mtupu mkuu..
 
Watanzania tunapaswa sasa kubadilika

1. tuanze kuwa wabinafsi kwa kupendana wenyewe kwa wenyewe... Mtanzania mpende mtanzania mwenzako popote ulipo na kuipenda nchi yako... mkiwa mahala watu wajue watanzania wako mahala..

2. Tuipende nchi yetu pamoja na yote yakisiasa na ujinga wa wanasiasa, tuipende nchi yetu kwa pamoja ipasavyo na kuitetea popote pale..

3. Tupende na kutangaza kila kinachoitwa mali ya Tanzania kuliko chochote, na popote ukiona bendera ya Tanzania basi unaifeel..
 
Back
Top Bottom