Hii ngoma bado mbichiii. Vicky Kamata kumbe yuko serious sana na hii mirathi ya Dr. Likwelile.
Baada ya hukumu ya mahakama kutoka na kutomtambua yeye kama mke halali, kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika haya:
"Post ya Muda mfupi.
Nakuomba msamaha mume wangu kwa kuwa mimi ni Mkatoliki na Imani yangu inaniambia unaona na unajua kila kitu kinachoendelea kati yangu na wanao. Najua muda utaongea lakini kwa kuwa nami ni binadamu naomba niseme yafuatayo!
Ni kweli mimi ni kiumbe dhaifu na mwenye dhambi nyingi tu kama wengine. Lakini wanangu kwanini mnapindisha ukweli? Nimedhulumu mali gani? Nimemfukuza nani? Nyumba ipi? Niliishi nyumba yoyote kati ya zile nilimkuta nazo na mama zenu?
Wanangu hata kama ni chuki iwe na kiasi basii. Sitaki kumuaibisha mume wangu lakini mnanichochea na kunisukuma wanangu! Niambie Dunia ukweli wa maisha yangu na Baba yenu? Alikuwa na pesa kunizidi yes! Lakini alikuwa na asset gani ya maana kunizidi mimi?
Alipokuwa na Mama zenu alifanya nini? Raymond bila aibu wala hofu ya Mungu ukaorodhesha majengo yangu yote ukakimblia mahakamani ni nani anaetaka kudhulumiwa hapo? Ni mimi au nyie?. Tuwe na kiasi wanangu, tunagombania vitu ambavyo tutakufa tuviache. Baba yenu alikuwa na nyumba za kawaida na msululu wa watoto.
Kwanini alipokuwa na Mama zenu hakufanya maendeleo? Je mmeniona popote katika mali ambazo sina jasho langu? Leo mnanichafua na kunipaka matope kwa uongo? Kwa jasho langu? Mungu mnamjua nyie watoto?
Nimetoka familia masikini sana, na nimefika hapa kwa jasho la damu. Naomba sana mshangilie ushindi wenu kwa heshima! Sijafukuza mtu! Sijadhulumu na sintakuja kudhulumu maishani kwangu.
Nafanya kazi usiku na mchana kwa kuwa najua sina wa kunipa cha bure. Baba yenu hata swimming pool ameikuta kwangu. Na baadae tukachimba tukiwa wote. Bahati Mbaya Mungu kamuita mapema.
Najua tunamuumiza sana. Tulieni sihitaji hata kijiko ambacho siyo cha jasho langu. Maisha ni hadhithi tu.
🙏🙏🙏🙏 Nimemaliza hamtanisikia tena juu ya jambo hili.