Vicky Kamata asema marehemu mume wake "Alikuwa na vinyumba vya kawaida na msururu wa watoto!"

Vicky Kamata asema marehemu mume wake "Alikuwa na vinyumba vya kawaida na msururu wa watoto!"

Mtu aliekuwa kitengo nyeti BOT mtaalamu wa Uchumi anatambiwa na kilaza
BOT hadi miaka ya 2010 ilikuwa na upuuzi wa kuwekana pale kwa kujuana. Kuna siku mwaka 2009 nilikuta vigogo wa wizara ya fedha wanalalamika kwamba angalau wao wanachomeka watu wao wenye sifa ila BOT wanachomeka vilaza kwenye ajira. Nadhani wakati wa Magu alifagia fagia. Huyo Vicky hakuwa na sifa za kuwa BOT unless ilikuwa kazi ya kufanya usafi au secretary... awamu ya 4 ilikuwa na mambo ya kijinga sana.
 
images (70).jpeg


Vile ni Vijumba.
 
Na nyie wanaume hivi mkikaa bila kugegeda mnashindwa nini?.mtu umeshazeeka bado busy mpk kuoa tena...ndo maana mnakufa mapema...kaa mwenyewe na wtt wako ule uzee wako bila stress...
Tatizo watu wengi wana maono kama yako!

Saazingine tunaishi kwa dhiki duniani kwa ajili ya misimamo kama hii!

Hivi mkuu let say umefiwa ukaoa mwanamke mwingine, ni lazima mwanamke huyo akuletee stress?

Tatizo labda hizo ndoa za kuoa majina ndiyo nyingi zinasumbua hivyo!

Lakini uelewe kwamba, hakuna chochote, iwe mali ama pesa ambacho kinaweza kumpatia faraja mwanaume kama mke!

Mke mwenye sifa stahiki zinazopaswa awe nazo mke ni hazina kubwa inayobeba uhai wa mwanaume.

Raha atapata, heshima utapata na maisha marefu utapata.
 
Hii ngoma bado mbichiii. Vicky Kamata kumbe yuko serious sana na hii mirathi ya Dr. Likwelile.

Baada ya hukumu ya mahakama kutoka na kutomtambua yeye kama mke halali, kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika haya:

"Post ya Muda mfupi.
Nakuomba msamaha mume wangu kwa kuwa mimi ni Mkatoliki na Imani yangu inaniambia unaona na unajua kila kitu kinachoendelea kati yangu na wanao. Najua muda utaongea lakini kwa kuwa nami ni binadamu naomba niseme yafuatayo!

Ni kweli mimi ni kiumbe dhaifu na mwenye dhambi nyingi tu kama wengine. Lakini wanangu kwanini mnapindisha ukweli? Nimedhulumu mali gani? Nimemfukuza nani? Nyumba ipi? Niliishi nyumba yoyote kati ya zile nilimkuta nazo na mama zenu?

Wanangu hata kama ni chuki iwe na kiasi basii. Sitaki kumuaibisha mume wangu lakini mnanichochea na kunisukuma wanangu! Niambie Dunia ukweli wa maisha yangu na Baba yenu? Alikuwa na pesa kunizidi yes! Lakini alikuwa na asset gani ya maana kunizidi mimi?

Alipokuwa na Mama zenu alifanya nini? Raymond bila aibu wala hofu ya Mungu ukaorodhesha majengo yangu yote ukakimblia mahakamani ni nani anaetaka kudhulumiwa hapo? Ni mimi au nyie?. Tuwe na kiasi wanangu, tunagombania vitu ambavyo tutakufa tuviache. Baba yenu alikuwa na nyumba za kawaida na msululu wa watoto.

Kwanini alipokuwa na Mama zenu hakufanya maendeleo? Je mmeniona popote katika mali ambazo sina jasho langu? Leo mnanichafua na kunipaka matope kwa uongo? Kwa jasho langu? Mungu mnamjua nyie watoto?

Nimetoka familia masikini sana, na nimefika hapa kwa jasho la damu. Naomba sana mshangilie ushindi wenu kwa heshima! Sijafukuza mtu! Sijadhulumu na sintakuja kudhulumu maishani kwangu.

Nafanya kazi usiku na mchana kwa kuwa najua sina wa kunipa cha bure. Baba yenu hata swimming pool ameikuta kwangu. Na baadae tukachimba tukiwa wote. Bahati Mbaya Mungu kamuita mapema.

Najua tunamuumiza sana. Tulieni sihitaji hata kijiko ambacho siyo cha jasho langu. Maisha ni hadhithi tu.

🙏🙏🙏🙏 Nimemaliza hamtanisikia tena juu ya jambo hili.
🤣🤣Hakuna mlatolik wa hivyo
Asituharibie dhehebu letu
Nami mkatolik kindakndaki
 
1. Posho za Ubunge kama hela za madini Mkuu si unaona Zitto anabangaiza pamoja na kuwa Mbunge miaka yote?

2 Demu pamoja na Mzee wa awamu ya 44 kula bado hakufanya maendeleo.

3. Demu bado pisi atatokea boya mwingine nae ale vitu ajenge nyumba kisha atangulizwe kama Dr
Kuna yule mtoto wa mjini alitangaza ndoa na Vicky michango ikachangwa kisha mwamba akasepa na kijiji kabla ya ndoa kufanyika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakupaswa kuandika eti hata swimming pool kaikuta kwake,eti hakuwa na asset kumzidi,jamani aibu nimesikia Mimi....hiki ni kiasi Kikubwa Cha utomvu wa nidhamu
Hivi jamani.... Swimming pool kumbe ni kitu Cha maana Sana ambacho ukikiongelea kinashitua watu eee.... Jamani.... Mimi ni huu ushamba umenielemea.... Like Seriously.... 😅🤣
 
Back
Top Bottom