Video: Bernard Membe akutana na kuteta na Baba Askofu Ruwai'ch

Video: Bernard Membe akutana na kuteta na Baba Askofu Ruwai'ch

Nimeileta kimkakati tu , wala si lengo langu kumpeleka Membe Chadema
Hamna mkakati wowote! Nakuhakikishia hamna plan yoyote! Subirini huyu Membe mnayemshabikia muone atakavyowaacha kwenye jua kali na yeye akimbilie kivulini...
 
Sasa ni wakati gani mwanachama mpya anaaminiwa na kupewa uongozi CHADEMA?! Na anapimwa vipi kwamba hatorejea ccm au ACT?!

Wangalau 2yrs minimum kwa utashi wangu, na kama ni urais au uenyekiti wa chama, not less than five consecutive yrs, tena apimwe mwenendo wake kulingana na nafasi husika.

Sio ule uhuni wa kama Lowassa alijiunga CHADEMA miezi miwili kabla ya uchaguzi, ndani ya siku 2 ni mwanachama na kupewa nafasi ya uongozi kubwa kuliko zote nchini kupitia chama! Kichekesho akawa hata kusalimia anakosea na kusema "CCM hoye" kosa lile limeigharimu sana cdm mpaka hivi leo.

Jaribu kuangalia wabunge wangapi na madiwani wamerudi CCM, angalia wengi wao walipokuja cdm toka ccm walijiunga lini. Sasa mtu kama Membe kwa sasa bado miezi kumi uchaguzi ufanyike na bado yuko CCM, usishangae akajiunga upinzani kwa mwendo ule ule wa kubadili gear angani kisha akapewa nafasi ya kugombea. Kwa hilo hatuko tayari tena.
 
Mkuu tuachane na huyo Membe tumeshaumwa na nyoka Lowassa, hakuna mwanaccm anayetufaa tena. Ni juu yetu kuanza kudai Tume huru ya uchaguzi na tuhakikishe tunaonyesha kuwa hakuna uchaguzi chini ya tume iliyopo. Wananchi wameshaelewa, ni juu ya wapinzani kusukuma tu hiyo ajenda. Lissu kaonyesha njia jana.
Tatizo la Tanzania sio CCM kama wengi wanavyoamini bali ni watanzania wenyewe
 
Membe anapita njia ileile alopita Lowasa na hata ile ilopigwa deki.

Mwisho wa siku akatangaza amerudi nyumbani CCM.

Upinzani kwa sasa haupo Tanzania na hata ukiwepo utatokea CCM kwenyewe.

Lakini sio kupitia Bernard Membe wala huyo Tundu Lisu.

Kheri ya Christmas
 
Kwa ujumla upinzani umeshakata tamaa! Dalili zinaonyesha kabisa. Ukiona wanavyomshabikia Membe unajua kabisa wako kwenye panic attack na wako tayari kushika chochote kilicho mbele yao! Hawana plan, hawana strategy, wapo kusubiri muujiza ambao hautatokea.

Huyo Membe anashabikiwa na vyama vya upinzani au ni manazi wa upinzani huku jukwaani? Huku mitandaoni sio office ya chama chochote cha siasa useme mipango yao utaionea huku jukwaani. Labda hujui ni wapi sehemu sahihi ya kupata mipango ya vyama. Ingekuwa huko kukosekana kwa mipango unatuambia umeiona kwenye ofisi husika za hivyo vyama, hapo ungekuwa na hoja, na sio hizi predictions zako.
 
Mkuu tuachane na huyo Membe tumeshaumwa na nyoka Lowassa, hakuna mwanaccm anayetufaa tena. Ni juu yetu kuanza kudai Tume huru ya uchaguzi na tuhakikishe tunaonyesha kuwa hakuna uchaguzi chini ya tume iliyopo. Wananchi wameshaelewa, ni juu ya wapinzani kusukuma tu hiyo ajenda. Lissu kaonyesha njia jana.
Hapana Mkuu
Bernard Membe anafaa sana kugombea CCM.
Jamaa wameamua kwenda na Membe 2020

Sent from my SM-A207F using Tapatalk
 
Hapana Mkuu
Bernard Membe anafaa sana kugombea CCM.
Jamaa wameamua kwenda na Membe 2020

Sent from my SM-A207F using Tapatalk

Akigombea huko ccm sawa, nitamuunga mkono awe mgombea wa ccm ili kutuondolea hili janga lililopo, lakini sio kuwa rais, maana tatizo la ccm litaendelea kuwepo.
 
Mkuu tuachane na huyo Membe tumeshaumwa na nyoka Lowassa, hakuna mwanaccm anayetufaa tena. Ni juu yetu kuanza kudai Tume huru ya uchaguzi na tuhakikishe tunaonyesha kuwa hakuna uchaguzi chini ya tume iliyopo. Wananchi wameshaelewa, ni juu ya wapinzani kusukuma tu hiyo ajenda. Lissu kaonyesha njia jana.
Mkuu Tindo, huwa unajifungia kamba ngumu sana katika misimamo yako kiasi kwamba inapobidi uilegeze ili uwe huru inakuwia ngumu sana kuilegeza.

Ngoja nijieleze usinihukumu bila kupima ninachomaanisha.

Sasa hivi katika nchi hii adui ni mmoja tu na anafahamika, sina haja ya kumtaja hapa.

Kama kuna mtu ambaye hata hukubaliani naye, akajitokeza kusaidia kumudhoofisha adui yenu huyo ili mpate urahisi wa kumwondoa, bado utaendelea kushikilia huyo mtu asifanye hiyo kazi kwa vile yupo/alikuwa upande uleule wa adui yako?

Kama huko ndani ya CCM wapo watu wasiopenda haya yaliyopo, kwa nini wasisaidie kazi hiyo iwe rahisi? Kwani ni lazima Membe au wengineo walioko huko waje CHADEMA? Hawawezi wakaifanya hiyo kazi ya kutusaidia kumwondoa wakiwa huko huko waliko?

Kwani CHADEMA sasa hivi, kati ya kuondoa balaa lililopo sasa, au kubaki kwenye upinzani lakini wakiwa huru kufanya kazi yao; ni lipi lililo la mhimu zaidi kati ya hayo mawili, kwa wakati huu tulio nao sasa.
 
Hamna mkakati wowote! Nakuhakikishia hamna plan yoyote! Subirini huyu Membe mnayemshabikia muone atakavyowaacha kwenye jua kali na yeye akimbilie kivulini...
bado unaandika uongo ili iweje ?
 
Back
Top Bottom