Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Mahakana kutozingatia haki ndiyo kunakoleta picha mbaya.
Lakini Serikali ina uwezo na haki ya kuilalamikia mahakana and vice versa.
 
Hii imenikumbusha yule jaji aliyeamua kesi ya wafanyabiashara wa madawa wakiwemo raia wa Pakistan

Kuna majaji wengine wana mambo mengi sana

Ova
 
Majaji nani anawateua? Wanateuliwa kwa vigezo gani? Kusikia haya madudu kunatia unajisi mahakama
Tulishaonya siku nyingi kuwa utaratibu wa uteuzi wa majaji haufuatwi. Upuuzi huu ulianza enzi za Magufuli kuteua majaji kiholela,nakumbuka kuna hakim mmoja aliteuliwa na Magufuli kuwa jaji simply kwa sababu aliandika hukumu kwa Kiswahili, matokeo yake ndiyo haya kuteua majambazi kuwa majaji. Tunajua kuwa mawakili wengi siku hizi siyo waadilifu kabisa wanauza haki za wateja wao kwa tamaa ya utajiri wa haraka haraka. Ndiyo hapa tulipofika sasa.
 
Jaji kama huyo unamfanyaje Sasa???.

Ndio sababu PAUL MAKONDA, ANAPENDWA KAMA ALIVYOKUA MAGUFULI.

Nchi hii Kwa Sasa tuna

Makonda.... Silaa, Mpina....Mchengerwa...Msambatavangu.... Gwajima..Gwajima Ke, Bashungwa ,

Bado tuna watu bado tunao.
Tena hao Viongozi wapenda haki wote tutawalinda kwa kila namna hadi kwa swala kwenda kwa Mwenyezi Mungu awalinde na maovu ya wasiopenda haki kutendeka!!
 
Jerry ni LLB, imekuwaje afike mbali hivi na kutoa tuhuma kubwa namna hii bila kusikiliza pande zote mbili? anayesemekana kuwa tapeli alipoongea kwenye clip yake mbona kama hoja zake zina mashiko?

kuna kitu kimoja tufahamu, kati ya vitu unatakiwa kuogopa wewe ambaye pengine umefanikiwa maishani, ni kugombana na mtu wa hali ya chini. kuna wafanya biashara, kuna wafanyakazi wa umma au matajiri, huwa wanapoteza sana haki zao mbele ya watu wa hali ya chini kwasababu kiongozi yeyote hasa hawa wa kisiasa akiwaangalia, anaamini lazima wewe mwenye uwezo utakuwa unamuonea na anakuwa biased against you kwasababu tu una kipato. ndio maana tunahitaji chombo kilicho katikati bila kuwa biased, na Mahakama hata ikilalamikiwa vipi ndio chombo cha katikati, kila mtu alete hoja zake na mahakama iamue. huna hoja umepoteza. nilishawahi kupitia mazingira kama hayahaya tena kwenye mambo ya ardhi kama haya,mtu mmoja wa hali ya chini ameenda kulalamika hadi kwa waziri huko ati namwonea, nilipambana na kwa msaada wa Mungu ikaja kugundulika kumbe yule mtu wa chini ndio alikuwa mwongo na tapeli akitumiwa na watu wengine wenye pesa kupora ardhi yangu ili wafaidike pamoja. hapa ndipo nilipojifunza sio kila unayekutana naye analia ameonewa, wengine huwa wanalia kwasababu wamekwamba kuonea wengine, wamekutana na saizi yao.
Ukiona Slaa kaonge vile juwa nyuma yake kuna Rais aliyemtuma akapambane haki za watu zipatikane.

Samia akiwa ni mwanamama hawezi kuwa na ugumu ule ule wa JPM, anatumia wanaume kumfanyia kazi ngumu.

Makonda anaonekana hafai kuwa mkuu wa mkoa lakini kampa cheo, anayapenda anayoyafanya kwani yeye akiwa mwanamama hawezi kuyafanya kwa ujasiri wanaokuwa nao hao anaowatuma.
 
Huyo Jaji muda si mrefu atatimuliwa, na uhakika kwa uongozi makini wa Mama yetu Samia, hatuwezi kuwa na Jaji anatumia taaluma yake kulinda matapeli, ukiona hiyo huyo Jaji ni mla rushwa mkubwa sana na uhakika ataondolewa haraka sana
Kifupi ni kuwa huyo jaji ni jambazi.
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Huna hata haya ndugu yangu!
 
Nchi yetu tuna mifumo ila haifanyi kazi, na ndiyo maana kina makonda wanajizolea pointi 3 kila kukicha kutatua migogooro ambayo ki uhakisia haitakiwi iwepo.

Yaani mkandalasi anafanya kazi ya Halmashauri anamaliza afu miaka 07 hajalipwa, kichekesho.

CCM ishajichokea kila kona.
 
Anayedhani kuwa hajapata hukumu ya haki tokana na sababu anazoeleza huyu waziri Jerry Silaa utaratibu wa kisheria si unamtaka apinge hiyo hukumu kwa kukata rufaa mahakama ya juu?

Yeye Waziri anamwandikia Waziri wa Katiba ili iweje? Kwani Waziri wa Katiba ni ngazi ya rufaa ktk mfumo wa utoaji haki wa kimahakama?

Huyo ambaye hakutendewa haki, anapaswa kwenda mahakama ya juu na aielezee scenario yote ya Jaji Y, na X na Z kuwa ndio chanzo cha yeye kutopata hukumu ya haki..

Mahakama ya rufani ikipima sababu za mrufani na ikaziona zina uzito wa kisheria, ni wazi kuwa hukumu ya awali itatenguliwa..

Lakini kama tukitaka nchi iende ki - Makonda Konda au ki - Jerry Silaa silaa, basi tutaishi maisha ya dizaini ya "Animal Farm" au "Shamba la Wanyama" kuwa mwenye nguvu anawatawala wasio na nguvu atakavyo yeye..

Ofcoz, hata mhimili wa mahakama nao uko very much compromised. Na umeharibiwa na mfumo wetu mbovu wa kikakatiba na utawala. Na hili lilijidhihirisha zaidi wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli...

Huyu Jerry Silaa na Paul Makonda bado wanaishi ktk mentality ya ki - Magufuli na wanataka kuuendeleza kwa kuielekeza mahakama ifanye vile watakavyo wao kinyume cha taratibu na sheria..
.wamezoea kuchezea mahakqman sasa mwendo wa kulipuana mkuuu unajua ghara.ma za kufika mahakama kuu ama rufaniii???Mungu akiamua kusimama anatumia...hata viongozi mkuuu tukia Singapore iwaaingieee kuna mtu katumiwa barua ya kujieleza mkuu uwe mpoleee tu

M.mahakaman sifiki yaaan nakuavha unajenga nakujakubokoa ukanishtakii mahakaman mm
 
Awali "Y" alikuwa Wakili na aka attest nyaraka za Mzee "X". Hatimaye Tapeli "Z" akadhulumu kiwanja, kesi ikafunguliwa. Na kwa bahati mbaya ikaanguka kwa Jaji "Y" ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Mzee "X". Na sasa Jaji "Y" anawaita Mawakili wa Serikali kutaka kuwa CORRUT.

Je huyu Jaji "Y" ni nani? Na Je huyu Tapeli "Z" ndiye Alex Msama au Mushi?

Haya wataalamu wa mambo ya ARDHI tufungulieni codes.
---
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuwa ameandika barua kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria kufuatia jaji mmoja wa mahakama kukiuka kanuni za taaluma.

Waziri Silaa akihitimisha hoja ya bajeti yake bungeni amesema kuwa mwaka 2015 jaji huyo alikuwa wakili, na akamsaidia tapeli mmoja kuchukua ardhi ya watu.

Amesema warithi wa aliyetapeliwa walipoenda makamani hivi karibuni, wamekuta wakili yule sasa ni jaji, bado akaamua kwa kumnufaisha tapeli.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwamba jambo hilo amelichukua yeye ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na haki inapatikana.

Credit: TBC
Mara kadhaa imetokea baadhi ya watumishi hasa wa umma wanapowaumiza wananchi baada ya muda wanapandishwa vyeo, nadhani siyo sawa kabisaa.
 
sasa uhatari wake upo wapi, wakati wewe huna pesa, na amekusaidia kukukopesha? mkiwa na shida mnaenda kwao, mkishindwa kurudisha deni mnaamua muwauzie tu nyumba mnalalamika kuwa ni watu wabaya. ongea kwa facts, ubaya wake kwa hiki ulichoongea ninini?
Kwani ni wewe ndiyo Valence Matunda? Mumezoea vya kunyonga. Subiri muziki wa Jerry Silaa
 
sio raisi kihivyo ndugu. Jaji kubuliwa ni issue kubwa sio ya kitoto kama hii. kwanza hapo ni tuhuma tu, si ukute jaji ana hoja zote za utetezi. pia, issue ya utapeli kiwanja, tumesikia upande mmoja, upande wa anayesemekana tapeli hawakumhoji. pia, siku zote wenye nacho huwa wanachukiwa na masikini, wewe ukiona unaona wivu maendeleo ya tajiri, jua ni kapuku. ukiona unaona wivu na kuchukia majaji jua umepambana kuwa jaji na umeona hautakuja kuwa kama wao au unatamani mafanikio yao.
Wewe jamaa hauko mbali na mfumo kandamizi. Wewe kama siyo dhulumat wa viwanja basi uko karibu na majaji
 
Back
Top Bottom