Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

Si kwamba ni mara ya kwanza Wizara ya Aridhi kuzingumzia kesi hii, hata Mh. Mabula alishawahi kuizungumza na kumtaja hadharani Bw. Valence Simon Matunda kama tapeli sugu. Inakuaje yupo mtahani mpaka leo🤔?​

Huyu Valence Matunda ni hatari sana. Hata hapa Mbezi Makonde ana nyumba yake na jirani na ndugu yake aliye mkaribisha. Sasa huyo jirani yake ambaye ni shemeji yake alikuwa anakopa hela kidogo kidogo. Matokeo yake baada ya deni kuwa kubwa akamuambia amuongeze hela kidogo ili huyo shemeji yake amuachie nyumba wanayopakana. Jamaa akawa hana namna kachia nyumba na kapewa hela kidogo kahamia sijui Trgeta A.
 
Kwani waziri kusema tu hivyo ndiyo kumfanya 'jaji amsaidie tapeli'. Aende mahakamani ili mbivu na mbichi zieleweke. Kumwandikia tu waziri wa sheria hakusaidii kitu kwa tuhuma kama hizi. Lakini pia kama waziri hatakuwa na ushahidi wenye nguvu jaji anayeshutumiwa akifungua kesi ya madai kumshushishia heshima mbele ya jamii, patakuwa patamu hapo!
Jaji afungue kesi sasa, na sisi tutamfungulia ya kumvua UJAJI kupitia Judicial Srvice Commission
 
Huyu Valence Matunda ni hatari sana. Hata hapa Mbezi Makonde ana nyumba yake na jirani na ndugu yake aliye mkaribisha. Sasa huyo jirani yake ambaye ni shemeji yake alikuwa anakopa hela kidogo kidogo. Matokeo yake baada ya deni kuwa kubwa akamuambia amuongeze hela kidogo ili huyo shemeji yake amuachie nyumba wanayopakana. Jamaa akawa hana namna kachia nyumba na kapewa hela kidogo kahamia sijui Trgeta A.
sasa uhatari wake upo wapi, wakati wewe huna pesa, na amekusaidia kukukopesha? mkiwa na shida mnaenda kwao, mkishindwa kurudisha deni mnaamua muwauzie tu nyumba mnalalamika kuwa ni watu wabaya. ongea kwa facts, ubaya wake kwa hiki ulichoongea ninini?
 
Jaji afungue kesi sasa, na sisi tutamfungulia ya kumvua UJAJI kupitia Judicial Srvice Commission
sio raisi kihivyo ndugu. Jaji kubuliwa ni issue kubwa sio ya kitoto kama hii. kwanza hapo ni tuhuma tu, si ukute jaji ana hoja zote za utetezi. pia, issue ya utapeli kiwanja, tumesikia upande mmoja, upande wa anayesemekana tapeli hawakumhoji. pia, siku zote wenye nacho huwa wanachukiwa na masikini, wewe ukiona unaona wivu maendeleo ya tajiri, jua ni kapuku. ukiona unaona wivu na kuchukia majaji jua umepambana kuwa jaji na umeona hautakuja kuwa kama wao au unatamani mafanikio yao.
 
Jaji afungue kesi sasa, na sisi tutamfungulia ya kumvua UJAJI kupitia Judicial Srvice Commission
Kwa kawaida anayelalamika ndiye anayefuangua kesi. Mfano, kama A anamlalamikia B, kwamba B kamwibia, A ndiye anatakiwa afungue kesi na atoe ushahidi kuonyesha B alivyomsibia. Endapo A atashindwa kufanya hivyo, B anaweza Kufungua kesi dhidi ya A kwamba A kamdhalilisha kwa kumvunjia heshima machoni mwa jamii.
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Kwajins mfumo ulivyooza ukienda kwa utaratibu hupati kitu ni kwenda nao kimbwa mbwa tu. Kama slaa anayosema ni kweli bas njia bora ni kwenda nao bila mfumo maalum.
 
Awali "Y" alikuwa Wakili na aka attest nyaraka za Mzee "X". Hatimaye Tapeli "Z" akadhulumu kiwanja, kesi ikafunguliwa. Na kwa bahati mbaya ikaanguka kwa Jaji "Y" ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Mzee "X". Na sasa Jaji "Y" anawaita Mawakili wa Serikali kutaka kuwa CORRUT.

Je huyu Jaji "Y" ni nani? Na Je huyu Tapeli "Z" ndiye Alex Msama au Mushi?

Haya wataalamu wa mambo ya ARDHI tufungulieni codes.
---
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuwa ameandika barua kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria kufuatia jaji mmoja wa mahakama kukiuka kanuni za taaluma.

Waziri Silaa akihitimisha hoja ya bajeti yake bungeni amesema kuwa mwaka 2015 jaji huyo alikuwa wakili, na akamsaidia tapeli mmoja kuchukua ardhi ya watu.

Amesema warithi wa aliyetapeliwa walipoenda makamani hivi karibuni, wamekuta wakili yule sasa ni jaji, bado akaamua kwa kumnufaisha tapeli.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwamba jambo hilo amelichukua yeye ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na haki inapatikana.

Credit: TBC
Hii nchi imeoza pakubwa sana. Ukifuatilia ziara za Makonda na Jerry utajua madudu yaliyopo. CCM iondoke tu waje wengine nao wajaribu kurekebisha mambo
 
Wadau hamjamboni nyote?

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuwa ameandika barua kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria kufuatia jaji mmoja wa mahakama kukiuka kanuni za taaluma.

Waziri Silaa akihitimisha hoja ya bajeti yake bungeni amesema kuwa mwaka 2015 jaji huyo alikuwa wakili, na akamsaidia tapeli mmoja kuchukua ardhi ya watu.

Amesema warithi wa aliyetapeliwa walipoenda makamani hivi karibuni, wamekuta wakili yule sasa ni jaji, bado akaamua kwa kumnufaisha tapeli.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwamba jambo hilo amelichukua yeye ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na haki inapatikana.
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
wewe mbona ukishindikiza Mahakama katika kesi ya Mbowe? au kwa sababu lilikuumiza wewe?
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Kwa kiwango gani haki yaweza kupatikana mahakamani?

Nadhani shida ni katiba ns mfumo wa uteuzi..
 
Kutokana na clip inayosambaa kwenye whatsup ikionyesha mh waziri wa ardhi akilalamika kuna. Jaji amekuwa akisaidia matapeli kuiba ardhi za watu

Kimaadili nilitaman kusikia jaji mkuu akitoa maamuzi yake kisheria kuhusu huyu bwana na kumtaja kabisa

Kwa yale aliyoongea napendekeza huyu jaji akae nje ya ofisi huku uchunguzi ukiendelea

Si hivyo tu swala lake nilitamani kusikia tume ya maadili .Mkitoa neno kwenye hili

Kama makazin tunasimamishwa uchunguzi unafanyika tunarudishwa na wengine wenye makosa wanaondoka shida nn kwa jaji??

Uchunguzi ufanyike na tupewe ripoti ya kilichotokea .Maana wananchi wengi wamekosa haki zaoo kupitia mahakaman na hawa matapeli

Kuna siku niliwahi sema hapa kama unahakika una docs halali za kiwanja chenu ukiona wahuni wanajenga subiria wafike kati

Peleka katapila na mapolisi kadhaa vunjavunja mpaka msingi

Ole wakoo usubiri kwenda mahakaman ndugu wale mkiwa mahakaman wanamalizia majumba yao

Unawaza wamepata kibali wapi ukirudi tena mahakaman wanafanya ufunguzi na party kubwa kwenye kiwanja chako

Dawa sumu maziwa fasta wapelekeee moto....

Polen sana wahanga yaliwahi kunikuta mjomba wangu akaniambia subiria wamalize msingi wapande kidogo

Tukafika tukaweka kwa gari walinzi katapila ikasafisha

Jamaa akapiga nkamwambia wasiliana na wakili wangu mjomba

Kufika kaonyeshwa docs kaleta wakili wake wakaziangalia akaanza anataka anilipe ashaingia hasara

Nkamtajia bei akashuka kidogo maisha yanaendelea

Hawa wahuni mtandao waoo mrefu mkuu umeshika mpaka wizaran yaan tunahitaji commited waziri kama silaha kurudisha heshima wizaran na manispaa

Allah atusaidie
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Serekali Kuu inawajibu wa kuingilia Muhimili wowote ule,hasa pale inapo ona haki haitendiki! Na ndiyo maana ya kua na Amiri Jeshi Mkuu, na haya wanayofanya kina Makonda na Silaa ni maagizo ya Mkuu wa Nchi ya kusimamia haki,hadi yule mwanakijiji wa chini kabisa apate haki yake bila ya kutumia nguvu!!
 
HAWA MBWAA WANA WATU LIKUKI MANISPAAA..MAHAKAMAN YAAN WAKIFIKA WANAONEKANA KAMA MIUNGU WATU UNA DOCS HALALI KABISA LAKINI WAPI
 
Awali "Y" alikuwa Wakili na aka attest nyaraka za Mzee "X". Hatimaye Tapeli "Z" akadhulumu kiwanja, kesi ikafunguliwa. Na kwa bahati mbaya ikaanguka kwa Jaji "Y" ambaye ndiye alikuwa Wakili wa Mzee "X". Na sasa Jaji "Y" anawaita Mawakili wa Serikali kutaka kuwa CORRUT.

Je huyu Jaji "Y" ni nani? Na Je huyu Tapeli "Z" ndiye Alex Msama au Mushi?

Haya wataalamu wa mambo ya ARDHI tufungulieni codes.
---
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa amesema kuwa ameandika barua kwenda kwa Waziri wa Katiba na Sheria kufuatia jaji mmoja wa mahakama kukiuka kanuni za taaluma.

Waziri Silaa akihitimisha hoja ya bajeti yake bungeni amesema kuwa mwaka 2015 jaji huyo alikuwa wakili, na akamsaidia tapeli mmoja kuchukua ardhi ya watu.

Amesema warithi wa aliyetapeliwa walipoenda makamani hivi karibuni, wamekuta wakili yule sasa ni jaji, bado akaamua kwa kumnufaisha tapeli.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria, na kwamba jambo hilo amelichukua yeye ili kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake na haki inapatikana.

Credit: TBC

Anayedhani kuwa hajapata hukumu ya haki tokana na sababu anazoeleza huyu waziri Jerry Silaa utaratibu wa kisheria si unamtaka apinge hiyo hukumu kwa kukata rufaa mahakama ya juu?

Yeye Waziri anamwandikia Waziri wa Katiba ili iweje? Kwani Waziri wa Katiba ni ngazi ya rufaa ktk mfumo wa utoaji haki wa kimahakama?

Huyo ambaye hakutendewa haki, anapaswa kwenda mahakama ya juu na aielezee scenario yote ya Jaji Y, na X na Z kuwa ndio chanzo cha yeye kutopata hukumu ya haki..

Mahakama ya rufani ikipima sababu za mrufani na ikaziona zina uzito wa kisheria, ni wazi kuwa hukumu ya awali itatenguliwa..

Lakini kama tukitaka nchi iende ki - Makonda Konda au ki - Jerry Silaa silaa, basi tutaishi maisha ya dizaini ya "Animal Farm" au "Shamba la Wanyama" kuwa mwenye nguvu anawatawala wasio na nguvu atakavyo yeye..

Ofcoz, hata mhimili wa mahakama nao uko very much compromised. Na umeharibiwa na mfumo wetu mbovu wa kikakatiba na utawala. Na hili lilijidhihirisha zaidi wakati wa u - Rais wa John P. Magufuli...

Huyu Jerry Silaa na Paul Makonda bado wanaishi ktk mentality ya ki - Magufuli na wanataka kuuendeleza kwa kuielekeza mahakama ifanye vile watakavyo wao kinyume cha taratibu na sheria..
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Wwe lazima utakua wale Mawakili wa mchongo wasio taka kesi ziishe ili waendelee kula kwanza, kesi gani inaendeshwa kwa miaka kumi,kama siyo utapeli huo!?
 
Back
Top Bottom