Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Mahakana kutozingatia haki ndiyo kunakoleta picha mbaya.
Lakini Serikali ina uwezo na haki ya kuilalamikia mahakana and vice versa.
 
Hii imenikumbusha yule jaji aliyeamua kesi ya wafanyabiashara wa madawa wakiwemo raia wa Pakistan

Kuna majaji wengine wana mambo mengi sana

Ova
 
Majaji nani anawateua? Wanateuliwa kwa vigezo gani? Kusikia haya madudu kunatia unajisi mahakama
Tulishaonya siku nyingi kuwa utaratibu wa uteuzi wa majaji haufuatwi. Upuuzi huu ulianza enzi za Magufuli kuteua majaji kiholela,nakumbuka kuna hakim mmoja aliteuliwa na Magufuli kuwa jaji simply kwa sababu aliandika hukumu kwa Kiswahili, matokeo yake ndiyo haya kuteua majambazi kuwa majaji. Tunajua kuwa mawakili wengi siku hizi siyo waadilifu kabisa wanauza haki za wateja wao kwa tamaa ya utajiri wa haraka haraka. Ndiyo hapa tulipofika sasa.
 
Jaji kama huyo unamfanyaje Sasa???.

Ndio sababu PAUL MAKONDA, ANAPENDWA KAMA ALIVYOKUA MAGUFULI.

Nchi hii Kwa Sasa tuna

Makonda.... Silaa, Mpina....Mchengerwa...Msambatavangu.... Gwajima..Gwajima Ke, Bashungwa ,

Bado tuna watu bado tunao.
Tena hao Viongozi wapenda haki wote tutawalinda kwa kila namna hadi kwa swala kwenda kwa Mwenyezi Mungu awalinde na maovu ya wasiopenda haki kutendeka!!
 
Ukiona Slaa kaonge vile juwa nyuma yake kuna Rais aliyemtuma akapambane haki za watu zipatikane.

Samia akiwa ni mwanamama hawezi kuwa na ugumu ule ule wa JPM, anatumia wanaume kumfanyia kazi ngumu.

Makonda anaonekana hafai kuwa mkuu wa mkoa lakini kampa cheo, anayapenda anayoyafanya kwani yeye akiwa mwanamama hawezi kuyafanya kwa ujasiri wanaokuwa nao hao anaowatuma.
 
Huyo Jaji muda si mrefu atatimuliwa, na uhakika kwa uongozi makini wa Mama yetu Samia, hatuwezi kuwa na Jaji anatumia taaluma yake kulinda matapeli, ukiona hiyo huyo Jaji ni mla rushwa mkubwa sana na uhakika ataondolewa haraka sana
Kifupi ni kuwa huyo jaji ni jambazi.
 
Anachofanya Silaa ni kujaribu kuingilia muhimili wa mahakama, Jambo ambalo siyo Sawa na haileti picha nzuri, aache watu waende mahakamani kujitetea au kujibu mashtaka waliyoshtakiwa nayo, atakayeibuka mshindi basi ndio ameshinda
Huna hata haya ndugu yangu!
 
Nchi yetu tuna mifumo ila haifanyi kazi, na ndiyo maana kina makonda wanajizolea pointi 3 kila kukicha kutatua migogooro ambayo ki uhakisia haitakiwi iwepo.

Yaani mkandalasi anafanya kazi ya Halmashauri anamaliza afu miaka 07 hajalipwa, kichekesho.

CCM ishajichokea kila kona.
 
.wamezoea kuchezea mahakqman sasa mwendo wa kulipuana mkuuu unajua ghara.ma za kufika mahakama kuu ama rufaniii???Mungu akiamua kusimama anatumia...hata viongozi mkuuu tukia Singapore iwaaingieee kuna mtu katumiwa barua ya kujieleza mkuu uwe mpoleee tu

M.mahakaman sifiki yaaan nakuavha unajenga nakujakubokoa ukanishtakii mahakaman mm
 
KAMA UNAMJUA MUULIZE MAAGIZOO ALIYOPOKEA LEOOO KAZI IENDELEEEEE MKUU
 
Mara kadhaa imetokea baadhi ya watumishi hasa wa umma wanapowaumiza wananchi baada ya muda wanapandishwa vyeo, nadhani siyo sawa kabisaa.
 
sasa uhatari wake upo wapi, wakati wewe huna pesa, na amekusaidia kukukopesha? mkiwa na shida mnaenda kwao, mkishindwa kurudisha deni mnaamua muwauzie tu nyumba mnalalamika kuwa ni watu wabaya. ongea kwa facts, ubaya wake kwa hiki ulichoongea ninini?
Kwani ni wewe ndiyo Valence Matunda? Mumezoea vya kunyonga. Subiri muziki wa Jerry Silaa
 
Wewe jamaa hauko mbali na mfumo kandamizi. Wewe kama siyo dhulumat wa viwanja basi uko karibu na majaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…