Video Clip: Jerry Silaa adai kuna Jaji anamlinda tapeli wa viwanja

manake ameshindwa kwenye evidence na mchakato wa nje, ameona akimbilie bungeni ili mhimili mmoja utuhumu mhimili mwingine. pia, anaharibu kesi sasa manake kama ameshatuhumu na yeye ni waziri, watakaochunguza watakuwa huru kiasi gani?
Kumbuka huyo jaji na tapeli wana watu na pia wanaweza kuharibu ushahidi.
Kama waziri, anashindwa kukusanya ushahidi kimya kimya kisha akapeleka Takukuru na yeye akawa kama msimamizi mkuu?
 
kama nakumbuka, ile clip ninayo, sio kwamba nyaraka zimebadilishwa, yule anayesemekana ni tapeli anayo hati halisi hadi leo ipo vilevile, ila baada ya kugoma kuitoa, wizara ndio wakatoa duplicate ili mlalamikaji abadilishe umiliki na auze. kwahiyo huyo anayetukanwa kwamba ni tapeli hajabadilisha kitu, yeye kabaki na mikataba ileile halisi na title ile ile halisi. na wakija kwenye issue ya mil.200 wanazodai mahakama ilisema apewe, kama anachodai huyo jamaa ni cha uongo kwanini walikubali kudeposit 1b kama hawakuwa naw ajibu kufanya hivyo?
 
Kumbuka huyo jaji na tapeli wana watu na pia wanaweza kuharibu ushahidi.
Kama waziri, anashindwa kukusanya ushahidi kimya kimya kisha akapeleka Takukuru na yeye akawa kama msimamizi mkuu?
angefanya hivyo, takukuru wangekuja na taarifa nzuri sana ambayo ingesaidia kuunda tume na kumwondoa huyu jaji. hadi hapa jerry kaenda bungeni kamwaga confidential trap, jaji na washirika wake watapambana kupoteza ushahidi na hakuna kitakachowapata. pia, huyo tajiri kama amesavaivu hivi miaka yote, unafikiri hana watu?
 
Sheria za Tanzania kwenye suala la ardhi ni mbovu. Zinaangalia makaratasi zaidi.
Wewe ukiwa na kiwanja chako, nikienda kukitengenezea hati, tayari wewe unanyang'anywa ukumbuke viwanja tunarithishana kwa mababu.
 
Kama ndio ivyo hata huyo Jerry Silaa asingeaika maana kuna ushahidi gani huyo mlalamikaji ana haki na ardhi husika.

System ya ardhi ina record kuanzia mtu wa kwanza anaepewa offer ya eneo ata akiuza huko mbele bado wanatunza info za historia ya wamiliki wote. Sasa wewe ukienda kufanya utundu wako jina la umiliki likabadilishwa bado wamiliki wa awali wanabaki kwenye records za ardhi.

Kwa ivyo mmiliki wanyuma akijitokeza na kudai kiwanja ni chake wewe mpya inabidi ueleze umekipata vipi bila ya ridhaa yake au kuuziwa na yeye.

Isitoshe maamuzi ya mahakama sio rahisi kupingwa hata na vyombo vya kuchunguza rushwa kama PCCB na TAKUKURU ni hiyo tume yao ndio inamamlaka ya kuamua kwanza.

Jerry yeye anafuata taratibu hakurupuki tu kisa waziri na kutumia madaraka yake vibaya.
 
Sheria za Tanzania kwenye suala la ardhi ni mbovu. Zinaangalia makaratasi zaidi.
Wewe ukiwa na kiwanja chako, nikienda kukitengenezea hati, tayari wewe unanyang'anywa ukumbuke viwanja tunarithishana kwa mababu.
Ndio wanavyo jiongopeaga ivyo matapeli; record za ardhi ni traceable kuanzia mmiliki wa kwanza.

Unaweza badili ukajipa umiliki kwa utapeli lakini aina maana records za mmiliki wa awali ardhi zinapotea, sasa akitokea inabidi uelezee hiko kiwanja umekipataje.
 
unachotakiwa kuelewa ni kwamba, pale hakuna mgogoro wa umiliki wa ardhi, huyo tajiri aliingia mkataba wa kiuwekezaji na marehemu, akawekeza pesa ndefu, na akapewa hati halisi ambayo ndiyo anayo hadi leo hajabadilisha. kwahiyo ushahidi uliopo ni mikataba ambayo walalamikaji wote wapo na picha zao zipo na saini zao, wamepata mwekezaji au mnunuzi mpya awanataka kumpiga chini huyo tajiri ili waendelee na maisha yao, hapo ndipo mgogoro ulipo, jamaa kasema basi nirudishieni pesa niliyowekeza niwarudishie hati yenu, hawataki. yeye kafungia hati ile ile halisi kwenye kabati.
 
Kumbuka huyo jaji na tapeli wana watu na pia wanaweza kuharibu ushahidi.
Kama waziri, anashindwa kukusanya ushahidi kimya kimya kisha akapeleka Takukuru na yeye akawa kama msimamizi mkuu?
Wwe usicheze na hao Matapeli wa Aridhi, wana mtandao mpana hadi huko Takukuru unako sema wwe!!
 
Na hili Ndio Tatizo Unakuja Waziri amekuja na bidii ya kutumikia Taifa
Mwisho anakutana na Manguli Serikalini na Mahakamani au chamani Chamani Wanawakingia kifua Mabedui
 
OK this is developed information to me sina hii background. As yet hoja zangu ni kutokana na ka clip ka waziri.

Ngoja niishie hapa mpaka nitakapo lielewa sakata lote, nimeona video kwenye hii mada sijui ndio mfanyabiashara mwenyewe ngoja nimsikilize na yeye.
 
Ndiyo maana yule Tapeli Mmasi alitolewa nishai na Silaa baada kujimilikisha Nyumba ya Marehemu kwa njia za utapeli, kumbe Marehemu anamiliki ile hati toka mwaka 1985, tena nasikia tayari amekutwa na kesi.ya kujibu kwenye kesi yake ya kugushi nyaraka za uhamisho!!
 
Ngoja nisikilize hizo clip na mimi badala ya kuendelea kujiropokea tu without all the details.
 
Tumesema repeatedly, Makonda ni kilaza no doubt ila anafanya kazi ambayo mahakama imewashinda na CJ hashtuki kapoa kama uji wa mgonjwa.

Chakushangaza, badala ya kuhangaika kurekebisha mambo, ili mahakama ipate heshima na kuaminiwa, wanakazana kupambana na Makonda. Another fatal error of judgement in their approach
 
Angalia upande mwingine.

What if judge mkuu anatenda kwa remote? Maybe anasubiri directions afanye nini na hapa kaambiwa, “sshs, keep quite, it will pass”, na yule yule aliemuweka hapo?

Maana Kama “kawekwa, ni lazima afate directives.

Na hata huyo atakaewekwa atafanya maajabu yapi tofauti na “mamlaka iliyomuweka?

Uwajibikaji Tanzania, is a long lost dream. Very unfortunate.
 
Shida ipo kwenye mifumo ya upatikanaji haki,Fedha imekuwa kachumbali muhimu..Huna pesa ya kutosha huwezi pata wakili mzuri..Mawakili wazuri ni ghali na adimu..

Kama ilivyo kwa elimu na afya..Una bima? Ipi?ya Wapi?..Una watoto? Wanasoma nini na wapi?

Haki imekuwa bidhaa inauzwa na kununuliwa..Naamini majaji jamii ya kina Samatta,Mwalusanya?Nyarali kama wapo ni wachache..Wenye wivu wa kutoa na kumimina haki..
 
Tunajadili mambo serious na wewe unaleta ya Zerobrain
Wenye brain wanaivuruga nchi kiasi kwamba sisi wenye zero brain tumeshituka. Na cha kushangaza, kule mkoani, sababu ya hizi tambo na majigambo,zero brain mwingine anaongoiza race so far.

Mnajidanganya sana nyinyi mnaofikiria mna akili na mnaweza kufanya kitu chochote cha kuharibu desturi na taratibu njema, bila kupata madhara yoyote. Eti kwa sababu mna akili. Akili zenyewe ni zile mnazosema tumesomea this and this na tuna this degree.

Hata kama usomi wenu ni kufanya kazi zenye ubora hafifu na kuongea mambo yenye kutoa ushuzi mwanzo mwisho
 
hao majaji wengine hata hawaogopi, wapo wengine walikuwa kwenye taasisi walikuwa wanalipwa karibia 10m, marupurupu rundo, wamepewa ujaji wanalipwa kama nusu ya hiyo hela na marupurupu kidogo, wengi wanatamani hata kuacha. ila ndo hawana pa kwenda. wengine wanaamua wapige rushwa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…