Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
-- Bwawa limeelemewa na maji, namna ya kuliokoa lisivunje kuta zake ni maji kuachiwa, matarajio ni kwamba maji yataachiwa na lita 700,000 kwa sekunde zitamwagwa
-- Wananchi wameanza kuambiwa kuhama sababu maafa yanayokuja ni makubwa
-- UNESCO waonya kuhusu mafuriko kusabibishwa na bwawa, Mwalimu Nyerere aliambiwa kuhusu hii hali, Mwalimu akaona hapana tuachane na hili bwawa
-- Hili Bwawa linachangamoto moja, linamwaga maji wakati maji yanaelekea kwenye maeneo yenye shughuli za utalii, makazi ya watu na maeneo ya kilimo
-- Changamoto hizo zilionekana mwaka 1970 wakati huo kulikuwa na population ndogo rufiji
-- Kwa sasa serikali ina changamoto ya kulinda usalama wa bwawa kutovunjwa na maji, lakini pia kuzuia maji na kuyaachia kwa kasi pia, kwenye hii operation kama bwawa litavunjika litasomba rufiji yote na chochote mbele yake, Njia salama ni kuachia haya maji kama wanavyofanya sasa, lakini shida ni kwamba hawataki kuwaambia wananchi ukweli, wanatakiwa kuhamisha wananchi na kuwalipa usumbufu, kwa maji yanayokwenda kuingia kwenye bwawa ili bila kuyaachia kwa kasi bwawa zitavunjia
-- Makadirio ya kuachia maji ili bwawa liwe salama ni 700,000 lita kila sekunde , kwa maana nyingine ni kuachia maji ya kujaza uwanja wa mpira wa mkapa ndani sekunde 2 au chini ya hapo
Haya maji yanakwenda kusomba watu, serikali iwe wazi, maana kuna tahadhari ya mvua kunyesha,
-- Haya maji yakiachiwa yataijaza wilaya ya rufiji kwa kimo cha 1.8 mita , wilaya yote ya rufiji
-- Mbili haya maji yaliyoachiwa na yanayoenda kuachiwa sio ya kuzalisha umeme, ni kwamba maji yameingia kwa wingi kwenye bwawa na bwawa alina uwezo wa kuimiri hivyo wanayafungulia ili kingo vya bwawa zisije vunjwa, na wanaelekea kuachia maji mengi zaidi ili kuokoa bwawa sio kuzalisha umeme hapana ni kuokoa bwawa maana waliaenda kujenga bwawa kwenye eneo lenye mto mzito bila kuzingatia athari za mazingira, kujenga bwawa kwenye mto kama rufiji iliitaji tekinologia kubwa sana na pia fedha nyingi sana zilitakiwa kutumika kutokana na hali ya kijiography ya mto, kwa maana nyingine huu mradi ulikuwa ni hatari , mvua zikipiga basi lazima maji yaachiwe vya kutosha.
Kwa sasa wamefungua milango 4 tu na bwawa lina milango 9 na katika hiyo 4 ambayo ni chini ya nusu tayari rufiji imezama, sasa sijui wakifungua full scale itakuwaje yaani 9 ili kuokoa bwawa, na swali kubwa ni je ili bwawa liko salama? tutadumu na ili bwawa kwa muda gani kama haya maji yakijaa yanakuwa mengi kiasi kikubwa hivi ?
Mungu ilinde rufiji, Mungu walinde Watanzania