Video: CZA wa Clouds FM hongera kwako. Mrema ndani ya dakika 3 kapata kigugumizi, kashindwa kuelezea "No Reforms No Election"

Video: CZA wa Clouds FM hongera kwako. Mrema ndani ya dakika 3 kapata kigugumizi, kashindwa kuelezea "No Reforms No Election"

Wakuu,

Yaani CZA wa Clouds FM amefanya kazi ya kitume sana.

Ndani ya Dakika 2, Mrema ameshindwa kuelezea na kutoa tafsiri ya No Reforms No Election yaani anajikanyaga tu.

Hapa ndo unajua kina Mrema ni project ya CCM na walikuwa ni mapindikizi.

Chezea diko la ma nigga rungwe!!!
 
..Tundu Lissu ame-earn trust ya wananchi ndio maana wananchi hawakuwa na tatizo naye alipochangiwa na Ccm. In fact Ccm walilenga kumkejeli walipomchangia.
Mpenda chongo..... Hamtaki criticism yeyote ya Dear Leader! Hamuulizi michango ya gari imefikia wapi na gari liko wapi? Alichangiwa na watu pesa za kulipia fomu ya kugombea lakini tukaambiwa Sativa kalipia fomu bila kuelezwa michango ilikuwa kiasi gani na kafanyia nini. Amekataa kuchangia Mkutano Mkuu mkamezea. Mtu wenu ana miguu ya udongo na hii blind loyalty itawafikisha pabaya.

Hamuoni kosa kwake lakini mnakimbilia ( sio wewe binafsi) ku spread spurious rumours dhidi ya wale wanao tofautiana nae. Kuanzia pesa za mama Abduli hadi ya mabilioni ya pesa kutoka X! Kwa kweli inasikitisha.

Amandla..
 
Wanapaswa kusikilizwa, haina maana maoni yao yasikilizwe kwa lazima. Chama chenye wafuasi kina mitazamo tofauti , maamuzi hufikiwa kwa pamoja hata wale wasiokubaliana nayo.
Mbona uliwabeza wakina Mrema kwa kutaka hoja zao zisikilizwe kwa kusema kuwa wamesahau kuwa sasa hivi ni wanachama wa kawaida? Kusikilizwa ni muhimu ingawa sio lazima kufuata ushauri wao.
Kwa mfano, CHADEMA karibia 70% hawakukubaliana na maridhiano lakini ilipoamuliwa na vikao ikabidi
Adhabu ya kutowasikiliza ikatolewa Mlimani City, watu wakapoteza kazi zao. Ndivyo inafanyika
Mbona unaanza kuwa muongo.? Hiyo tathmini ilifanywa na nani? Ingekuwa Mbowe alikataliwa kwa sababu ya Maridhiano basi Lissu angemshinda kwa zaidi ya asilimia 70! Au alimshinda kwa 70% lakini sisi wengine hatukuona?

Hata wakina Mrema wanaweza kusema asilimia 90 ya wanachama wa CDM hawakubaliani na NRNE.
Akina Kigaila na Mrema wanapoongoza makundi kuondoka kwasababu hawasikilizwi, who are they!
Kwani ni mara ya kwanza maamuzi kufanyika kwa kutofautiana. Ni vyeo na vibuyu vya asali! wanavyo!
Walioondoka CDM hawakuondoka kwa sababu Mrema kasema. Kusema hivyo ni kuwatukana wakina Ruge, Kiwanga Aisha, Mwalimu na wengine. Wote hao ni watu capable kabisa ya kuamua wanachotaka na miaka yote wamefanya hivyo.
Sina neutrality, nasimama upande wenye ukweli kwa mujibu wangu.
Ukweli is in the elections of the beholder. Kweli yako sio lazima iwe kweli yangu.
Ndiyo maana nasema wazi, I don't support CCM. Chama kinachoweza kuwatia msuko suko nakiunga mkono. Sijawahi kuongelea Chaumma na sera ya Ubwabwa, sioni tatizo na sera
Ni haki yako.
Nipo katika rekodi JF nikisema akina Kigaila, Mrema , Mwalimu na wafuasi wana haki ya kuhamia chama wanachotaka! Swali, kwanini ninawasema sasa hivi?
Jibu ; wanapotosha Umma! hawana sababu za kuondoka, kila mmoja anazua zake
Kuna Ubaguzi- Boni yai katoa takwimu za kuonyesha hakuna ubaguzi huo
Kwa vile Boni Yai hajabaguliwa haimaanishi kuwa hakuna aliyebaguliwa. Hoja ya kubaguliwa na kubezwa imesemwa na wengi tu. Hata yule dada aliyemtumia kama propaganda kuwa amerudi CDM aliwaambia waache kelele na kutenga wenzao. Mbele yake. Na Boni ametoa takwimu zipi? Boni ameamua ku kiss the ring lakini hawezi kuwasemea wenzake. Asikubali kutumika. Mbona wenzake wanaunga mkono NRNE bila kuwasemea vibaya waliohama CDM?
Chama kimepoteza uelekeo- hawaelezi ni upi
CHADEMA ishiriki uchaguzi itashinda Ubunge na udiwani
Kamati kuu haijakaa kujadili suala la Tundu Lissu

Ukisoma hoja hizo, ni utter nonsense! Kigaila hajaonyesha wapi katiba inataka mtu akikamatwa kikao cha kamati kuu kiitwe. Kigaila anatoa mfano wakati wa Mbowe, amesahau yeye si naibu KM tena
Nonsense gani? Mwenyekiti wa chama anakamatwa lakini Kamati Kuu haikai kupanga nini cha kufanya? Hasa ukizingatia kuwa ilikuwa haijakaa toka utawala mpya kuingia madarakani. Imekaa baada ya Devotha Minja aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu kuwakumbusha.

Hizo kwangu mimi ina harufu ya udikteta uchwara. Chama kinaongozwa na ka Cabinet ka jikoni. Hii ni tofauti na uongozi wa Mbowe ambae inaelekea kuwa alikuwa anawasikiliza wenzake. K.m. binafsi naamini kuwa alitaka kuwasamehe wakina Halima lakini wenzake walipompinga akakubali wafukuzwe na akasimamia uamuzi huo.
Kigaila na Mrema wanasema wakishiriki CDM itapata ushindi, stupid! Hawa ni viongozi chaguzi zaidi ya 5.
Ya 2019, 2020, 2024 yametokea katika mikono yao! leo wanafanya Watanzania wapuuzi !
Hakuna chama kinachoingia katika uchaguzi na kusema kuwa kitashindwa. Hata Lipumba anasema atashinda. Ndivyo inavyopaswa kuwa. Wakishindwa watapambana tena mpaka washinde. Ndio upambanaji.
Ukisoma hayo utabaini hawa Kigaila, Mrema na Mwalimu ni matapeli fulani waliotaka vyeo.
Wana haki ya kuhama, sababu za kuhama ni none sense! Sasa hivi wamepata vyeo watulie!
Una personal animus dhidi yao kiasi kuwa hauoni kuwa unachosema ni nonsense. Hauwezi kumwambia mwanachama wa chama kingine atulie kwa sababu tu haumpendi. Ni wajibu wao kuelezea umma msimamo wao kuhusu No Elections. Umma ndio utaamua na sio JF na Space za kwenye mitandao. Ni wajibu wa CDM kuelezea umma hiyo No Elections itatekelezwa vipi unless kama njia watakazotumia ni kinyume na Katiba na Sheria.
Ukiona ujinga kama huo huhitaji neutrality, unauzunguzia , unaukemea kwasababu ni upuuzi , period.
Mradi hauukemei kizushi. Unachoona wewe upuuzi wengine tunaona una mantik ndio maana nasi hatusiti kuwapinga mnaotaka kupotosha wanacho sema.
Rose Mayemba ni mjumbe wa Kamati Kuu, hana nafasi ya kulipa kisasi. Just for the record ''architect'' wa vengeance ni Kigailam alimnyanyasa sana Rose Mayemba. Kinachomtokea ni Karma!
Rose Mayemba amemshughulikia sana Sigrada. Na bila shaka ameshiriki katika maamuzi ya kuwa shughulikia wakina Kigaila. Ni vengeful sana.

Kinacho ni shangaza ni kwa mnahangaika na watu ambao mnasema kuwa walikuwa cancer katika chama chenu? Kwa hii chuki mliyokuwa nayo dhidi yao mngewafanyia kitu kibaya wasingeondoka. Mngewasingizia upuuzi wowote. Kama ule wa kula hela za Twitter.
The point is, wali own accounts! Je, wamerudisha kwa uongozi mpya!
Ndio mmejua miezi mitatu baada ya kuchukua uongozi? Mlishindwa nini ku take ownership mara mlipoingia madarakani? Na kama mliona wanazengua si mnge wa ripoti kwa Elon Musk?

Wakati mkifanya hivyo mtuambie pia nani anamiliki accounts za Twitter za Chadema Diaspora, Chadema Nyasa, Bavicha, Bawacha n.k. Na mtuambie mabilioni wanayopata toka kwa Musk wanapeleka wapi?

Ushauri wangu ni angalieni uwezekano wa kumiliki domain zote zenye neno Chadema. Kama hamja fanya hivyo msilaumu mtu akifungua website ya CHADEMA.com , Chadema. org NRNE.com, account ya X ya Chadema NRNE n.k.
Tarehe 22 March kama sikosei niliwatahadharisha CHADEMA, barua ya Mchome ilipaswa kufuata taratibu za Chama. Kitendo cha kunukuu kwa Msajili kina maana kubwa sana.
Bureaucrats kama kawaida. Hili jambo lilitakiwa lipewe priority, sio kusingizia taratibu. Barua aliandikiwa Mtendaji Mkuu wa Chama na alipaswa kuchukua hatua na sio kusubiri tawi lililomwandikisha Mchome limshughulikie. Uongozi makini unatambua jambo la hatari na kulidhughulikia mara moja.

Kiburi kinawaponza na kitaendelea kuwaharibia. Kama waliona kuwa hoja ya Mchome haina mashiko wangeomba Mahakama iweke zuio. Hao ma lawyer wabobezi waliosheheni CDM hawakutambua hatari iliyokuwemo kwenye barua ya Mchome? Barua ilionyesha wazi kuwa kuna nakala imeenda kwa Msajili hivyo walipaswa kuipa umuhimu.

Mchome angeweza kuipeleka moja kwa moja kwa Msajili kwa kificho. Kiyendo alichofanya ni cha kiungwana. Lakini sikio la kufa halisikii dawa. Mmebaki sasa kukwepa kuwajibika. Mbona ACT Wazalendo waliweza ku neutrality barua kama hiyo? CDM inashindwa nini? Badala ya kushughulikia hoja zake mnakimbilia kumchafua kwa kudai kuwa analipiwa nyumba na Msajili bila ushahidi wowote. Ovyo kabisa.

Naanza kuamini kuwa kuna insidious plot ya kuihujumu CDM inayofanywa na baadhi ya viongozi wa sasa.
Niliwatahadhrisha ima warekebishe kosa au watoke na kujibu tuhuma, walipuuzia! Wana pay the price
Niliwapa mifano ya NCCR, CUF n.k. nikiwaeleza Mchome ni chambo, kuna wenye issue
Kumbe kinachokusumbua ni kuona kuwa walikupotezea? Price gani waliyolipa wakati sasa hivi wako huru kufanya wanachotaka. CDM sio Alpha na Omega. Sasa hivi future yao iko mikononi mwao na sio mtu mwingine. Aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA Devotha Minja amesema kuwa huko waliko wana peace of mind. Hilo ni muhimu kulko cheo chochote.
Kupiga kura isiyohesabiwa ina maana gani? definition ya Insanity ni yanayoendelea. Kama akina ACT Wazalendo wangeunga mkono CDM , CCM isingefanikiwa.
Bahati mbaya ACT wameridhika kuwa chama cha pili Zanzibar, Bbara wanataka ruzuku tu !
Mmewatukana sana ACT-WAZALENDO pamoja na viongozi wake kama ambavyo mnafanya sasa dhidi ya Chaumma. Lakini bado mnataka wawasujudu.

Kama kweli mnaona mkiungana mnaweza kuishinda CCM kwa nini msiungane na ACT-WAZALENDO ambao wana base ya uhakika Zanzibar? ACT-WAZALENDO haijakata tamaa kama nyinyi ndio maana inaendelea kupambana maana wanajua iko siku haki itatendeka.
Bila kufuata NRNE, mwenye akili timamu hawezi kupiga kura! Unapiga kura ihesabiwe na kuheshimiwa. Kama haihesabiwi wala kuheshimiwa unapiga ili iweje?
Unapiga kura kuonyesha kuwa hautakata tamaa kupigania haki yako. Kuonyesha kuwa pamoja na kujua kuwa utadhulumiwa lakini utaendelea kupambana. Ku sulk na kususia ni cowardice.
Unapiga kura Bunju mtaa X kura inaenda kuhesabiwa Ilala! huu kama si upuuzi nishawishi ni nini.
Pengine kuna mahali sielewi, hebu elimisha Umma kwenda kupiga kura ni ili iweje!
Unapiga kura kuonyesha kwa sababu ni haki yako. Anaekufanyia fitna anafanya hivyo kwa sababu anakuogopa na sio vice versa.

Umma ungepuuza zuio la mikutano ya hadhara tusingekuwa hapa. Wangeona kuwa umma uko tayari kuumizwa kutetea haki yao ya kikatiba mapema tu wangeacha kuizuia.
Nimeshiriki chaguzi za chama kimoja na vyama vingi. Maalim Seif tangu 1995 anashiriki hadi anafariki.
Hivi ni mapambano gani waliyobakiza tena! Unakumbuka Tume ya Pamoja ya Uchaguzi Zanzibar! matokeo yakapinduliwa na Jecha! CUF wakati walifanya nini, nothing! Hakuna kwenda mahakamani.
Hayo si mapambano ni insanity. CDM wameona ya CUF nadhani wakasema hawakubali insanity
Insanity ni kuacha kupambana kwa sababu tu mpinzani wako ni mbabe. Inawezekana kizazi hiki hakitaiondoa CCM kwenye madaraka lakini iko siku kitatoka. Ilichukua zaidi ya miaka 60 kukiondoa chama tawala cha Mexico madarakani lakini kiliondoka. ACT-WAZALENDO na sasa Chaumma kinasema kuwa hawatakata tamaa hata iweje. Wanatakiwa kupongezwa, sio kubezwa.
Kula nusu mkate kila siku ukidhani ni mkate mzima si ujinga huo! Na ujinga zaidi ni kuamini Rais Mzanzibar atawafanyia hisani mwaka huu! Hawajui CCM ni CCM tu , CCM mzuri ni yule aliye kaburini.
Hiyo ni imani yako. Wengine tunawajua wanachama wa CCM ambao ni watu wema tu.
At least wana credibility ukilinganisha na wenzao. Think about this, ACT Wazalendo walikuwa moto na Muungano! umewasikia tena siku hizi. Kisa Rais ni 'mwenzetu' hawa unawaamini kwa nini.
Muanglie mtu kama Zitto ! anaamini wakipata Wabunge 5 wataweza kufanya mabadiliko nchini
Again, una ruhusu chuki binafsi itie kiwingu katika kufikiri kwako. Zitto ni mpambanaji ndio maana ACT-WAZALENDO imefikia ilipofikia.

Ninachojua mimi ni kuwa ACT-WAZALENDO haijaacha kuzungumzia suala la Muungano. Hata mbunge mmoja ni afadhali kuliko kutokuwa na mbunge kabisa. Tumeona Aidan anavyohakikisha masuala ya uonevu dhidi ya viongozi wake yanavyoingia bungeni. Wanampuuza lakini umma unamsikia na yanaingia kwenye hansard. Asingekuwemo isingekuwa hivyo.
Chama kingine ni vya brief case ikiwemo Chaumma cha Kigaila na Mrema, hawa utawaambia nini wakiwa wamekabidhiwa vibuyu vya asali, wanalamba. Wamejaa katika mfumo! unawashirikisha kwa lipi
Majuzi Boni ametumia muda wote aliokuwa jukwaani kumsifia na kumshukuru mtu ambae mlitaka kutuamikisha kuwa alilamba asali. Mnachojua ni kufanya character assassination kwa kila anae tofautiana nanyi.

Achaneni na wakina Kigaila, wale sio wanachama wenu. Jibuni hoja zao, msikimbilie matusi. Mnavyofanya hivyo mnazidi kuthibitisha kuwa kweli vilivyokuwa vichwa CDM vimehamia Chaumma na waliobaki wanajua kutukana ( kuwaita wenzao punda) tu na kusema uongo ( Mrema alikuwa anapokea mabilioni kutoka Twitter).

Jirekebisheni. Adui yenu sio Chaumma, ni CCM. Chaumma ni mshindani, sio adui wenu.

Naona niishie hapa nime exhaust kila ninachotaka kusema. Kuendelea kujibishana na wewe ni kujipotezea muda tu.

Amandla...
 
Mpenda chongo..... Hamtaki criticism yeyote ya Dear Leader! Hamuulizi michango ya gari imefikia wapi na gari liko wapi? Alichangiwa na watu pesa za kulipia fomu ya kugombea lakini tukaambiwa Sativa kalipia fomu bila kuelezwa michango ilikuwa kiasi gani na kafanyia nini. Amekataa kuchangia Mkutano Mkuu mkamezea. Mtu wenu ana miguu ya udongo na hii blind loyalty itawafikisha pabaya.

Hamuoni kosa kwake lakini mnakimbilia ( sio wewe binafsi) ku spread spurious rumours dhidi ya wale wanao tofautiana nae. Kuanzia pesa za mama Abduli hadi ya mabilioni ya pesa kutoka X! Kwa kweli inasikitisha.

Amandla..

..tuombe MUNGU Lissu asinyongwe katika kesi ya uhaini ili tupate muda wa kumhoji kuhusu michango.

..pia Lissu ni mlemavu kwa kuumizwa na watu wabaya, sasa sio vizuri kumtolea mifano ya kejeli kwamba ana " miguu ya udongo. " Kuwa muangalifu na mifano unayotumia.
 
Wasaidie Chadema kwa kutufafanulia namna No Elections itakavyofanikishwa. Sioni ugumu wa kutenganisha NR na NE wakati NE ni matokeo ya NR. Kwa kifupi, kama hapatakuwa na reforms hapatakuwa na elections. Kwa vile ni wazi kuwa hapatakuwa na reforms basi mnabidi kutuambia NE itafanikishwa vipi.

Chaumma haina uhusiano na CDM kwa hiyo ni wajibu wao kuainisha tofauti zilizopo kati yao. Chaumma sio Chadema au CCM lite. Heshimuni uamuzi wao.

Amandla...

..nyinyi mmeshakata tamaa.

..ndio maana unasema hapatakuwa na Reforms.

..muda mwingi nilikuwa naongea na wewe sikujua kama huu ndio msimamo na mtizamo wa Chaumma.

..nyinyi mlipaswa kujiunga na Ccm kwasababu hamko kwenye Reforms, na hamko kwenye No Election.

..kama Tanzania tuliandika Katiba mpya bila vita, tukaingia kwenye vyama vingi bila vita, basi tunaweza kuahirisha uchaguzi bila vita.

..Uchaguzi uahirishwe, ili kutoa nafasi kwa mabadiliko kufanyika.
 
..tuombe MUNGU Lissu asinyongwe katika kesi ya uhaini ili tupate muda wa kumhoji kuhusu michango.

..pia Lissu ni mlemavu kwa kuumizwa na watu wabaya, sasa sio vizuri kumtolea mifano ya kejeli kwamba ana " miguu ya udongo. " Kuwa muangalifu na mifano unayotumia.
Hatanyongwa maana hamna kesi pale. Wanamuonyesha tu kuwa wanaweza kufanya lolote. Kama walivyomfanyia Mbowe.

Amandla...
 
..nyinyi mmeshakata tamaa.

..ndio maana unasema hapatakuwa na Reforms.

..muda mwingi nilikuwa naongea na wewe sikujua kama huu ndio msimamo na mtizamo wa Chaumma.

..nyinyi mlipaswa kujiunga na Ccm kwasababu hamko kwenye Reforms, na hamko kwenye No Election.

..kama Tanzania tuliandika Katiba mpya bila vita, tukaingia kwenye vyama vingi bila vita, basi tunaweza kuahirisha uchaguzi bila vita.

..Uchaguzi uahirishwe, ili kutoa nafasi kwa mabadiliko kufanyika.
Sisi ni pragmatism. Ni kujidanganya kudhani kutakuwa na reforms kabla ya uchaguzi wa mwezi wa 10. Watatumia kisingizio cha muda hautoshi. Hawa ndio watu ambao mlipodai tume huru ya uchaguzi wakaongeza neno Huru na kubakiza kila kitu. Tunachosema sisi ni kuwa mpambano utaendelea.

Mimi siwaelewi mnaposema uchaguzi uhairishwe. Hamuoni kuwa mtaipa serikali muda zaidi wa kuongoza nchi. Hiyo ni pamoja na wabunge wao.

Ni wazo baya sana

..sio wazo baya kuahirisha uchaguzi.

..uchaguzi umeshawahi kufutwa, sasa tunashindwa nini kuahirisha?

..uchaguzi unaahirishwa kwa malengo mazuri ya kuleta MABADILIKO.

..kama tuliweza kuandika Katiba Mpya bila vita, basi tunaweza kuahirisha uchaguzi bila vita.

Cc Nguruvi3
 
Uchaguzi wa JMT haujawahi kuahirishwa au kufutwa. Uliofutwa ni wa SMZ.
Swali ni kuwa unaahirishwa mpaka lini? Na nani ataamua kuwa marekebisho yaliyofanywa yanakidhi mahitaji. Nini itakuwa role ya Bunge ambalo 99.99 % ni CCM? Si bora kuwe na uchaguzi na kufanya kila namna idadi ya wabunge wa upinzani waongezeke. Wasipoongezeka kutakuwa na miaka mitano ya kushinikiza mabadiliko. Kwa vile Mwenyekiti wa CCM itakuwa term yake ya mwisho anaweza kukubali marekebisho ili aingie katika vitabu vya historia. Akikubali sasa atakuwa Rais wa mwisho wa CCM na hiyo hawezi kukubali. Aidha 2030 CCM watakuwa wanagombea uenyekiti hivyo watakuwa vulnerable zaidi.

Amandla...
 
Uchaguzi wa JMT haujawahi kuahirishwa au kufutwa. Uliofutwa ni wa SMZ.
Alipofariki Dr Omar! haukuahirishwa?
Swali ni kuwa unaahirishwa mpaka lini?
Hata miaka 3 au 4, hoja si kufanya uchaguzi 'for the sake''. Ni kufanya uchaguzi meaningful
Jifunze kwa ''ACT Wazalendo'' a.k.a CUF, walikwenda mbio wakaitaka uchaguzi wakasahau mambo mengi yanayohusu uchaguzi. Tume huru haikuwasaidia kwasababu mfumo mzima haukufumuliwa.
Na nani ataamua kuwa marekebisho yaliyofanywa yanakidhi mahitaji. Nini itakuwa role ya Bunge ambalo 99.99 % ni CCM?
OMG! kwani sasa hivi Bunge ni % ngapi! Hata kama CCM itakuwa 60% nini kitawazuia ikiwa 2/3 ndicho kigezo.
Si bora kuwe na uchaguzi na kufanya kila namna idadi ya wabunge wa upinzani waongezeke.
Wataongezeka kwa akili gani? Mwaka 2015 walikuwa zaidi ya 50, Magufuli akafuta 2020 akabaki 1. Unataka kueleza kwamba CCM walishinda kwa halali ndio maana idadi ilipungua.
Tufanye Chaumma watapewa na CCM Wabunge 10 na wakuteuliwa 4. So what!
Wasipoongezeka kutakuwa na miaka mitano ya kushinikiza mabadiliko.
Badala ya kuanza sasa unasubiri kutoa ''uhalali''. Hivi unaishi nchi gani kwa kudhani CCM watawapa CCM B hata viti 5. Muulize Mbatia na Selasini.
Kwa vile Mwenyekiti wa CCM itakuwa term yake ya mwisho anaweza kukubali marekebisho ili aingie katika vitabu vya historia.
Alright! anaweza! maisha ya kuhisi na kubuni
 
..uchaguzi unaahirishwa kwa malengo mazuri ya kuleta MABADILIKO.
Hapa ndipo wengi hawawezi kuona kwasababu wanaishi ''kesho'' .
Hata kuahirisha miaka 4 ilimradi kuna mbadiliko ya maana ni jambo zuri
 
Mimi siwaelewi mnaposema uchaguzi uhairishwe. Hamuoni kuwa mtaipa serikali muda zaidi wa kuongoza nchi. Hiyo ni pamoja na wabunge wao.Ni wazo baya sana
OMG! hivi unategemea CCM inaweza kushindwa October 2025!
Unachoeleza hapa ni kwamba kuliko kuahirisha uchaguzi na kuwapa muda, ni afadhali kuwaongezea muda kwa uchaguzi ''fake''.
 
Uchaguzi wa JMT haujawahi kuahirishwa au kufutwa. Uliofutwa ni wa SMZ.
Swali ni kuwa unaahirishwa mpaka lini? Na nani ataamua kuwa marekebisho yaliyofanywa yanakidhi mahitaji. Nini itakuwa role ya Bunge ambalo 99.99 % ni CCM? Si bora kuwe na uchaguzi na kufanya kila namna idadi ya wabunge wa upinzani waongezeke. Wasipoongezeka kutakuwa na miaka mitano ya kushinikiza mabadiliko. Kwa vile Mwenyekiti wa CCM itakuwa term yake ya mwisho anaweza kukubali marekebisho ili aingie katika vitabu vya historia. Akikubali sasa atakuwa Rais wa mwisho wa CCM na hiyo hawezi kukubali. Aidha 2030 CCM watakuwa wanagombea uenyekiti hivyo watakuwa vulnerable zaidi.

Amandla...

..kwani Zanzibar sio Tanzania?

..kama uchaguzi umewahi kufutwa, basi inawezekana kuuahirisha.

..sote tunapaswa kuwa na nia njema, katika mabadiliko tunayotaka kuyafanya, na muda wa kuahirisha uchaguzi.

..huwezi kuingia kwenye uchaguzi wakati Ccm wameharibu mifumo yote, na wanatumia silaha bila aibu wala uoga.

..msikate tamaa katika kudai mabadiliko. Na ni mtakuwa mnakosea kuahirisha kudai mabadiliko mpaka baada ya uchaguzi.
 
..pia Lissu ni mlemavu kwa kuumizwa na watu wabaya, sasa sio vizuri kumtolea mifano ya kejeli kwamba ana " miguu ya udongo. " Kuwa muangalifu na mifano unayotumia.'
Nimeshangaa! so sad. Kwamba anafurahia ulemavu kutoka CCM.
Political discourse should not compromise moral compass.
 
..kwani Zanzibar sio Tanzania?
Sasa ujue CCM walivyokuwa ruthless. Walifuta wa SMZ lakini hawakufuta wa JMT.
..kama uchaguzi umewahi kufutwa, basi inawezekana kuuahirisha.
Swali langu ni lile lile. Uhairishwe mpaka lini? Mnategemea kuwa Bunge hilo mnalotaka liendee litaridhia mabadiliko yeyote yatayoweka viti vyao hatarini? Mnadhani wataona aibu kuendelea kwa miaka mingine tano halafu kumchagua huyu huyu agombee tena kwa sababu ana muhula mwingine wa kugombea? Halafu mnatuona sisi naive!
..sote tunapaswa kuwa na nia njema, katika mabadiliko tunayotaka kuyafanya, na muda wa kuahirisha uchaguzi.
Kama aliyeshika mpini hana nia njema hilo halitasaidia. Huyu ni kushindana nae humo humo mpaka wananchi watakapo mchoka. Wakimchoka, ataondoka tu.
..huwezi kuingia kwenye uchaguzi wakati Ccm wameharibu mifumo yote, na wanatumia silaha bila aibu wala uoga.
Ukisusia, utashangaa atakavyoendesha uchaguzi wa uwazi na haki ili ionekane kuwa ni uoga wenu tu. Na kwa vile mlisusa mtakosa ushahidi wa hizo shutuma zenu. Chaumma na ACT-WAZALENDO wakishindwa itakuwa ni kwa mtindo ule ule wa siku zote kama ilivyokuwa 2024. Hawatakuwa na moral authority ya kudai wanaendesha uchaguzi wa haki na uwazi. Chaumma na Act Wazalendo watatumia miaka mitano ijayo kumbamiza kwa suala hilo hilo ndani na nje ya Bunge. Wakati huo CDM watabaki X na kwenye majukwaa ya diaspora.
..msikate tamaa katika kudai mabadiliko. Na ni mtakuwa mnakosea kuahirisha kudai mabadiliko mpaka baada ya uchaguzi.
Chaumma na ACT-WAZALENDO hawajakataa sera ya mabadiliko. Hata kampeni zao za kuomba kura watapigiloa hapo hapo. Hamna atakayeweza kuwaziba mdomo maana watakuwa na wagombea kila mahali. Chadema watabaki kulalamikia nje kwa sababu wamesusa. Waliokata tamaa ni Chadema, sio hao wengine.

Amandla...
 
Hapa ndipo wengi hawawezi kuona kwasababu wanaishi ''kesho'' .
Hata kuahirisha miaka 4 ilimradi kuna mbadiliko ya maana ni jambo zuri

..Tume Huru iliyoanzishwa inaelekeza kwamba Mwenyekiti, Makamishna, Katibu, wanapaswa kuteuliwa kwa kufuata utaratibu mpya.

..Mpaka hivi tunavyozungumza Rais Samia hajafuata sheria inavyoelekeza kuhusu Tume Huru.

..Sasa kiongozi wa aina hiyo unamuaminije katika kusimamia uchaguzi? Au unaamini vipi ahadi zake nyingine?
 
..tuombe MUNGU Lissu asinyongwe katika kesi ya uhaini ili tupate muda wa kumhoji kuhusu michango.

..pia Lissu ni mlemavu kwa kuumizwa na watu wabaya, sasa sio vizuri kumtolea mifano ya kejeli kwamba ana " miguu ya udongo. " Kuwa muangalifu na mifano unayotumia.
Unajua maana ya miguu ya udongo? Kusema mtu ana miguu ya udongo ( clay feet) hakumaanishi kuwa ana ulemavu. Maana yake ni kuwa ana udhaifu ingawa anaonekana mwamba. Google "clay feet" utaiona.
I hope umesima hivyo kwa kutoelewa na sio kujaribu mbinu yenu ya kawaida ya character assassination.

Amandla...
 
Back
Top Bottom