Ndugu wa Marehem bilionea Msuya akilia mahakamani baada ya washtakiwa wa mauaji ya Aneth Msuya kuachia huru na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es salaam leo Februari 23.
Pia soma:
Hukumu za hivi zenye kuvuta hisia za umma zinatakiwa kutolewa kwa 'haki' isiyopendelea ama kuonesha kuegemea upande wowote.
Iwe ni ya haki isiyotia shaka wala doa kwa jaji ama wakili.
Lakini kwetu sisi Tanzania hasa awamu hii ya6 hakuna kiongozi niliyemuona kutia kurunzi kumulika ufedhuli huu wa kuchezea haki za watu hata kwa maneno matupu, inamaana wanaridhishwa na matendo haya!
Haki ya raia inaweza kukanyagwa wazi mchana kweupe na halafu mhalifu akifikishwa mahakamani anaonekana kuwa hana hatia!
Rushwa tupu!
Watu masikini wasiokuwa na uwezo wa kutoa rushwa wanafungwa kwa makosa saazingine si yao na hawajayatenda na hakuna anayejali!
Chukulia mfano wa ile hukumu ya kesi ya 'nyama ya swala' namna ilivyovuta hadhira ya waTz na jinsi ilivyotolewa!
Ukisikiliza pande zote mpaka mtu unaushangaa weledi wa hakimu huyo aliyetoa hukumu na kujiuliza kuwa huyo mheshimiwa kesi hiyo aliisikiliza tangu mwanzo kweli au alikurupuka kutoa hukumu tu?
Lakini hii mihimili ya utawala nchini ikae ikijua kwamba matendo yao ya kifisadi wanayoyafanya kwa wananchi kupelekea kukandamiza haki zao za msingi wazi wazi, yana mwisho mbaya kwa sababu huwa ndiyo chanzo cha kujenga chuki za kihasama katika matabaka ya kijamii.
Manufaa ya watu wachache kwa mirungula na kufanya ukiritimba wa upatikanaji wa haki, kunaifanya tasnia nzima ya sheria kuonekana wameoza, hawaaminiki na hawastahili kutegemewa!
Na siku raia wataposhindwa kuvitegemea vyombo vya haki na mihimili mingine ya Serikali kwa kutokuwa na imani navyo, raia hao watajilinda kwa sheria za mkononi mwao na hapo ndipo Serikali itakuwa imekwisha poteza sifa ya kuendelea kutawala mazima.
Sababu huwaga hakuna yeyote anayeweza kutuliza hasira na uasi wa umma(ref to Rwandan genocide 1994), chanzo chake ni chuki kama hizi zilizojengwa polepole katika matabaka ya kijamii kwa muda mrefu, Mungu ayaepushilie mbali.
Kama viongozi wote wakuu wa Serikali wameshindwa kuona uozo zilizotamalaki kila kona kwa sasa, basi tunaomba ajitokeze Kiongozi yeyote mwenye guts bila kujali ni wa chama ama dhehebu gani angalao aweze kutuliza hasira za watu kwa kukemea haya hadharani kwamba tunakokwenda siko, tutafute njia ya kutoka tulipokwama kama taifa.
M/Mungu hawezi kubariki taifa linalotweza haki za watu wake.