Video: Dada wa Bilionea Msuya aangua kilio Mahakamani baada ya Mke wa Msuya kuachiwa huru

Video: Dada wa Bilionea Msuya aangua kilio Mahakamani baada ya Mke wa Msuya kuachiwa huru

Kwa ambao tumekuwa tukifuatilia hii kesi from day one lazima tushtuke sana 😭😭😭Sasa nani alimuua Anathe jamani ?? Kwamba hao wameachiwa je muuaji kapatikana???
Ukweli wanaujua wao na Mungu anaona kama ni kweli ila damu ya mtu haipotei! Daah
Swali, maana umesema umeifuatilia hiyo kesi toka mwanzo:

Hakukuwa na ushahidi wowote wa DNA?

Maana kama mhanga alichinjwa, naamini aliupigania uhai wake kwa kadri alivyoweza, iwe kuwa kung’ata, kuparua kwa kucha, kuvuta nywele, na kadhalika.

Hakuna ushahidi wowote wa DNA ya mtu mwingine zaidi ya DNA yake yeye mhanga uliowasilishwa wakati kesi ikiendelea?

Kwa uzoefu wangu, kesi kama hizo huwa zinaacha trail ya forensic evidence ambayo hutumika kujenga kesi dhidi ya mtuhumiwa/ watuhumiwa.
 
ZIPO KESI AMBAZO HUKUMU ZAKE HUITAJI HEKIMA ZA MFANANO WA MFALME SOLOMON, HATA KAMA KAMA UNATAKA KUFANYA LIQUIDIFICATION, LAKINI UNATAZAMA PANDE ZOTE, KWA SABABU SHIDA ILIYO KUBWA HUWA NI "" MALI "" NA NDIYO HUWA CHANZO CHA UKATILI MKUBWA, UWIANO UTENGENEZWE, POSIBLY UPANDE WA DADA NA NDUGUZE WAKABAKI WEUPE PYE, HAPA NDIPO HEKIMA ITUMIKE, TUNAOA WAKE, LAKINI SOMETIMES HUJITAKIA VIFO SISI WENYEWE.
#To be noted!
 
Pesa ya Damu,Pesa alizoacha Msuya hazikuwa baraka bali zimegeuka laana.Yeye mwenyewe zilimuua,dada yake nae amechinjwa,familia yake(mke na watoto) ni kama watatengwa na ukoo sababu kila mmoja atavuta upande wake,watoto watamtetea mama na wazazi wanamaumivu ya Aneth.Hizi pesa za Msuya alizipata kwa haki?na je hakuwahi kudhulumu/kuua mwingine?kwa nini hizi pesa zimekuwa na mkosi kiasi hiki?Mwisho wa siku hakuna anayejua ,Hakimu wa kweli ni Mungu peke yake.
 
Masikini hanaga haki duniani,I sipo kuwa Mwenyezi Mungu amhurumie.Hii kesi imenifanya nikumbuke maneno ya Makonda ingawa tunamdharau ila yule kaka kuna muda anasemaga ukweli
 
Huku mtaani ingekuwa haki inatolewa, sijui kama watu wangepata haki zao. Watu wanahukumu kwa kufuata hisia, au kwa kutumia story za magazeti.
 
Uchawi haupo ni stori tu ambazo hata wazungu walikuwa nazo zama za middle age.

Kama uchawi ungekuwepo na una nguvu. Waafrica tusingeteseka kuomba viza za kwenda majuu, tungekuwa tunaenda marekani na Ungo na kuhamia huko
Kama unaamini hakuna uchawi, mambo ni sayansi mbona unalilia yanga icheze juani? Huamini sayansi ya mpira?
 
Swali, maana umesema umeifuatilia hiyo kesi toka mwanzo:

Hakukuwa na ushahidi wowote wa DNA?

Maana kama mhanga alichinjwa, naamini aliupigania uhai wake kwa kadri alivyoweza, iwe kuwa kung’ata, kuparua kwa kucha, kuvuta nywele, na kadhalika.

Hakuna ushahidi wowote wa DNA ya mtu mwingine zaidi ya DNA yake yeye mhanga uliowasilishwa wakati kesi ikiendelea?

Kwa uzoefu wangu, kesi kama hizo huwa zinaacha trail ya forensic evidence ambayo hutumika kujenga kesi dhidi ya mtuhumiwa/ watuhumiwa.
Kwenye court of public..ni feelings over facts
 
Back
Top Bottom