VIDEO: Hali ya Uwanja wa Mkapa ambao ulitarajiwa kutumika mechi ya Simba SC vs RS Berkane

VIDEO: Hali ya Uwanja wa Mkapa ambao ulitarajiwa kutumika mechi ya Simba SC vs RS Berkane

Sasa iweje achaguliwe?
Confirmed.
Screenshot_20250515_162743_Instagram.jpg
 
Kwahiyo mnataka kila mara muulizwe mnacheza uwanja gani wakati tayari mechi iliyopita mlishaonesha uwanja gani mnautumia kama mbadala wake.
Mechi ilirudishwa Mkapa stadium sasa kama hawaridhiki wawaambie watafute uwanja mwingine.
 
Mechi ilirudishwa Mkapa stadium sasa kama hawaridhiki wawaambie watafute uwanja mwingine.
Wanaangalia uwanja mbadala waliochagua kwenye mechi iliyopita. Ingekuwa hawakuwahi kuchagua uwanja mbadala basi wangeambiwa watafute uwanja. Kule kuna watu wanaakili zao timamu za kufikiria, sasa Tanzania kuna uwanja gani mwingine mbadala wa huo wa Mkapa ambao una hadhi ya ku host fainali ya CAFCC?
 
View attachment 3334676

Kama maelezo haya ni kweli basi Africa nzima ni corrupt aisee
Nadhani cha kujiuliza kwanza je ni kweli uwanja ni mbovu ? Kama kweli ni mbovu kwanini uwe mbovu ? Kwanini tuache loopholes za kuweza kutumiwa na wengine ?

Nadhani lawama hizi peleka kwa wahusika wa uwanja na nchi yako na sio wengine wanaotumia udhaifu wako.
 
Wanaangalia uwanja mbadala waliochagua kwenye mechi iliyopita. Ingekuwa hawakuwahi kuchagua uwanja mbadala basi wangeambiwa watafute uwanja. Kule kuna watu wanaakili zao timamu za kufikiria, sasa Tanzania kuna uwanja gani mwingine mbadala wa huo wa Mkapa ambao una hadhi ya ku host fainali ya CAFCC?
Ndio wangeulizwa wachague, hata akitumia uwanja huo huo utakao chezewa tar 17 ni sawa tu na sio kuamriwa!
 
Ndio wangeulizwa wachague, hata akitumia uwanja huo huo utakao chezewa tar 17 ni sawa tu na sio kuamriwa!
Mtu anachagua kama kuna options zaidi ya moja, sasa una mwambia mtu achague nini wakati hana options zaidi ya moja? Hivi unaelewa kweli unachoongea?

Nitajie viwanja vitatu vinavyoweza kutumiwa kwa fainali ukiachana na huo wa Mkapa ili ujione ulivyokosa hoja.
 
Hapa kuna namna nyingiii zinafanyika kumtoa simba mchezoni.
1.Taarifa imetoka siku moja kabla ya mchezo wa kwanza kufanyika.Hapa kuna namna.
2.Kwa mkapa imeonekana kuwa ni tishio sanaaa kwa timu mgeni.Hivyo simba asipatumie.
Simba ipambane game ipigwe kwa mkapa kwa namna yoyote ile.
Hizi ni hujuma za wazi
Sidhani kama itawezekana tena..Labda Watu wang'oe hata Viti au kuharibu pitch Amani Stadium ionekane haufai kwa game..
 
Magori aliwahi kuwa na akili lini? Kwani Zanzibar siyo Tanzania? Mngeambiwa Tanzania nzima hamna uwanja unsokidhi vigezo mchaguwe nchi nyingine ingekuwaje?
Zanzibar siyo Tanzania ila ni Nchi mojawapo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Use your PhD responsibility. Usituchanganye
 
Tazama hali ya sasa Uwanja wa Mkapa ambao ulitarajiwa kutumika katika mechi ya Kombe la Shirikisho Simba SC vs RS Berkane

Kuufungia uwanja wa Taifa, CAF wana hoja, tuache kutumia hisia kwa vitu vinavyohitaji weledi, huu uwanja hauna mifumo mizuri ya utoaji maji iwapo mvua ikinyesha, na hii ni fainali inayotazamwa karibia dunia nzima, inaweza leta taswira mbaya kwa mpira wetu wa Afrika,

Ni wakati sasa viongozi wetu wanaosimamia michezo wajifunze na waache kufanya mambo kisanii na kisiasa, watu wenye weledi na viwanja wasimamie na siyo wanasiasa
 
Juzi juzi MwanaFA alinukuliwa akisema sababu ya mechi ya nusu fainali ya Simba vs Stellenbosch kupelekwa Zanzibar ilitokana na ombi la serikali ya Zanzibar kuomba mechi ipelekwe kule eti ili kudumisha muungano.

Kwa nini hamfikiri hata hili la fainali linatokana na ombi kama hilo?
 
Back
Top Bottom