VIDEO; Hii sio sawa kabisa, mnaachaje kumsaidia mwenzenu ili tu muendelee kuswali?

VIDEO; Hii sio sawa kabisa, mnaachaje kumsaidia mwenzenu ili tu muendelee kuswali?

Huyo jamaa inavyoonekana amepata changamoto ya kiafya na Kuna matatizo mengine ya kiafya unatakiwa u respond haraka ukichelewa unampoteza mtu

Hao wanaoswali hapo walitakiwa kusitisha hizo taratibu za ibada na kumsaidia jamaa maana msaada wa haraka Kwa huyo jamaa ni sehemu ya ibada pia Tena kubwa tu kiufupi wamezingua wanaswali ila hawajui kwann wanaswali ni kama vile wanaenda msikitini kukamilisha taratibu za ibada tu.
 
we kwa akili yako hapo kuna mtu ana ubongo hapo? Wote wamejaza vinyesi kichwani, labda hao watoto ndio wanaweza kuokolewa
 
Unaonesha kujali. Ni vizuri sana. Lakini Je, unao utaalam au ufahamu juu ya masuala ya kiafya?

Pole.
Kumsaidia mtu hadi uwe na utaalamu wa masuala ya afya?

Kwamba kumpa mtu huduma ya kwanza napo lazima uwe mtaalam wa afya?

Kumkimbiza na kumuwahisha hospitali ili kuokoa uhai napo panahitaji utaalamu wa afya?
 
Kumsaidia mtu hadi uwe na utaalamu wa masuala ya afya?
Ndiyo. Sio kila tukio linalohusu uhai/afya ya mtu ni la kukurupukia. Unaweza kuwa na nia njema lakini kitendo chako hicho ukajikuta ndo unammalizia
Kwamba kumpa mtu huduma ya kwanza napo lazima uwe mtaalam wa afya?
Ndiyo. Huduma ya kwanza inatolewa kwa Utaratibu fulani na mtu mwenye walau ufahamu wa katika tukio hilo ni nini kifanyike ili kuokoa maisha ya muathirika.
Kumkimbiza na kumuwahisha hospitali ili kuokoa uhai napo panahitaji utaalamu wa afya?
Hapana. Sio lazima bali Hilo linaweza kutolewa na yeyote mwenye chombo cha Usafiri na watu wengi (madereva)wanalifahamu hilo na muathirika inatakiwa awekwe kivipi katika chombo kitakachomsafirisha na pia mwendesha chombo awe na tahadhari zipi wakati wa kumsafirisha mgonjwa. Ni lazima kuzingatia Usalama wa mgonjwa ili afike akiwa hai Hospitali.
 
Uislam sio ukiristo au dini nyengine kama swala yao ni kuimba kuimba , Unapofunga swala na kuanza kuswali hakuna kitu kitachokukatisha, labda kujamba tu yaani kutenguka udhu
Dah, kujamba ni sawa wakati wa swala ila siyo kutoa msaada mtu akihitaji!
 
Ww sio muislam huna elimu yeyote kuhusu muislam na Sheria zake katika swala.
Muislam unsongozwa kwa Sheria na si kwa mihemko.
Katika Sheria za swala hakuna kitu chochote kinacho weza kukatisha swala bali mtu utenguke udhu hapo ndo utaruhusiwa kukatiza swala ili ujisafishe ili urudi kusali upya.
Inapo tokea changamoto kama ya hiyo video ni mpaka swala imalizike ndo mambo engine yafuate na bahati nzuri swala ya waislam huwa haizidi hata dakika 5.
 
Nyie mna dini yenu na wao wana yao milio ya kazi gani sasa
 
Back
Top Bottom