VIDEO: Huko Mauritania bado kuna biashara ya kichini chini ya kuuza watumwa

Mada mezani ni utumwa mauritania tuweke masuala ya biblia pembeni
MPUMBAVU HANA BREAK

MWENYE KOSA HAKOSI KUSEMA MBONA HIVI, MBONA YULE..

kwa hio usishangae hao wakuda mkuu kuleta kuanzsha udini katika ukweli😂😂
 
Kunahaja ya kukaa chini na kupitia mikataba ya kimataifa ya haki za binadamu, Kila siku tunasikia report za utumwa duniani kote, imefika hatua hata kumyanyasa binti wa kazi linaonekana ni jambo la kawaida, hii si sawa na hatari kwa afya ya Ulimwengu...
 
Ukiwaambia wanajawa povu na kusema unawapondea kidini. Hawa jamaa waarabu hawajawahi kumtazama mwafrika kama mwenzao. Nenda kwa wazungu utaoa binti zao na watakurithisha mali zao na hata kukuweka katika biashara zao kama mwanafamilia.

Nenda kwa wachina mtafanya biashara na mtagawana faida bila shida. Ila muarabu anataka akae kiti kirefu wewe kifupi ili akuongeleshe juu ya utosi.

Waarabu ukioa binti yule wa kiarabu pure ni labda umtoroshe na ukijaribu familia yake watawatafuta hata miaka 100. Kwa sheria zao za kiarabu wanatakiwa kumuua huyo binti (honor killing).

Ila wavaa kobazi wakiwaona sasa hawa watu dah hadi wanadinda kwa namna wanawatukuza na kuwalamba nyayo zao wakiamini ni binamu zao.
 
Kwa hiyo wewe umeangalia kwenye hiyo angle ya kuoana tu? Ushenzi wa wazungu ni mwingi mara elfu ya waarabu. Wazungu ni chanzo cha maovu mengi.
 
Rekebisha hapo mkuu,
Mtumwa ni halali kwa wayahudi sio wakristo.
Ukristo unasimamiwa na injili
 
hata lile dini lao ni la kuwaachia, hawana utu viumbe hao
 
Kwa hiyo wewe umeangalia kwenye hiyo angle ya kuoana tu? Ushenzi wa wazungu ni mwingi mara elfu ya waarabu. Wazungu ni chanzo cha maovu mengi.
Topic ni inchi ya Mauritania ambayo ni ya kiarabu kuruhusu hiyo kitu na hata ukienda Saudi Arabia,Iraq,Libya ambazo ni watu wa jamii moja habari ni ile ile.

Mimi sitetea wazungu but naongelea swala la kistaarabika na kuchangamana na jamii nyingine wapo vema. Ndio maana huko Ulaya na marekani waarabu,waafrika,wachina wamejaa tele na wanaishi kwa uhuru na kuoa au kuzaa na wanaetaka.

Nenda wewe tu hapo kwa mfano hapo Libya halafu uteletee ripoti ya uchangamano. Kwasababu wanakutazama kama mtumwa kwao na ni takataka.

Watu wengi sana weusi wameoa wazungu na wachina na wanaishi nao kawaida. Ila ni nadra sana kukutana na couple ya mwafrika na muarabu pure tena yule anaeishi uarabuni au muhindi pure ameoana na mwafrika pure.

Wazungu wabaguzi wapo ila wana aibu sana siku hizi sababu ya mabadiliko ya sheria za usawa na kutambua haki za kibinadamu na kupiga vita ubaguzi wa rangi.

South Africa hapo tu ni mfano, ubaguzi ulikuwa mkali ila sasa makaburu wamekuwa wapole wanaridhia watoto wao wa kizungu kuolewa na waafrika.

Sasa wewe unataka kubadili mjadala hapa ionekane mimi nataka ligi za kitoto wakati tunazungumza mambo serious yanayotokea katika jamii. Mimi sio wakili wa wazungu kuwa nawatetea kwani hayo mataifa ya magharibi si kila siku ninawaponda hapa kuhusu ushoga, na mambo mengine ya hovyo ?

Sasa wewe unaanzisha sijui mjadala gani hapa.
 
Naona wadau wameamua kukabia juu kwa juu kabla ya comments za "oooh kobazi" "oooh waarabu". Kumbe bible inaruhusu bhana tuendelee kukata vidali wanangu humu tuuuu
 
Hapa Duniani hakuna jamii ilostaraabika sema tunapishana vipaumbele katika uovu


Nawasilisha
 
Agano la kale ni kabla ya Ukristo.
Wakristo ni wafuasi wa kristo,
Kristo anqpatikana kwenye Agano jipya
Hawa mbuzi hawajui chochote kuhusu biblia 😂🤣

Wanabwaja bwaja kwa kutafuta uthibitisho feki ili uendane na utapeli wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…