The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 4,249
- 11,592
View: https://www.youtube.com/live/vLdO-z31bOY?si=DxKCHlFGEDmG6wWD
In brief:
➡NO REFORMS, NO ELECTION is there na CHADEMA is a proper channel to carry it forward...
➡Katika chaguzi za 2015 kurudi nyuma tuliweza kugombea na kushinda kwa sababu ingalau kulikuwa na competition japo mazingira yalikuwa very hostile....
➡Ili ushinde ilikuwa lazima ugangamale kwelikweli. Mfano, John Heche huko Tarime ktk uchaguzi wa mwaka 2010 na 2015 ili atangazwe watu walilazimika kubeba madumu ya petrol na kutishia kuteketeza majengo ya Halmashauri ya wilaya Tarime kama DED msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tarime asingetangaza mshindi halali...
➡Aidha, Ili John Mnyika atangazwe mwaka 2010 ktk jimbo la Ubungo walilazimika kumteka mkurugenzi wa uchaguzi ndugu Kiravu ndani ya ofisi na kumwambia usipotangaza mshindi halali tutafia wote humu ndani...!
Hoja ya CHADEMA kuwa itakufa iwapo itazuia na hivyo kutoshiriki uchaguzi kwa sababu itakosa ruzuku na wabunge na madiwani. Tundu Lissu anajibuje hoja hii..?
➡Anaanza kwa kumkatiza mhojaji na kusema, wenye hoja hii ni aidha hawana ufahamu au hawajui kabisa historia ya kupambania demokrasia Tanzania na Afrika kwa ujumla..
➡Anatolea mfano wa ANC ya South Africa chini ya wapigania mageuzi na uhuru kina Nelson Mandela wakati huo. Kwamba ANC sio tu haikushiriki chaguzi fulani fulani bali ANC ilipigwa marufuku (banned) kabisa kujihusisha na siasa na hata neno "ANC" kutamkwa tu kwenye vinywa vya watu ilikuwa ni marufuku. Anawauliza swali wanaotaka kushiriki kwenye chaguzi za kilaghai, kuwa, Je ANC ilikufa...?
##Fuatilia interview hii hadi mwisho ujifunze kitu kutoka kwa gwiji huyu wa siasa na harakati za binadamu na ukombozi..