Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

Zanzibar 2020 VIDEO - KAMPENI ZANZIBAR: Tundu Lissu awapa somo muhimu Wazanzibar na Watanganyika juu ya Muungano. Je, Magufuli - CCM anaijua historia hii kweli?

Huyu kweli anastahili kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Kwa kauli hizi, si ni wazi ameonesha kuwa atavunja Muungano?
Kwani huo ni muungano au ukoloni tu! Hebu niambie serikali 3 zinakupunguzia nini wewe Kama wewe!
 
Niseme wazi mimi ni mmoja ambaye Historia sekondari nikioata D na hadi Leo huwa nalalamika kuwa baraza la mitihani lilinipendelea ilitakiwa wanipe F Historia mimi siipendi ni somo la kuongelea marehemu...
Kwani nini maana ya historia?
 
Kaingia mitini

Mshana afadhali umekuja.

Achana na rasimu ya Warioba, ningependa uniambie, Lissu amezungumza sawasawa Kama kiongozi tena anayejiandaa kiwa mkuu wa nchi?

Aliposema wazanzibar wa Upinzani, nadhani alimaanisha akina Maalim Seif wamekuwa akishinda tabgu 1995, je ni sahihi kisheria? Hii nikimaanisha kuwa akitakiwa kuthibitisha, atawezana?

Aliposema kuwa Karume alilazimishwa kusaini makubaliano ya Muungano kuwa kwamba yeye alokataa. Ni kweli? Anaweza atathibitisha Hilo?

Tuanzie hapo?
 
..muungano ni tatizo la KISIASA.

..CCM-Znz wamekuwa wakitumia vyombo vya dola toka Tanganyika kuwakandamiza waZanzibari wenzao.

..sisi wa-Tanganyika kama tunataka kuulinda muungano ni lazima tuhakikishe HAKI inatenda Zanzibar.

..maingiliano ya kiuchumi, kiulinzi, kibiashara, na kifamilia, yanaweza kudumishwa bila ya Watanganyika kujihusisha na dhambi ya kuunga mkono upande mmoja wa waZnz kudhulumu haki za kisiasa za upande mwingine.
Ni sawa
 
Tuliona hili nikaandika huu uzi

CCM versus Opposition: Political Lessons to Learn
Kwanini mlishangilia wakati vyama vya siasa vya upinzani vinabakwa huku mnaimba eti kazi tu. Sasa ndio mnapata akili wakati akina Polepole wanatembeza unafiki kwa mwenyekiti wenu mlikuwa jandoni? Mnaambiwa hapa kazi tu mnakenua mimeno. Kuleni hapa kazi tu kimya kimya....
 
Mshana afadhali umekuja.

Achana na rasimu ya Warioba, ningependa uniambie, Lissu amezungumza sawasawa Kama kiongozi tena anayejiandaa kiwa mkuu wa nchi?

Aliposema wazanzibar wa Upinzani, nadhani alimaanisha akina Maalim Seif wamekuwa akishinda tabgu 1995, je ni sahihi kisheria? Hii nikimaanisha kuwa akitakiwa kuthibitisha, atawezana?

Aliposema kuwa Karume alilazimishwa kusaini makubaliano ya Muungano kuwa kwamba yeye alokataa. Ni kweli? Anaweza atathibitisha Hilo?

Tuanzie hapo?

..hataweza ku-prove kwasababu vyombo vya dola na mahakama ni za ccm.

..hata mauaji yaliyotokea mgodini Bulyankhulu miaka ya 90 alishindwa ku-prove kwasababu vyombo vya dola/uchunguzi vilikuwa upande wa serikali na siyo upande wa wahanga ambao TL alikuwa anawatetea.

..ccm mnapozidiwa ktk majukwaa ya kisiasa mnakimbilia kwa Polisi wenu, waendesha mashtaka wenu, na mahakama zenu.
 
Mimi sio mwanasheria "Ni yeye" ni mwanasheria nguli. Anajua kuwa Kati ya mambo ambayo ni very sensitive ni pamoja na suala la Muungano.

Hivi akiambiwa athibitishe kuwa "Hayati Karume alilazimishwa kusaini hati ya Muungano, atathibitisha"?.
Mahakama ziko wazi, tangulia na hoja zako, udhibitisho upo wa kumwaga¡
 
Hoja yangu ni moja tuu, Tundu Antipas Lissu athibitishe kauli yake kuwa Hayati Karume alilazimishwa kusaini makubaliano ya Muungano

..wewe una uthibitisho gani kwamba Hayati Karume alisaini bila kushinikizwa?
 
Ukiangalia video yote jamaa kaongea vyema na katoa hamasa nzuri sana ingawa kwenye habar ya muungano sijaona akil yoyote kubwa iliyotumika.Kaongea vitu vya kawaida kabisaaa ambavyo vinafahamika na majority though ni vya kwel ila viko obvious kabisa kabisa.Vinajulikana.
 
B
Ila Mungu fundi sana, hivi Magufuli, angepewa hata robo ya akili ya Lissu, na vile anapenda ajue kidhungu, na kutoa takwimu za kilomita za bara bara tungekoma.

Anachojua kwenye historia ya Tanzania ni Chato. Na maeneo mengingine yenye majina ya kiuasharati tu. Eneo la katerero na mto wake wa maji.

Kumuuliza historia ya Muungano Magufuli ni kumuonea bure.

Miaka 5 inatosha akapunzike, acheni kumsukumia huko.
Endeleeni kujifariji 😂. Baada ya uchaguzi, humu ndani patapoa kweli.
 
Back
Top Bottom