Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda amependekeza kufanyike mdahalo wa wazi kati yake na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ili Watanzania wachague ikiwa wataendelea na maandamano au kuchagua maridhiano.
Your browser is not able to display this video.
========================= For English Audience
Secretary of Publicity and Ideology of CCM Paul Makonda, has proposed an open debate between him and the leaders CHADEMA so that Tanzanians can choose whether to continue with protests or opt for reconciliation.
Ina maana Makonda hajui kwamba maridhiano yalishakufa, ndio maana yeye akawekwa hapo ili kumrahisishia njia yule aliyemweka aliyeshindwa kufanya kulingana na maridhiano?
Samia ndie anayetakiwa kuitisha mdahalo na viongozi wa Chadema, sio Makonda, yeye amepewa cheo juzi tu, hajui A wala B kuhusu maridhiano.
Sioni mtu wa kuandamana,watanzania sio wajinga ambao wanaweza pelekwa na vibaraka wa wazungu ili kuvuruga amani na mstakabali wa taifa letu.Mwenyeki wangu makonda huhitaji kuwa na hofu juu ya hawa watu .
Wewe Makonda unaweza kujibu hoja za Lissu kwa kipi? Kipindi kile alipowachachafya mpaka akapata madhila kwanini hukuita mdahalo?
Too late, hakuna mwenye muda wa kupoteza kufanya mdahalo na wewe.
Na uwezo huo huna!
Makonda aache kulazimisha sifa! Uwezo wa kufanya mdahalo wa aina yoyote ile na mtu kama Tundu Lissu, John Mnyika, nk. hana!
Asisahau kichwa kimoja cha Tundu Lissu ni sawa na vichwa laki 1 vya makada wa ccm vikiunganishwa kwa pamoja! Na akumbuke huyo Tundu Lissu hajatumia jina la mtu mwingine kama alivyofanya yeye Bashite, kufika hapo alipo.