Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Si ajabu Magufuli akamteua Bulembo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar baada ya Bashite sababu ya huu mchango wake wa wito wa kutaka Zito auawe
 
Bunge linajadili kumuua Zitto Kabwe kwa sababu ameisema vibaya serikali nje ya nchi na wabunge wanashangilia. Yani kweli kama taifa tumefikia hatua hii? Kufikiria kumuua mtu, na kujadili hadharani bila woga? Na Spika wa bunge yupo, anasikia na hakemei? Mnajadili kuua kwani nyie mtaishi milele?

Nimesikitika kuona hata Mchungaji Lwakatare ambaye alipaswa kukemea UPUMBAVU huu nae anashangilia. Tena wanasema auawe hukohuko asirudi akiwa hai. Yani irudi maiti yake. Hili ndio bunge la Job Ndugai, linalojadili kuua watu, badala ya kujadili ustawi wa watu. Halafu likiitwa bunge dhaifu Ndugai anafura. Marekani wakisema tunakiuka haki za binadamu, tunajificha kwenye kivuli cha ushoga?

Hivi uliwahi kuona wapi duniani popote bunge likijadili kuua watu wake? Kama wanaweza kujadili hadharani kuua, wakiwa peke yao kwenye vikao wanafanyaje? Unajadili kumuua mbunge, ndani ya bunge na wabunge wanashangilia?? Aibu, aibu, aibu.!!
 
Pamoja na haya yote yanayoendelea ya uminyaji wa demokrasia bado mmejipanga kushiriki uchaguzi.

Upinzani mmepoteza dira na hamjui mnataka nini.
Zitto amejitahidi na kufanikiwa kuwanyima watoto kilichokuwa kiwasaidie kutoka eneo moja kwenda lingine, bila aibu anataka kwenda kuomba kura kwa wazazi wao...only in Tz!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…