Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Si ajabu Magufuli akamteua Bulembo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar baada ya Bashite sababu ya huu mchango wake wa wito wa kutaka Zito auawe
 
Bunge linajadili kumuua Zitto Kabwe kwa sababu ameisema vibaya serikali nje ya nchi na wabunge wanashangilia. Yani kweli kama taifa tumefikia hatua hii? Kufikiria kumuua mtu, na kujadili hadharani bila woga? Na Spika wa bunge yupo, anasikia na hakemei? Mnajadili kuua kwani nyie mtaishi milele?

Nimesikitika kuona hata Mchungaji Lwakatare ambaye alipaswa kukemea UPUMBAVU huu nae anashangilia. Tena wanasema auawe hukohuko asirudi akiwa hai. Yani irudi maiti yake. Hili ndio bunge la Job Ndugai, linalojadili kuua watu, badala ya kujadili ustawi wa watu. Halafu likiitwa bunge dhaifu Ndugai anafura. Marekani wakisema tunakiuka haki za binadamu, tunajificha kwenye kivuli cha ushoga?

Hivi uliwahi kuona wapi duniani popote bunge likijadili kuua watu wake? Kama wanaweza kujadili hadharani kuua, wakiwa peke yao kwenye vikao wanafanyaje? Unajadili kumuua mbunge, ndani ya bunge na wabunge wanashangilia?? Aibu, aibu, aibu.!!
 
Kwa kweli inabidi kama kuna wauaji wachangiwe tu pesa na hawa wabunge wa CCM maana kujenga hoja hawawezi tena. Zitto kaandika barua katoa hoja zimeeleweka na World Bank na nyie jibuni basi mpangue hoja zake, mnashindwa nini? Mnakimbilia kuua ua tu kama mlivyotaka kumfanya Lissu

So pathetic mnadhani ni Zitto peke yake, kulikuwa na pettition online ya hilo suala na World Bank walikuwa tagged. Ili kuwa na sigantures zaidi ya 10,000 mimi mwenyewe niliandika emails, world bank ilikuwa flooded na emails zikilalamika udikteta wa awamu ya tano.

Endeleeni kulala tu maana mmejaza vilaza kwenye hilo chama chakavu.

Mwisho HONGERA sana mama mchungaji nimeona unakenuaaaaa uliposikia WITO WA ZITTO KABWE KUUULIWA no wonder wanasemaga ulizika makondoo hai kwenye geti la St. Mary's school na kanisani kwako FULL MAKAFARA ya damu.

View attachment 1344066
Pamoja na haya yote yanayoendelea ya uminyaji wa demokrasia bado mmejipanga kushiriki uchaguzi.

Upinzani mmepoteza dira na hamjui mnataka nini.
Zitto amejitahidi na kufanikiwa kuwanyima watoto kilichokuwa kiwasaidie kutoka eneo moja kwenda lingine, bila aibu anataka kwenda kuomba kura kwa wazazi wao...only in Tz!
 
Back
Top Bottom