Mzee Mkapa, Mangula,Kikwete na wengineo mko wapi? Haya ndiyo mliyotuachia? Amani, umoja, uvumilivu na mshikamano wa kitaifa mliohubiri na kutuasa tusijaribu kuvichafua mbona vinavhafuliwa na Hawa ccm wenu?
Toeni tamko juu ya kauli hizi kwani mwanzo wa Moto ni cheche! Tafadhalini Sana ccm msiige ya majirani zetu na mistake kuja kusuluhishwa na Marais wastaafu kwa ujinga wa Hawa wachache! Wakemeeni na ikibidi washtakiwe kwa uchochezi kwani akiuawa kweli na wafuasi wake wakataka kulipiza kisasi tutaishia pabaya!
Haya siyo ya kuyakalia kimya hata kidogo kwani hata Kama ndivyo wanausalama hufanya kimya na kwa Siri hawajinadi hadharani!
Vyombo vya usalama timizeni wajibu wenu na pia viongozi wa dini kemeeni matamko haya ya uvccm na wabunge wao!
Hilo halikubaliki hata kidogo kwa jamii ya kistaarabu!