Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Vijana wapumbavu tu wanatafuta kujikomba. Ni wa kupuuza tu.
 
Kijana anawaomba wasomi wa chuo kikuuu na wamsikilize ujinga anaotapika...hivi elimu inafanya nini kichwani mwa hawa vijana..eti nchi hii kumetokea genge linalotamka hadharani kutoa uhai wa mtu mwingine...Nani kawambia nchi hii ni yenu peke yenu? Kama mtu amekosea si mwende mahakamani...kwanni msemo kuua umekua kama chakula siku hizi?vijana mnatuangusha sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mkapa, Mangula,Kikwete na wengineo mko wapi? Haya ndiyo mliyotuachia? Amani, umoja, uvumilivu na mshikamano wa kitaifa mliohubiri na kutuasa tusijaribu kuvichafua mbona vinavhafuliwa na Hawa ccm wenu?
Toeni tamko juu ya kauli hizi kwani mwanzo wa Moto ni cheche! Tafadhalini Sana ccm msiige ya majirani zetu na mistake kuja kusuluhishwa na Marais wastaafu kwa ujinga wa Hawa wachache! Wakemeeni na ikibidi washtakiwe kwa uchochezi kwani akiuawa kweli na wafuasi wake wakataka kulipiza kisasi tutaishia pabaya!
Haya siyo ya kuyakalia kimya hata kidogo kwani hata Kama ndivyo wanausalama hufanya kimya na kwa Siri hawajinadi hadharani!
Vyombo vya usalama timizeni wajibu wenu na pia viongozi wa dini kemeeni matamko haya ya uvccm na wabunge wao!
Hilo halikubaliki hata kidogo kwa jamii ya kistaarabu!
 
Hii inaweza kuwa mbinu... Yaan wamepanikishwa afu wamepanic wanaanza kuropoka ukweli... Then watu wanachukua kama ushahidi halafu wanawapiga tofali...

Mdomo hauna ushuru, chunga ulimi usilete mgogoro
 
Back
Top Bottom