Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

Video: Mchungaji Mama Rwakatare akishangilia wito wa kuuawa “msaliti Zitto” uliotolewa na Bulembo

View attachment 1346062
HONGERA sana mama mchungaji nimeona unakenuaaaaa uliposikia WITO WA ZITTO KABWE KUUULIWA no wonder wanasemaga ulizika makondoo hai kwenye geti la St. Mary's School na kanisani kwako FULL MAKAFARA ya damu.

View attachment 1344066
Nimeusikiliza huu mjadala, kiukweli baadhi ya wabunge wametoa kauli kali na hatarishi, ikiwemo kauli ya kifo kwa Mhe. Zitto Kabwe, ni ajabu kwa Mbunge Mlokole, Mchungaji Rwakatare, kushangilia mtu auawawe!.

Naendelea kusisitiza kuhusu kauli huumba, kauli kama hii ilitolewa kumhusu Lissu na mara ikatekelezwa, sasa ni kumhusu Zitto, bahati nzuri Zitto ni mtu wa Kigoma, mwisho wa reli, na kule kwao, kaaga!, likimtokea la kutokea, kama sio mpango wa Mungu, kwa mujibu wa Zitto mwenyewe, hawa waliochangia adhuriwe, kule majumbani kwao, hakutasalia hata panya alive!.

https://www.jamiiforums.com/threads...ui-nguvu-zako-chunga-sana-kauli-zako.1666370/
P
 
Nimeusikiliza huu mjadala, kiukweli baadhi ya wabunge wametoa kauli kali na hatarishi, ikiwemo kauli ya kifo kwa Mhe. Zitto Kabwe, ni ajabu kwa Mbunge Mlokole, Mchungaji Rwakatare, kushangilia mtu auawawe!.

Naendelea kusisitiza kuhusu kauli huumba, kauli kama hii ilitolewa kumhusu Lissu na mara ikatekelezwa, sasa ni kumhusu Zitto, bahati nzuri Zitto ni mtu wa Kigoma, mwisho wa reli, na kule kwao, kaaga!, likimtokea la kutokea, kwa mujibu wa Zitto mwenyewe, hawa waliochangia adhuriwe, kule majumbani kwao, hakuta salia hata panya alive!.

P
Zitto mara nyingine ana mikwara sana,alimpiga mmoja Musiba mpaka leo hatujapata mrejesho.
 
Kweli Ukiwa Msafi usiingie kwenye siasa utachafuliwa mpaka kwenye chupi!
 
Nimeusikiliza huu mjadala, kiukweli baadhi ya wabunge wametoa kauli kali na hatarishi, ikiwemo kauli ya kifo kwa Mhe. Zitto Kabwe, ni ajabu kwa Mbunge Mlokole, Mchungaji Rwakatare, kushangilia mtu auawawe!.

Naendelea kusisitiza kuhusu kauli huumba, kauli kama hii ilitolewa kumhusu Lissu na mara ikatekelezwa, sasa ni kumhusu Zitto, bahati nzuri Zitto ni mtu wa Kigoma, mwisho wa reli, na kule kwao, kaaga!, likimtokea la kutokea, kwa mujibu wa Zitto mwenyewe, hawa waliochangia adhuriwe, kule majumbani kwao, hakuta salia hata panya alive!.

Kama kawaida Paskali katika ubora wake.

Paskali ni kama mdomo wa Ng'ombe kwanzi huwezi kujua yupo kushoto au kulia.

Karibu tena uwatetee wanyonge.
 
Ndio maana inasemwa kuwa huyu mama sio mchungaji kabisa! Ongea yake, tembea yake na matendo yake ni laghai mkubwa!
 
Pascal Mayalla,
Pascal huu uzi niliusoma,nilipoona video clip ina sec 16,nikaingiwa na mashaka.Nikataka kumwomba mleta mada alete video nzima,namshukuru Mungu jana nimeona video kwa sehemu kubwa.Sasa wewe mwenzangu sijui umeiona video ile ya huo mjadala yenye dakika zaidi ya 20?au umeonahii ya sec 16?

Swali langu la msingi kwako ni mbunge yupi alitoa kauli ya kifo kwa Zitto?Wabunge waliongea na mwishoni walitoa mapendekezo,mimi hakuna niliyemsikia anapendekeza Zitto auawe.Nitafungua uzi leo kuonyesha ambavyo watu wanapotosha mambo katika hili suala.kama mnalazimisha mfano wa kuwa vitani kagera kwamba mtu akisaliti auawe,kama mnautumia huo mtakuwa mmekosea.

Huyo aliyetoa mfano wa vitani(Mheshimiwa Bulembo) ,msaliti auawe,kuna kitu alipendekeza mwishoni,namnukuu "Huyu mtu kazoea anatakiwa apate kiboko kizuri sana".Ukiipata video aliongea muda dakika ya 13:44-14:45.
Mleta mada amechukua kaeneo tu ka sekunde 16,ambazo ni chache ukilinganisha na dakika 3 ambazo speaker alitoa kwa wachangiaji.Tuache ushabiki,tuyachunguze mambo.

Nitaijibu hii thread leo nikijariwa ,imepotosha.Hata speaker alivyomalizia hili jambo alilikabidhi kwa ofisi ya mwanasheria mkuu.Hakumalizia kwa kusema Zitto auawe.Huyo aliyesema "Zitto auawe ni nani?na kwenye video aliongea muda upi au kuna video hatujaiona walisemahivyo?
NB:love distort judgement
 
Aqua,
Mkuu, Aqua, hoja yangu kuhusu kauli huumba bado inasimama!, mtu unaweza ukatamka maneno 100, lakini kati ya hayo, ni neno moja tuu ndio likawa powerful with power vibrations, hivyo haijalishi alianza kwa kusema nini na kumaliza kwa kusema nini, as long as alitamka msaliti vitani huuwawa kabla ya kurejea, na kusema Zitto ni msaliti, bila hata kusema Zitto auliwe, tayari alionyesha ana wish Zitto afanywe nini na jirani yake mtu wa Mungu, akapiga makofi kushangilia.

Jee ulibahatika kumsikia mtu huyu alisema nini hapa, na aliyesemwa unamjua ni nani?,

Find out nini kilimkuta huyo aliyesemwa hapo na kilimkuta baada ya siku ngapi?.
P
 
Pascal Mayalla,
Mimi nataka nibaki kwanza kwenye hoja ya wabunge kutaka Zitto auwawe,kama inavyoenezwa mitandaoni na kuweka vikatuni. Nakubali kwamba maneno huumba sikatai,katika communication skills wanasema "You should not worry about what you say worry about how people are going to interpret what you say".Sasa tusifanye tafasiri ya jinsi tunavyotaka sisi iwe ndivyo alivyokusudia msemaji.Umeiona hiyo video yenye dakika 28:54?Mleta mada ana hidden agenda.
 
Video kamili ya hili suala ipo hapa naomba tuiangalie hii video bila kuwa na upendeleo.Mbunge aliyetoa mfano wa msaliti vitani ni Mheshimiwa Bulembo aliongea muda wa dakika ya 13:44-14:56 (1min 12sec).Ukimsikiliza hapo utagundua amesema "mkiwa vitani pale kagera Tanzania inapigana na Uganda,akitoka mtu mmoja akapeleka habari zetu,hatakiwi kuvuka kurudi anatakiwa auwawe kulekule".

Mheshimiwa amesema mkiwa Kagera mnapigana na Uganda.Sasa huu ulikuwa ni mfano,sasa kwa nini watu wanang'ang'ania mfano kwamba ndicho kilichokusudiwa kifanyike?Na utaona mfano huu aliutoa kama utangulizi,ndiyo maana baada ya kumaliza mfano huo akasisitiza "usaliti".

Nakubali wabunge wengi wamesema Zitto amesaliti lakini je walipendekeza auawe?Angalia video hiyo natoa summary ya kila alicyechangia na alichpendekeza mwishoni.Mimi binafsi sijamsikia mbuge yeyote akisema Zitto auawe,kwa hiyo mnaosambaza taarifa kwamba wabunge wataka Zitto auawe hamko sahihi na mnaposema mama Rwakatale kashangilia kuuawa kwa Zitto bado ni uongo juu ya uongo,huyo mama alipiga meza kussupport msaliti vitani auawe.
Summary

1.Bulembo 13:44-14:56 (1min 12sec)

"Huyu mtu kazoea anatakiwa apate kiboko kizuri sana"

2.Mhesh: Kessy: huyu ni mtu hatari,unaenda kusaliti nchi nchi za nje unafaa?hufai hata kidogo (time 13:15-13:42)


3.Mhe:Janeth Mbene ;"Zitto amepotosha kwa makusudi kwa ajenda yake binafsi ya kuleta fujo nchini kwetu"(muda 15:03-17:28)

4.Mhesh.Mary Chatanda :muda 17:30-18:13

"Ametusaliti kutumia nembo ya Bunge kinyume na sharia,"

ni vizuri akapatiwa adhabu anayostahili ( 18:08-18:13)

5.Mhesh.Stanslaus Mabula: Amepotosha(19:45-20:17),”Bunge lako kama lina namna ya kuchukua hatua ni lazima tufanye kazi ya kuijenga nchi na siyo kuibomoa”

6.Mhesh:Juma Nkamia:muda 20:20-22:58

"Tufike hatua watu wa namna hii wanayoiyumbisha nchi wachukuliwe hatua(muda 22:50-22:58)"

7.Mhesh Dr.Godwin Moleli: kwa kufuata taratibu za Bunge,kwa kufuata kanuni za nchi na sheria za nchi ninakuomba hili jambo liende kwenye mfumo ambao utatuletea watu wa aina hiyo ambao wanasaliti taifa hili wanatakiwa kufanywa nini,na isiishie hapo……..”(muda 23:50- 24:15)

Hata speaker wa Bunge alivyomalizia lilipeleka kwa mwana sheria mkuu wa serikali aliangalie.Kwa hiyo mimi binafsi sijaona popote ambapo kuna mbuge ameshauri Zitto auawe.Ushauri:Tuwe makini,matatizo au mafanikio ya mwanadamu huanza kama wazo na baadaye hutekelezwa katika mwili.Tusitumie nafasi zet vibaya au influence tuliyo nayo kwenye jamii vibaya.

peaker alitoa dakika 3 kwa kila mtu,video hii ina sec 16 tu, 3min=3x60=180sec

Je 16sec ni asilimia ngapi ya muda wote=16/180=0.0889=8.89% asilimia zaidi ya 90 ya maongezi ya Mhesh.Bulembo haijawekwa kwenye hii clip chochezi.
 
Mimi nataka nibaki kwanza kwenye hoja ya wabunge kutaka Zitto auwawe,kama inavyoenezwa mitandaoni na kuweka vikatuni.Nakubali kwamba maneno huumba sikatai,katika communication skills wanasema "You should not worry about what you say worry about how people are going to interpret what you say".Sasa tusifanye tafasiri ya jinsi tunavyotaka sisi iwe ndivyo alivyokusudia msemaji.Umeiona hiyo video yenye dakika 28:54?Mleta mada ana hidden agenda.
Kwenye kauli huumba, kinachotamkwa ndicho hatari na sio watu watakutafsiri vipi.
P
 
Video kamili ya hili suala ipo hapa naomba tuiangalie

Je 16sec ni asilimia ngapi ya muda wote=16/180=0.0889=8.89% asilimia zaidi ya 90 ya maongezi ya Mhesh.Bulembo haijawekwa kwenye hii clip chochezi.
Mkuu Aqua, naomba kukupongeza wewe una kipaji cha transcription, uliopaswa uwe a reporter wa hansard, au journalist, lawyer.
Haijalishi yamesemwa mangapi, as long as there was a death wish, the rest is immaterial.

Kwenye kutoa kauli, kuna just paying lip services but they don't mean what they say. Kauli za lip services haziumbi.

Kuna wanaotoa kauli expressly or impliedly but with motive behind, hizi ndizo kauli hatari sana. Hata utafute siagi, jam, hata asali kutaka kuipaka kauli ya Bulembo ili kui sugar coat ionekane tamu, haitasaidia kitu, shubiri ni shubiri tuu hata uichanganye na debe la asali, bado itaichachua asali yote, Bulembo wishes Zitto to be killed, to die and be dead kama walivyowish kwa Lissu, Mungu akaingilia kati kuzuia.

Sasa wait for karma ya Zitto itakavyo mshukia Bulembo , mimi nitakukumbusha tuu. Bulembo belongs to kundi hili ila karma ina act kiajabu ajabu, sometimes waovu ndio huwa wanafanikiwa, hivyo kunaweza kutokea kitu cha ajabu, badala ya karma kuanzia kwa wazungumzaji, inaweza kuanzia kwa washangiliaji!.

P
 
Kwanini aanze na kauli hiyo ya kutaka msaliti auawe? Mifano iliisha au misemo mingine imeisha? Au kakutuma uje umtetee baada ya kuona reaction ya watu baada ya kauli yake hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu jifunze kusikiliza alisema "tukiwa kule kagera,tunapigana na uganda akitokea mtu (hajasema akitokea Zitto) akapeleka taarifa zetu upande wa pili(upande wa pili hapo alimanisha Uganda) sasa ili huo mfano uapply kwa Zitto,je Zitto alipigana vita vya Tanzania na Uganda na Je Zitto amepeleka taarifa zetu Uganda wakati wa vita?Suala la mnapokuwa vitani kama hujui mambo ya vita kawaulize wanajeshi.

Je msaliti vitani inakuwaje? Msitumie vibaya uhuru wa kutoa maoni,mtu kaanza katoa mfano,nyie mnalazimisha mfano uwe ndicho alichokikusudia pamoja na kuwaonyesha walishauri nini mwishoni akili zetu mmeziprogram walishauri auawe.Acheni hizo tabia si nzuri.Mheshimiwa Bulembo alishauri hivi

"Huyu mtu kazoea anatakiwa apate kiboko kizuri sana"

Sasa kama kiboko kizuri maana yake ni kuuawa (ninyi mwasema na siyo yeye ) na siyo adhabu hapo mtakuwa sahihi kwa mujibu ya kamusi yenu mpya.Tuache ushabiki usiokuwa na tija kwa taifa,unapofanya uamuzi kuwa fair usiendeshwe na hisia,video iko "crystal clear".Hapo hata huwezi kumshitaki mtu,kwa sababu hajasema.

Huu mwaka tutaona na kusikia mengi.Iangalie video tena usiwe na haraka ya kujibu.Tagu lini mfano uchukuliwe ndiyo kitu halisi ambacho mtu amekusudia? Msiendeshwe na hisia zetu na mitazamo yenu ,penye ukweli mkubali.Kwa nini mtu alete video in sekunde 16? Kama utahukumu kwa haka ka clip unshida,ndiyo maana nilipoona moyoni nilijua kuna kitu hakiko sahihi nikatafuta video yote.Acheni kuwapotosha watu.
 
Aqua, Mkuu, huwezi kuyatumia maji kama mfano wakati unauzungumzia unga, itakuwa ni *irrelevant*

Kwani kuna vita ya tz na Uganda sasa hivi? Linajadiliwa suala la Zitto, jee Zitto ni mwanajeshi? Kazitoa taarifa zozote kuzipeleka Uganda?

Mkuu, tuna akili timamu kabisa wala msitake kutufanya wajinga na mazumbukuku, tumekielewa vizuri kabisa alichokimaanisha katika huo mfano wake na kama wewe unataka kutulazimisha tuamini kile unachokiamini regardless kiko sahihi au laa basi umechelewa.

Kuna kitu kinaitwa '*events chronology*', zilishawahi kusemwa kauli za mfano huo au kama hizo na yaliyotokea kila mmoja ni shahidi, na kumbuka TL hakuwa mwanajeshi au mpiganaji na huyo alokautoa huo mfano wala hakumtaja TL kuwa ndiye mkusudiwa, ila you and I we know what came after that.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wagotheleopardskiller,
Toa ushahidi wako kutoka kwenye video usilete mawazo yako na kulazimisha yawe ya muongeaji.
Kama "kiboko kizuri sana" maana yake ni kuuawa ndugu utakuwa sahihi otherwise hauko sawa.See the reality and not what you want to see.
 
Aqua, Tafsiri yako ya kipuuzi. Kama mfano wake haukumlenga Zito, kwa nini autoe anapojadiliwa Zitto?

Kauli inayofanana na hii, ilitolewa dhidi ya Lissu, kilichofuatia sote tunajua. Shetani siku zote kazi yake ni kuua. Akishindwa kuua roho huua mwili.

Anayefurahia kuua ama ni shetani au wakala wa shetani
 
Bams,
kama tafsiri yangu ni ya kipuuzi kwa mtazamo wako ibadilishe unavyotaka iwe ila utakuwa umesema wewe na siyo mimi.

Unaponiuliza mimi kwa nini atoe mfano huo akiwa anajadiliwa zitto,unategemea mimi nikujibu nini?Mtafute aliyeutoa umwulize kwa nini alitoa mfano huo,yule ni mtu mzima mimi siwezi kumsemea katika hilo.
Aliyekuambia shetani anaweza kuua Roho ni nani?Kasome tena biblia yako au rudi darasani.
 
Naona ushabiki umekutawala mkuu huwezi kuuona upande wa pili.

Ngoja tusubiri muda utatupa tafsiri ilo sahihi zaidi.
Toa ushahidi wako kutoka kwenye video usilete mawazo yako na kulazimisha yawe ya muongeaji.
Kama "kiboko kizuri sana" maana yake ni kuuawa ndugu utakuwa sahihi otherwise hauko sawa.See the reality and not what you want to see.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom