VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Kazi ya ulinzi ni kazi ngumu sana , Mungu amfanyie wepesi na pia mheshimiwa Rais ampe kitengo kingine ili apumzike hata hivyo nimependa utimamu wake kaulazimisha lakini mwili umeshindwa kuhimili .
 
Kupata nafasi kama hii ni bahati pengine aliugua siku nyingi akaona ajikaze hivyohivyo ili asijeakapoteza nafasi hiyo,pamoja na ndumba na ngai nazo zinaweza zikachangia kutoka kwa washindani wake.
 
Mbona hii hali inaweza kutokea tu msikuze mambo
Kupata nafasi kama hii ni bahati pengine aliugua siku nyingi akaona ajikaze hivyohivyo ili asijeakapoteza nafasi hiyo,pamoja na ndumba na ngai nazo zinaweza zikachangia kutoka kwa washindani wake.
N
 
Labda Jana yake kakesha klabu na mipombe, inapaswa waliopangiwa kusimama na rais wanakaa sehemu ikulu Jana yake bila raha au mbwembwe zozote.
Dah😂😂😂😂😂😂😂
Ingekuwa ni Mtanzania ningesema ila watz siyo watu
Wakenya mnatoa wapi tabia hizi za kitanzania?
 
Yule mlinzi alianza kuonekana hayuko sawa, nilitegemea ma cameraman wa ikulu wangeanza kuligundua mwanzo kabisa na kuwapa taarifa wenzao sababu probably lazima watakuwa ni watu wa usalama,

japo huyo camera man wa hii video aligundua ila hakua na uhakika na mashaka yake.

Ujue hapo kuna walinzi wa rais Samia Hassan timu nzima ilitakiwa waione lugha ya mwili ya mwenzao mapema, pamoja ya kuwa mpambe (Aide De Camp) alinongonezwa na aliyepata kadhia ilitakiwa mkuu wa timu ya ma bodyguard kuchukua hatua za haraka.

TOKA MAKTABA:
Mfano clip ya Rais Obama tayari watu wa usalama walio na kumtonya Obama nyuma yako kabisa kuna tukio ila mheshimiwa usipaniki, Obama akageuka na kumfariji aliyekumbwa na mfadhaiko

TEAM NZIMA YA MA - BODYGUARD WAKISOMA LUGHA YA MWILI WA KILA ALIYE KARIBU NA RAIS OBAMA

Umakini wa mawasiliano siri kukitokea changamoto, rais Obama apelekewa ujumbe siri ofisa kuwa nyuma yake mwanamama lugha ya mwili wake anaonekana hayupo sawa, rais Obama anageuka


View: https://m.youtube.com/watch?v=CbSFw7NTneQ

Umakini na teamwork (ufanyaji kazi kama timu) uliweza kugundua lugha ya mwili (body language) ya kiwingu cha watu walio jirani ya rais na hatua zikachukuliwa kwa spidi kubwa ..
 
Polee sana Dada, hope atapewa tiba sahihi na pumziko pia.
 
Itabidi mlinzi aliyepata mfadhaiko Dodoma apitie vipimo vyote muhimu kabisa kujua undani wa kadhia yake.

Vipimo vinalenga utimamu wa maeneo mengi, ikiwemo uwezo wa kuhimili ongezeko la kazi na mbinyo (pressure) wa hali nyumbani, kazini, itikadi za No Reforms No Election 2025 n.k listi ni ndefu mno ili yeyote aliye katika kiwingu kinachomzunguka rais kusiwepo na shaka ya upungufu katika mambo yote bila kuacha kitu kukosa majibu.
 
Back
Top Bottom