VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

VIDEO: Mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Itakuwa naye anashauriwa na Prof Janabi kuhusu afya na lishe.
 
Tazama mlinzi wa Rais Samia alivyotaka kudondoka wakati Rais akihutubia

Tukio hili limetokea leo Aprili 5, 2025, Dodoma, wakati Rais Samia Suluhu Hassan akizundua majengo ya mahakama ya Tanzania.

View attachment 3294214
Inawezekana ikawa ni uchovu kutokana na aina ya kazi ulinzi wa viongozi, hivyo kukosa nafasi ya mapumziko au kutopata vimiminika kama maji n.k vya kutosha mwili usizimike.
Kitaalamu hii hali ya kudondoka ghafla inaweza kusababishwa na:

-sukari kushuka (hypoglycemia)

-presha ya damu kushuka (hasa kwa mtu anayesimama kwa muda mrefu au kusimama ghafla: orthostatic hypotension)

-matumizi ya aina fulani za dawa

-upungufu wa maji mwilini (dehydration)

-hali ya kihisia mfano hasira, maumivu, uchovu nk

-maradhi mengine kama vile matatizo ya moyo nk
 
Si huyo tu. Hata mlinzi wa Prince Charles wa Uingereza yeye alipiga chini na alizimia kabisa. Mlinzi wa Ruto aliporomoka toka kwenye mlango wa gari ikikimbia hadi chini na kubiringita kama tairi. Binadamu tuna mbwembwe kibao ila ukweli tuna ukomo wa kila kitu kuanzia afya, uhai na umri.
Huyo hakuwa mlinzi (Bodyguard)wa Prince charles alikuwa royal guard alidondoka kwenye parade.
1743866949823.png
 
Labda Jana yake kakesha klabu na mipombe, inapaswa waliopangiwa kusimama na rais wanakaa sehemu ikulu Jana yake bila raha au mbwembwe zozote.
Hizo ni pombe nyingi, kukosa chakula cha kutosha na maji...Hakuna kingine!
 
Ni mambo ya kawaida kwa binadamu, majukumu yake ya kusimama mda mrefu, huenda kuna wakati pressure inashuka ghafla hivyo kusababisha ubongo kukosa oxygen ya kutosha.

Anaweza kupata hali hiyo mtu yoyote. Pole yake.
Kweli kabisa. Pole sana kwake
 
Back
Top Bottom