Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha

Mkuu, Linipokuja suala la serious kama kutetea uhai wa mtu kwanini tu-coclude kwa ku-guess??

Hao watu wanaoshuhudia hilo tukio kwanini wasingehoji huyo mtu amefanya nini mpaka achukuliwe hatua kama hiyo??

Vyombo vya dola si vipo?? kama kuna utata juu ya sababu iliyosababisha haya yote kutokea watu wanaoshuhudia hili tukio wangeshirikisha vyombo vya dola tu, kuliko kumuacha mtu anachukuliwa anapopelekwa hapajulikani, alichofanya hakijulikani na waliomchukuwa hawajulikani. Ni hatari sana
Huyo atakuwa ni mwizi tapeli au anabeba wake za watu na watu wa aina hii ni WA kuwashugulikia ipasavyo bila kuwaonea huruma
 
Masuala haya ya kutekana hapa Tanzania jinsi yanavyofanyika ni kama vile ilivyokuwa nchini Zaire (DRC) enzi za Utawala wa Dikteta Mobutu Sese Seko, Watu walikuwa wanatekwa mchana kweupe kama hivi wanavyofanya hawa Watekaji kwenye video hii. Nchini Zaire ilikuwa ukitekwa namna hiyo basi utapelekwa moja kwa moja nyumbani kwake Rais Mobutu Sese Seko kwenye makazi yake yaliyopo katika Kijiji Cha Gbadolite ili ukateswe na kisha kuuawa. Hali ilikuwa mbaya sana kupita kiasi nchini Zaire, naona hali kama hiyo hiyo sasa hivi ipo nchini Tanzania. Ni hatari kubwa sana kwa Usalama wa Umma na nchi yote kabisa kwa ujumla wake.
Matukio ya namna hii yana madhara mabaya sana ambayo kamwe hayataweza kuja kurekebishika.

Nashangaa Sana kuona kwamba Serikali iliyopo ipo kimyaaa kabisa licha ya kwamba vilio vya Wananchi ni vikubwa sana katika kulaani matukio ya namna hii. Kulikoni hasa huko Serikalini?
Tulishaliona hilo

Ova
 
Inasemekana kwamba tukio limetokea jana (20.2.2025) majira ya saa saba mchana.Mkoa wa Pwani, Kibaha, Njuweni, sheli ya Puma.

Huyu kijana (boda boda) alikuwa anapambania maisha yake, akaomba msaada. Wananchi waliposogelea eneo la tukio, alishuka dereva wa hiyo Noah nyeusi ya watekaji akiwa na mtutu wa bunduki (kama inavyoonekana kwenye video), watu ikabidi warudi nyuma.

Boda boda akafungwa pingu kwa kusumbuana nao sana. Wakaanza kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Boda hakukubali kirahisi mpaka alipotolewa bastola na huyo aliyevaa vest nyekundu.

Ila inasiikitisha hapo nyuma ya kituo hiko cha mafuta kina kituo cha polisi na hata mbele kule kama unaenda kituo cha nida(lolioondoll)
 
Hivi watu walishindwa kabisa kuwashughulikia hao watekaji.mnashindwa hata kutoboa matairi
Inasikitisha yaani gari imeondoka ,amebaki jamaa mmoja peke yake lakini wamemuacha ,asieee SISIEMU endeleeni kutawala tu mpaka mwisho wa dunia maana hamna watu ni mazezeta tu.
 
Inasikitisha sana ila Kwa kuwa Mnafunda mashoga sawa endeleeni kwa kweli Mtu anakuonyeshea bunduki unazani kwani atakupiga nayo hiv watu wote mkiwasonga songa hawo hamjui watatulia acheni uoga ninyi watu
Wanafunda Mashoga????
Kwa hiyo unataka kusema kwamba huyo bodaboda anayetekwa kwenye video hii ni shoga ambaaye antakiwa kwenda kufundwa? Kwa hiyo hao Watu wengine wote wanaotekwa ni maahoga ambao wanatakiwa kwenda kufundwa?

Unataka kusema kwamba sasa Mashoga wamekuwa Watu hatari zaidi kiasi kwamba njia pekee za kuweza kushughulika nao ni kuwateka? Is it?

Kwa Nini Mafisadi wa rasilimali za nchi nao hawashughulikiwi kwa njia hiyo hiyo ya kuwateka na kuwaua?
 
Mkuu kafanya nn ili tuache kumtetea. Kama kabaka au kaua tujuze basi, badala kutuacha njia panda
89% bodaboda wengi hufanya michezo michafu nyuma ya hizo kazi za boda boda wanazofanya nilishawahi kuwapa kazi bodaboda 20 ya kuendesha hizo boda kati ya hizo 2 tu ndio zilimaliza mkataba vyema hizo zilizobaki zote zilikumbwa na kadhia ya matukio yao ya ajabu ajabu waliyokuwa wanafanya ikiwemo wizi, utapeli , kungonoka na wake za watu , mabinti wa shule na girlfriends za watu so kabla hujamuonea mtu huruma think logically ndio uamue critically
 
Wakati utekaji unaendelea,toboeni tairi,wakati wanaziba pancha pigeni simu polisi.
Hapo mwenye Lori mmoja anajitoa ufahamu anawaoelekea Lori lote.

Alafu anashuka anakimbia wananchi wanamaliza kazi.

Hayo ndo matunda ya CCM kututengenezea kizazi cha watu wasiofikiri vizuri zaidi ya uchawa, kujipendekeza, starehe na umbea.

Amini maneno yangu. Nchi yetu ishajifia hiyo. Tusubiri kuzikwa tu kama Congo.
 
Inasemekana kwamba tukio limetokea jana (20.2.2025) majira ya saa saba mchana.Mkoa wa Pwani, Kibaha, Njuweni, sheli ya Puma.

Huyu kijana (boda boda) alikuwa anapambania maisha yake, akaomba msaada. Wananchi waliposogelea eneo la tukio, alishuka dereva wa hiyo Noah nyeusi ya watekaji akiwa na mtutu wa bunduki (kama inavyoonekana kwenye video), watu ikabidi warudi nyuma.

Boda boda akafungwa pingu kwa kusumbuana nao sana. Wakaanza kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Boda hakukubali kirahisi mpaka alipotolewa bastola na huyo aliyevaa vest nyekundu.

JamiiForums imewasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase kuhusu tukio hilo, amesema:

"Sina taarifa kamili juu ya tukio hilo, nami naliona tu, naomba mtupe muda tulifuatilie na tufanye uchunguzi wa kujua kilichotokea."
Duuh haya mambo kwa serikali ya CCM sio ya kushangaza
 
Kungekua na utawala unaofata sheria haya mambo yasingekuwepo ila ndio ivyo tena.
Mtu anahofia kuingilia huo ugomvi isijekua ni ugomvi wa ndugu tu.
 
Wanafunda Mashoga????
Kwa hiyo unataka kusema kwamba huyo bodaboda anayetekwa kwenye video hii ni shoga ambaaye antakiwa kwenda kufundwa? Kwa hiyo hao Watu wengine wote wanaotekwa ni maahoga ambao wanatakiwa kwenda kufundwa?

Unataka kusema kwamba sasa Mashoga wamekuwa Watu hatari zaidi kiasi kwamba njia pekee za kuweza kushughulika nao ni kuwateka? Is it?

Kwa Nini Mafisadi wa rasilimali za nchi nao hawashughulikiwi kwa njia hiyo hiyo ya kuwateka na kuwaua?
Achana na huyo mpumbavu wa CCM. Wameshatuharibia hili Taifa. The only way out saivi tusali atokee huko JWTZ mwanajeshi afanye ya Kepteni Traore tu nchi irudi kwenye mstari.
 
Inasemekana kwamba tukio limetokea jana (20.2.2025) majira ya saa saba mchana.Mkoa wa Pwani, Kibaha, Njuweni, sheli ya Puma.

Huyu kijana (boda boda) alikuwa anapambania maisha yake, akaomba msaada. Wananchi waliposogelea eneo la tukio, alishuka dereva wa hiyo Noah nyeusi ya watekaji akiwa na mtutu wa bunduki (kama inavyoonekana kwenye video), watu ikabidi warudi nyuma.

Boda boda akafungwa pingu kwa kusumbuana nao sana. Wakaanza kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Boda hakukubali kirahisi mpaka alipotolewa bastola na huyo aliyevaa vest nyekundu.

JamiiForums imewasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase kuhusu tukio hilo, amesema:

"Sina taarifa kamili juu ya tukio hilo, nami naliona tu, naomba mtupe muda tulifuatilie na tufanye uchunguzi wa kujua kilichotokea."
Saizi kutekwa sio habari ya kutisha tena.
Life speed
 
Hapo mwenye Lori mmoja anajitoa ufahamu anawaoelekea Lori lote.

Alafu anashuka anakimbia wananchi wanamaliza kazi.

Hayo ndo matunda ya CCM kututengenezea kizazi cha watu wasiofikiri vizuri zaidi ya uchawa, kujipendekeza, starehe na umbea.

Amini maneno yangu. Nchi yetu ishajifia hiyo. Tusubiri kuzikwa tu kama Congo.
Ajitoe ufahamu kuharibu Mali ya watu kisa kumtetea mwizi tapeli au mbeba wake za watu akili huna
 
Kwa hiyo chini ya utawala wa Sheria mtu akichukua mke wa mtu ndo anatekwa? Endeleeni tu kuliharibu hili Taifa yakiwarudia msiseme hamkuonywa.
 
Unataka mtu anaebeba wake za watu apewe zawadi Gani Kwa ushababi wake tofauti na hiyo ya kuwekwa mtu kati na wahuni
 
Huyo atakuwa ni mwizi tapeli au anabeba wake za watu na watu wa aina hii ni WA kuwashugulikia ipasavyo bila kuwaonea huruma
Kwenye hiyo video, inaonekana hata mashuhuda hawajui huyo dreva wa pikipiki amefanya kosa gani. Na wao wana assumptions kwamba jamaa ni mwizi, tapeli au anabeba wake za watu.

Assumptions za upande mmoja kuonyesha tu dreva pikipiki ana hatia.

vipi kama hao wanaomteka ndio matapeli? wezi? au ni watu wenye nia yoyote mbaya tu kwa dreva pikipiki?

Kwanini hao mashuhuda wasiingilie kati kujua ukweli kulikoni kwenye hilo tukio, kuliko kubakia na fikra za upande mmoja kwamba ni dreva pikipiki ndio mwenye hatia??
 
Waingilie kati kwani linawahusu yaani watu waache kutafuta pesa waongilie ugomvi usiowahusu
 
Back
Top Bottom