Inasemekana kwamba tukio limetokea jana (20.2.2025) majira ya saa saba mchana.Mkoa wa Pwani, Kibaha, Njuweni, sheli ya Puma.
Huyu kijana (boda boda) alikuwa anapambania maisha yake, akaomba msaada. Wananchi waliposogelea eneo la tukio, alishuka dereva wa hiyo Noah nyeusi ya watekaji akiwa na mtutu wa bunduki (kama inavyoonekana kwenye video), watu ikabidi warudi nyuma.
Boda boda akafungwa pingu kwa kusumbuana nao sana. Wakaanza kumlazimisha kuingia kwenye gari.
Boda hakukubali kirahisi mpaka alipotolewa bastola na huyo aliyevaa vest nyekundu.
JamiiForums imewasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase kuhusu tukio hilo, amesema:
"Sina taarifa kamili juu ya tukio hilo, nami naliona tu, naomba mtupe muda tulifuatilie na tufanye uchunguzi wa kujua kilichotokea."