Uchaguzi 2020 Video: Mwangalie Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kisha toa maoni yako

Uchaguzi 2020 Video: Mwangalie Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kisha toa maoni yako

Wengine tumepiga kelele mara kadhaa tugombee kwanza tume huru badala ya kugombea au kupigania vyeo, lakini wapi! Upinzani uliopo si rahisi kuleta mabadiliko ya kweli maana nao wanapenda sana vyeo kuliko kurekebisha kwanza mifumo yetu ya uchaguzi
 
Tena aliyechukua hii video ni mccm mwenzao, something is wrong within the system. Muda ni mwalimu
 
Umesema ukweli japo hauungwi mkono na wengi, hasa wanaopenda kupigania vyeo badala ya kupigania mabadiliko ya mifumo yetu huru ya uchaguzi
Miaka yote nimewaambia wapinzani, piganieni tume huru. Bila tume huru ni kutwanga maji kwenye kinu tu. Yaani hata baada ya kituko cha Jecha, bado wapinzani waliridhika tu! Wakatulia kimya mpaka leo 2020!
 
Habari wadau wa siasa na wanademokrasia wote.

Nimekutana na video ambayo ninaiweka hapa na kusikitika sana. Huyu ni mkurugenzi wa time ya Uchaguzi Tanzania NEC ambaye bila kupeprsa macho anaonesha asivyo fair kabisa. Hivyo basi napendekeza yafuatayo:
1. Ajiuzuru wadhfa wake au afikuzwe kwa kukosa maadili.
2. Maamuzi yote aliyoyafanya au aliyoshiriki kuyafanya au kuyafikiwa yachunguzwe na yatenguliwe.
3. Ashitakiwe kwa matumizi mabaya ya ofisi.
4. Time ituhakikishie namna itavyohakikisha uchaguzi unakuwa wa hali.

Watanzania wenzangu tumefikia pabaya sana kama taifa naomba tupaze sauti.
 
Wapwa,

Sina mengi, hii ndo tume yetu ya uchaguzi, hata upinzani ukishinda kwa asilimia 100%, ni ngumu kutangazwa.

Ruge aliwahi kusema: "Ogopa Mungu na Teknolojia"

Toa maoni

Swali la msingi la kujiuliza ni je wakati anayasema hayo alishateuliwa kuwa mkurugenzi wa uchaguzi? Sisi wananchi tuna imani nae msiemtaka shauri yenu sisi tunasonga mbele
 
Huyu bora anyamaze tu, maana bado watu wanahasira nae
 
Hivi tunaweza kupata MTz ambaye ni neutral kabisaaa,
Labda atoke sayari nyingine.

Issue sio tume ni Katiba.

Umeliona sawa sawa kabisa!! Tume yetu ina matatizo katika muundo, sio kazi zake!! Jinsi inavoundwa ndio swala la msingi. Inaundwa kwa namna ambayo muundaji anaifanya iwe chini kuliko maamuzi ya tume! Tume inakuwa ni rubber stamp ya matakwa ya muundaji!! Hakuna professionalism wala integrity - kuna political influence katika kazi za tume!
 
Back
Top Bottom