Uchaguzi 2020 Video: OCD wa Hai amwambia Mbowe hata afanyeje hawezi kumshinda mgombea wa CCM Hai

Tunaambiwa tuogope sana Techinolojia pamoja na Mungu, Ile Video inaweza onekana ni ishu ndogo sana ila ile Video ni ushahidi ulio shiba kabisa, Ule ni ushahidi mkubwa sana kwa Upinzani.

CCM na Police wanaweza ona ni swala dogo ila ule ni ushadi,

Ile VIDEO ya Hai ni ushahidi mzito sana na Upinzani wanatakiwa kushangilia maneno yale ya OCD wa Hai.

Police kutamka kwamba hamtamshinda Magufuri huo ni ushahidi mzito sana na kwa sababu ile video haiwezi futwa tena basi tushangilie.

Video kama zile tunaomba ziwe nyingi sana
 
Huu ni ushahidi mzuri sana,lazima ulimwengu ujue jinsi polisi wanavyotumika vibaya
 
Sasa ulitaka amwambie atashinda wakati hashindi kama nyie mbavyosema mtashinda wakati hamshindi?
 
Wote mnaompongeza huyo afande akili zenu zikapimwe wajinga nyinyi!
 
Alicho kosea Afisa wa polisi ni kusema ukweli, Ata wenyewe CHADEMA wanajua kuna majimbo machachesana ambayo wanaweza wakashinda ndiomaana hata kwenye kura za urais waneshakata tamaaa kabisa.
Ni sahihi au siyo sahihi?
 
Tunasafari ndefu sana.

Magufuli ndio ameharibu kila kitu hadi democrasia ya nchi .

IGP nae yupo tu.
 
Kosa lake ni kusema Ukweli, na ukweli siku zote huwa haupendwi!

Mbowe kaambiwa ukweli kuwa hata ajipasue pasue hawezi kumshinda Magufuli [emoji23][emoji23]
Ni sahihi askari wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kufanya hicho alichikifanya?
 
Tunasafari ndefu sana.

Jiwe ndio ameharibu kila kitu hadi democrasia ya nchi .

IGP nae yupo tu.
Natarajia IGP amchukulie hatua za haraka za kinidhamu, yupo katika mavazi rasmi, live na mhusika??? Mchana mbele ya watu!? Pamoja na madhaifu mifumo yetu that's 2 much!!!
 
Sasa ulitaka amwambie atashinda wakati hashindi kama nyie mbavyosema mtashinda wakati hamshindi?
Jeshi la polisi halipaswi kuegemea upande wowote. OCD hapaswi kusema fulani atashinda wala hapawi kusema fulani hatashinda. Ni kinyume na sheria.
 
Umejibu vizuri sana..Tatizo humu watu wengi wanachangia hoja kimihemko au hisia(ushabiki) sometimes unaweza dhani kwamba hawakusoma au hawana utashi but wala Ni kujitoa tu ufahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…