Video: Polisi wampiga na kumuumiza maeneo ya kichwani muumini wa Kanisa la Gwajima

Video: Polisi wampiga na kumuumiza maeneo ya kichwani muumini wa Kanisa la Gwajima

Sasa serikali inakomalia nini kwenye kanisa hilo, si wawaachie tu waumini hao wafanye ibada yao? Wanayemtafuta hayupo hapo, sasa ya nini kuzuia wananchi wasiabudu Mungu wao?
Ni jambo la kushangaza sana.

Anaetafutwa ni Gwajima, wanapigwa wengine. Eti wanapigwa kwa sababu wameenda kusali.

Ubabe usio na maana.
 
Huu unyama huu unaoendelea Mungu atafanya jambo kubwa kama kwa lile Gaidi alilofanyizia tarehe 27/3/2021
 
Kwan hawawez kwenda kwenye makanisa mengn mpk humo tu kwenye ufufuo au ndo kuleta issue za kenya hapa!!!
 
Warumi 13

13 Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri.

6 Kwa sababu hiyo hiyo mnalipa kodi, kwa maana watawala ni watumishi wa Mungu ambao hutumia muda wao wote kutawala. 7 Wal ipeni wote haki zao; mtu wakodi mlipe kodi; na mtoza ushuru mli pe ushuru; astahilie kunyenyekewa, mnyenyekee; astahiliye hesh ima, mheshimu.


Ukiisoma niblia kama kitabu cha hadithi, unaweza kugeuka na kuwa hayawani.

Hizo verses hazizungumzii kutii mamlaka dhalimu au zinazotenda kinyume cha mapenzi ya Mungu. Bali zinaongelewa mamlaka zinazosimamia haki. Ndiyo maana Paulo anasema kuwa kama hutaki kuitii mamlaka, basi tenda yaliyo sahihi, hutaingia kwenye mgogoro na mamlaka.

Lakini ukiwa kwenye mamlaka hizi dhalimu, hata usipotenda kosa, wanaweza kukutendea uovu. Ndiyo maana unaona watu wasio na hatia wanatekwa na kuuawa.

Ukiitii mamlaka dhalimu, na ukatenda kama malaka dhalimu inavyotaka, nawe unaingia kwenye udhalimu ule na kubeba laana ya Mungu.

Biblia Inasema Nini juu ya mtawala mwovu:

Mithali 28:15-28 :

“ Kama simba aungurumaye, au dubu arukaye, ndivyo alivyo mtawala mwovu juu ya watu wasiojiweza; mtawala mdhalimu hudhulumu; bali yeye achukiaye udhalimu atatawala muda mrefu ” (28:15-16).

" Yeyote anayeteswa na hatia ya mauaji atakimbilia kaburini; mtu yeyote asimzuie " (28:17).
 
Tulipofika kama Taifa si salaam,Hao Waamini wanakosa gani wakati wameenda Kuabudu?

Sasa serikali inakomalia nini kwenye kanisa hilo, si wawaachie tu waumini hao wafanye ibada yao? Wanayemtafuta hayupo hapo, sasa ya nini kuzuia wananchi wasiabudu Mungu wao?
 
Wakuu,

Kwenye heka heka na Polisi leo, muumini wa Kanisa la Gwajima ameonekana akiwa ameumizwa maeneo ya kichwani baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Polisi. Yaani damu zinatirirka kama maji waku

Kama mnamsikia hapo kuna muumini anasema "Samia utalipa damu hii. Mama Samia popote ulipo, damu hii utailipa, utailipa damu hii. Mungu hajawahi kushindwa. Mama Samia damu utailipa hii"


Ni hayo tu wakuu!
Ila Mungu naye tusipende majukumu ambayo siyo yake. Amekupa mikono, miguu, akili na vyote unavyohitaji kwa nini tumwachie Mungu?
 
Watz tuna moyo mnoo, hakosi wakumsaidia japo kuziba jeraha ili lisizidi Kuna serious.
 
Hii Nchi ngumu sana,
Kwani wakiuachiwa wakasali kuna shida gani,
Kama issue ni Gwajima tayari ni mshirika wao kwenye chama chao na form ya kuomba ridhaa ya ubunge kupitia sacoss yao kachukua,Kwa nn kusiwe na busara kidogo tu kuliko kukomoana?
 
Ukiangalia ni kama vile upande wa watoto wa mama mdogo kama wanalipiza kisasi kimya kimya kwa yale yalotokea enzi za magomeni mwembechai na kule msikiti wa mtoro pale mitaa ya Livingstone na yale ya mwembeyanga kule temeke
 
Dini ni ulevi mbaya sana…!
Afrika tutachelewa sana kupata maendeleo na moja ya sababu ni imani za kidini..!

Kanisa limefungiwa na kuna kesi mahakamani..! Waumini mnaenda kufanya nini hapo? Mbona Kiongozi wenu haonekani kuja hapo?

Nchi hii inaongozwa kwa mujibu wa sheria..kama waumini hamkubaliani na maamuzi ya serikali utaratibu upo wazi mnakwenda mahakamani kudai haki..!

Kitendo wanachofanya hawa waumini ni kujaribu kutafuta huruma kwa jamii jambo ambalo siyo sawa na haiwezi kuwasaidia hata kidogo..!

Bado naona kama polisi wametumia uungwana sana kwenye kudeal na hawa watu..! Otherwise nguvu kubwa inaweza kutumika na watakao athirika ni waumini..!

Kuna watu wanadhani ukishakuwa muumini wa dini fulani basi una kinga ya kutofuata sheria na kwamba dini zinapaswa kuogopwa na kufanya zinavyotaka..!
 
Ukiangalia ni kama vile upande wa watoto wa mama mdogo kama wanalipiza kisasi kimya kimya kwa yale yalotokea enzi za magomeni mwembechai na kule msikiti wa mtoro pale mitaa ya Livingstone na yale ya mwembeyanga kule temeke
🤔 😳👀
 
Wakuu,

Kwenye heka heka na Polisi leo, muumini wa Kanisa la Gwajima ameonekana akiwa ameumizwa maeneo ya kichwani baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Polisi. Yaani damu zinatirirka kama maji waku

Kama mnamsikia hapo kuna muumini anasema "Samia utalipa damu hii. Mama Samia popote ulipo, damu hii utailipa, utailipa damu hii. Mungu hajawahi kushindwa. Mama Samia damu utailipa hii"


Ni hayo tu wakuu!
Lazima apigwe ili fahamu zimrudie
 
Back
Top Bottom