GE2025 Video: Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi aliyefika mahakama kuu kufuatilia kesi ya Lissu

GE2025 Video: Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi aliyefika mahakama kuu kufuatilia kesi ya Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hapo raia kumi tu wangeingia walikuwa wanawavuruga hao was3nge wote hapo na ma helmet yao.. labda wangetumia bunduki tu..

Watu wenyewe wanaonekana hata nguvu hawana..
Walitakiwa wafanye body count kila askari watu raia watano. Wawili mnakamata mguu wa kushoto na kulia wawili mnagawana mkono wa kushoto na wa kulia kisha raia m'moja anabakia anachapa ngumi za uso na za mbavu hadi acheuwe chai na maandazi aliyokula asubuhi.
 
Yani uwarushie ngumi police wa kiafrica afu usipigwe?
 
Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi nje ya mahakama, mwananchi huyu alifika kufuatilia kesi ya Mh. Tundu Lissu leo.

PGO inawaelekeza askari wote, kujiepusha na vitendo vyote visivyo vya kibinadamu au vyenye kushusha heshima ya mtu kwa mazingira yoyote kwani havivumiliki kwa Polisi yeyote anayejihusisha na vitendo hivyo.

Utendaji wa Polisi kwa jamii ni lazima uzingatie heshima kadiri mazingira yanavyohitaji. Matumizi ya nguvu kwa kila askari yanaruhusiwa na kukubalika pale tu inapolazimu katika kufanikisha malengo yenye kukubalika.

Tukio hili miongoni mwa matukio mengi ya kikatili ambayo yamekuwa yakifanywa na Polisi kwa raia, Askari zaidi ya 10 wanamshambulia kwa virungu raia asiye hata na silaha ambapo ingewezekana kumdhibiti pasipo kumshambulia kikatili bila kujali usalama na utu wake.

Kila askari anatakiwa kutumia nguvu kwa majukumu yake pale tu inapohitajika na inapobidi, na pia ni pale tu nguvu hiyo inapohitajika kufanikisha malengo ya kisheria.

Vitendo kama hivi vya kukemewa vivyofanywa na baadhi ya polisi vinaashiria unjwaji wa makusudi wa haki za binadamu pamoja na kukiukwa kwa taratibu zinazowaongoza Polisi katika utendaji wao wa shughuli za kila siku.

Pia soma: Baadhi Ya Mambo Unayohitaji Kufahamu Kuhusu Polisi

Ipo siku watesaji kama Hawa watapigwa na kuvuliwa boxier hadharani.
 
kama alipiga kweli basi safi sana, hivyo ndivyo inayotakiwa, hawa kenge hatutakiwi kuwaogopa. Wao ni woga kuliko sisi na masiliha yao, ni vile wabongo ni wapumbavu tu
 
Amenikumbusha kuna mwanangu alimrudishia kofi mwalimu😆 ninachokumbuka tuliitwa tukambebe offisini akiwa amezimia.

By the way police wanazingua sana. Kuna muda kuna feeling fulani inakuja, lolote litokee tu
Na hapo kweli uliridhika huyo/hao waalimu walifanya jambo stahiki kwa mwanao?

Je, wewe mwenyewe ungefanya nini na mwanao katika hali ya namna hiyo?

Ina maana hao walimu, au wewe mwenyewe, mmejishusha na kuwa katika ngazi ya akili za huyo mtoto; hamna tofauti kabisa na yeye?

Hao walimu walitakiwa kuwajibishwa, lakini naona wewe mwenyewe mzazi ulifurahia mwanao kufanyiwa unyama kama huo.
 
..huyo mwananchi hakuwa na silaha, na hakuonekana kuwazidi nguvu Polisi.

..hakukuwa na haja ya Polisi kumshambulia kwa namna walivyofanya.

..kilichotokea kinachafua taswira ya Polisi, mahakama, na nchi kwa ujumla.
Taswira ya nchi sasa hivi inaelezwa na "nyomi" inayo onekana kwenye mikutano ya Samia.
Nyomi hizi zinamfanya afiti vizuri kwenye model ya akina Mseveni, ambayo ndiyo inayotafutwa katika uchafuzi huu wa Oktoba.
 
Video inaonesha tukio halijaanzia hapo

Inawezekana tukio la jamaa kurusha teke lilikuja baada ya mmoja wa hao polisi kumshambulia.

Hata wewe mwenyewe ukiwaza hivi unaona ina make sense kufikiria tu huyo mtu from nowhere amewakuta polisi ghafla tu akaanza kuwarushia mateke?
 
Yani mi ningekua polisi ningehakikisha nimemvunja huo mkono aliorushia ngumi ana bahati sana yuko Bongo , angekutana na polisi wa USA sahivi kashachapwa risasi nyumbani kwao kumefungwa maturubai
 
Back
Top Bottom