GE2025 Video: Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi aliyefika mahakama kuu kufuatilia kesi ya Lissu

GE2025 Video: Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi aliyefika mahakama kuu kufuatilia kesi ya Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Nguvu wazipatie wapi wakati mafunzo hawafanyi kwasababu kazi zenyewe hizi wanapewa kwa connection

Na hapo sio tu watu kumi.

Hata jamaa mwenyewe hakuamua tu kujihami kwa ile dhana ya kuamini kuwashambulia maafisa usalama ni kuingia kwenye matatizo zaidi.

Ila angeamua kumchapa mmoja kikombe cha maana, hao wasng wengine wangerudi nyuma.
View attachment 3472559
Rahisi sana kujiongelesha kuliko kutenda ndugu zako hata maiti yako wasingeweza kuiona.

Hii ni Tanzania sio U.S
 
Zile vurugu za uchaguzi miaka ya 2010, askari mmoja na helmet lake si akajikuta yeye ni komando...
Akaruka ukuta na kutoka nje ya jengo la manispaa eti anawafuata raia walipo, kumbe raia wanamlia timing..
Ile amefika tu raia wakampokea, jamaa mmoja akamlamba mtama wa nguvu halafu askari alivyokwenda chini, jamaa akamkanyaga kichwani halafu anawaambia wenzake "hamna mwenye kisu hapo?"... 🤣 🤣

Polisi kusikia habari ya kisu na hivi kakanyagwa chini kama mbuzi inayotaka kuchinjwa... polisi alipambana kuamka alivyopata upenyo alikimbia hio speed utadhani Hussein Bolt..🤣

Hio nilishuhudia kwa macho yangu... Wale Gen Z wa miaka ya 2005 - 2010 walikuwa wamevurugwa haswa..
Nadhani wengi wao sasa ni watu wazima na wengine wana familia... nadhani ndio kizazi cha mwisho ambao walijitambua sana...
Mbowe na Lowassa waliua kila kitu baada ya kutuliza hali pumbavu zao CCM tulikuwa tunaiongoa na damu nyingi ingemwagika for first time hapa nchini
 
Wachana na PGO,hata kama wanaisoma usiwaamini sana uwezekano wa kuipuuza ili wakuvunje ni 99%.
Kabisa Mkuu

Hakukuwa na ulazima kumpiga vile mtu ambaye hana silaha yeyote isipokuwa kuja kusikiliza kesi Mahakamani
 
Hatucheki na kima ukiruhusu kima wajikusanye kwa wingi shamban utavuna mabua
Nimeshindwa kupita kimya kimya; lakini hata la kujibu linanipa shida kubwa kulipata!

Labda niseme tu kuwa nimepata fursa ya kukusoma mara ya kwanza kabisa, humu JF, mkuu 'Kindus'.

Pongezi kwenu "msio cheka na kima..."
 
Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi nje ya mahakama, mwananchi huyu alifika kufuatilia kesi ya Mh. Tundu Lissu leo.
Hawa jamaa na uwingi wao hivyo walishindwa vipi kumdhibiti kwa kumkandamiza chini na kisha kumfunga pingu..?

Mbona inakuwa kama walitumwa kuambiwa, nyie msitumie akili zenu vyema, bali pigeni tu kama nguruwe yeyote anayepita mbele yenu..??

Kama hawa jamaa waliamua kuwa polisi, basi wanapaswa kutambua kuwa ktk majukumu yako watakutana na watu wa kila aina ambao kwa mawazo yao watatakiwa kuwa-arrest....

Swali ni je, kila anayekuwa na ukorofi wa aina fulani kwenye arresting process yao basi, suluhu ni kutumia mbinu hii ya kijinga kupambana na mtu huyu ambaye kiukweli (kwa huyu anayeonekana hapa) hata ukimtazama tu utamwona kabisa kuwa ni raia wa kawaida, hakuleta ukorofi wowote, hakuwa na silaha yoyote, isipokuwa labda walikuwa wanarusha maneno ya kuwakera tu hawa polisi...

Lakini, kwanini ukerwe na maneno kisha wewe polisi uamue kuvunja sheria waziwazi hivi..??

Nchi zingine zinazoheshimu sheria sawasawa, hawa polisi wote waliohusika kwenye tukio hili na aliyewatuma (commanding officer) wao, wangenyea debe lupango kesho tu...

Lakini kwa serikali yetu hii imeoza na kunuka uvundo tu, itachukua muda kidogo kwa hawa askari kuja kupokea hukumu yao....

Aaarrrgh😁😁😁😁, honestly, this is the stupidity of the impunity of the highest level from the TanPol...

Ipo siku kila tendo ovu litalipiwa gharama yake lazima...!
 
Excessive use of force & violence, huo upigaji si sawa.
Kama amevunja sheria si akamatwe na kuchukuliwa hatua stahiki.


Nje ya mada kidogo:
Watu wakija kuhudhuria kesi, na ikitokea wamekua wengi kuliko nafasi iliyopo ndani ya chumba cha mahakama, hivyo kuombwa kuondoka, lakini wakagoma. Nini inabidi kifanyike?

..wanatakiwa waachwe ilimradi hawaleti vurugu.
 
Polisi zaidi ya 10 wakimshambulia mwananchi nje ya mahakama, mwananchi huyu alifika kufuatilia kesi ya Mh. Tundu Lissu leo.
1000226909.jpg
 
Hii ni moja ya dalili ya anguko la Serikali,Serikali ya wananchi haiwezi kuruhusu jambo kama hili kamwe
 
Nimeshindwa kupita kimya kimya; lakini hata la kujibu linanipa shida kubwa kulipata!

Labda niseme tu kuwa nimepata fursa ya kukusoma mara ya kwanza kabisa, humu JF, mkuu 'Kindus'.

Pongezi kwenu "msio cheka na kima..."
Aise
 
Hivi hawa polisi wameshindwa kabisa kuwekeza kwenye matumizi ya akili zaidi kwenye karne hii ya 21, badala ya nguvu na ubabe usio na ulazima! Inakuwaje kwenye dunia ya leo bado tuna polisi wa aina hii!
Labda woga
 
Excessive use of force & violence, huo upigaji si sawa.
Kama amevunja sheria si akamatwe na kuchukuliwa hatua stahiki.


Nje ya mada kidogo:
Watu wakija kuhudhuria kesi, na ikitokea wamekua wengi kuliko nafasi iliyopo ndani ya chumba cha mahakama, hivyo kuombwa kuondoka, lakini wakagoma. Nini inabidi kifanyike?
Wanatakiwa kuwawekea screen nje na spika wasikilize kesi ya mwenyekiti wao. Waondoke waende wapi sasa ebo?🤔
 
Hivi hawa jamaa wanasoma hata PGO zao kweli?

Wanampiga Mwananchi kiasi hicho, ambaye hana hata silaha

Kuna haja, hili jeshi likavunjwa tuanze kuajiri upya
Wanaelewa sasa hata maana ya PGO. Hapo ukimwambia nipe maana ya PGO watakwambia ni Piga gumi ololooooooooo
 
Back
Top Bottom